Mkuchika: Hakuna Mafao Kwa Waliogushi Vyeti

Mkuchika: Hakuna Mafao Kwa Waliogushi Vyeti

This is very unfair.

Mtu amewafanyia kazi miaka na miaka, halafu mwishoni mnataka mumdhulumu stahiki yake kwa kisingizio cha cheti. Tena wengine mliwapandisha hadi vyeo kutokana na utendaji wao.
Kwenye hili Serikali wako sahiii, Hao watu mnaowatetea ni wezi kama wezi wengine too bad ni wezi wa kitaaluma.
Huyo Nesi/Daktar hadi hapo alipofikia baada ya kukamatwa unaweza kuta ameua wagonjwa wengi tu kwa ujinga wake kuhusu taaluma hiyo siku za mwanzoni.
Kuwafikilia hao wezi wa taaluma (walipaswa kuwa jera kwa kughushi) maana yake kuhalalisha wezi wengine wengi siku za usoni.
 
Kuna jambo moja sielewi. Watumishi wapo wale waliokuwa wanachangia mifuko ya jamii kama PSPF, LASPF, NSSF nk na walikuwa wanakatwa 10% ya mapato yao na seikali ilikuwa inaweka hiyo 10% nyingine.
Ok, sasa inakuwaje kuhusu hiyo 10% ya fedha zilizokuwa zinachangiwa na mtumishi kwa jasho lake nani anazichukua? kama
zinachukuliwa nazo serikalini huo sasa ni uporaji wa serikali wa wazi kabisa.
 
Kama hafai kupewa mafao wafute na kazi zao walizozifanya kwa kutumia vyeti feki,ikiwa ni haramu kuwapa mafao yao kwa kuwa walikuwa na vyeti feki hata kazi zao walizofanya ni haramu.
 
Mkuchika apigilia msumari malipo ya mafao kwa walioghushi vyeti

Kwa ufupi

Hakuna atayelipwa hata kama alibakiza mwaka mmoja kustaafu

Dodoma. Kwa mara nyingine tena, Serikali imeendelea kupigilia msumari kwa watu walioondolewa kwenye utumishi kutokana na vyeti feki kwamba hakuna malipo yoyote watakayolipwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ambaye amesema hakuna malipo yoyote wanayodai.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Haida Kenani, aliiomba Serikali kufikiria upya ni kwa nini isiwalipe hata watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu.

"Tatizo la Serikali mnaangalia vyeti hamuangalii taaluma ya watu na hata wabunge wengine mlifundishwa na hao lakini mnawatosa ni kwa nini,” alihoji Kenani.

Mkuchika alisema katika hali ya kawaida mwajiri alipowaajiri watumishi hao walionyesha kuwa na elimu stahiki na hivyo walipata mishahara kulingana na viwango vyao vya elimu wakati ni kosa.

Alisema sheria haimruhusu mtu kulipwa wakati inajulikana amedanganya.

Chanzo: Mwananchi Online
Mbona DAB anaendelea kupokea kodi zetu kama mshahara?
 
kele uwiiiiiiii starehe nilizipeenda ila sikujua mwisho wake ndo huu
 
Mkuchika apigilia msumari malipo ya mafao kwa walioghushi vyeti

Kwa ufupi

Hakuna atayelipwa hata kama alibakiza mwaka mmoja kustaafu

Dodoma. Kwa mara nyingine tena, Serikali imeendelea kupigilia msumari kwa watu walioondolewa kwenye utumishi kutokana na vyeti feki kwamba hakuna malipo yoyote watakayolipwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ambaye amesema hakuna malipo yoyote wanayodai.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Haida Kenani, aliiomba Serikali kufikiria upya ni kwa nini isiwalipe hata watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu.

"Tatizo la Serikali mnaangalia vyeti hamuangalii taaluma ya watu na hata wabunge wengine mlifundishwa na hao lakini mnawatosa ni kwa nini,” alihoji Kenani.

Mkuchika alisema katika hali ya kawaida mwajiri alipowaajiri watumishi hao walionyesha kuwa na elimu stahiki na hivyo walipata mishahara kulingana na viwango vyao vya elimu wakati ni kosa.

Alisema sheria haimruhusu mtu kulipwa wakati inajulikana amedanganya.

Chanzo: Mwananchi Online

TWO QUSTIONS:

- Is there a way wanaweza wakawarudishia utendaji wao maana kuna value serikali imepata toka kwao
- Kuna namna wanaweza kuwawajibisha watu waliowaajiri? maana the same serikali ndio imewagundua

UONEVU at WORK
 
Wacha tuisome namba wote
 
Dhumuni kuu la mifuko ya jamii ni kumsaidia mfanyakazi aweze kuendeleza maisha yake baada ya ajira yake kufikia kikomo ili ASIJE KUWA MZIGO KWA SERIKALI ktk maisha yake ya uzeeni.
Sasa kutowalipa mafao yao (pesa ni za kwao si mikopo), serikali itakuwa imeepuka vipi hiyo mizigo ambayo imejibebesha kwa makusudi kabisa.
Nadhani busara itumike hapa la sivyo tutashuhudia vifo vingi sana vilivyosababishwa na serikali yetu. Mungu hapendi.
Kibaya zaidi wengine unakuta alishabakiza mwaka au miaka isiyozidi 2 astaafu.
Jinsi familia zao zitakavyoteseka ndo laana itakavyozidi kuwakuta wale wote waliohusika ktk maamuzi hayo.
Mungu apishe mbali

Baadhi ya wafanyazi wana vyeti halali ambavyo hawajavisomea. Hiyo ndio bongo!
 
Kwanini serikali inatunga sheria kandamizi zidi ya wananchi wake? Hela uchangie vizuri then wakudhurumu .! Mungu tusamee wa Africa nadhani kuna mahali tulikukosea.
 
Back
Top Bottom