Mkt makini wa TLP Taifa Mhe. Dk Augustino Lyatonga Mrema anaendelea na ziara yake mikoa ya Arusha na K'njaro kukutana na watiania wa Ubunge na Udiwani

Ze Bulldozer

JF-Expert Member
Jun 12, 2020
1,002
525
Wakati chama chetu kikiendelea kujipanga sawasawa katika mtanange Wa Ubunge na Udiwani katika majimbo yote 264 na kata zote 3,956 Mkt. wa Chama ameongea na watia nia wa Ubunge/Udiwani jimbo la Arusha Mjini (Jana) leo ni Jimbo la Moshi Mjini.

Wale wote wanaodhani wameitiwa kuwatumikia Watanzania kwa nafasi za Ubunge na Udiwani mnakaribishwa sana TLP mtienia zenu,

Chama chetu ni chama cha kidemokrasia kinachoamini katika mashirikiano ili kuimarisha udugu na umoja watu kama Watanzania.

"TLP NI MOJA NA TANZANIA NI MOJA"


 
Ni wakati apumzike siasa mana umri umeshaenda kwa sasa. Naimani familia yake inaweza kumshauri. Ametumikia sana Tanzania lakini kwa sasa ni wakati apumzike siasa
 
Nafikiri ni wakati mwafaka kwa Mh. Mrema kujiuzulu siasa baada ya uchaguzi wa October. Amefanya mengi, amedumu kwenye siasa za upinzani na amekuwa mpinzani wa kwanza kuleta changamoto kubwa katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 1995. Akistaafu sasa atatunza heshima yake na kupata muda ya kupumzika.
 
Ile Itqaf aliyosomewa mwembechai wakati uleee ndiyo sasa imechanganya, yaani hana tofauti na mtoto wa chekechea
Hawa tuu mnatishana bure hakuna cha itifaki wala baba yake na itifaki yeye bado anadunda wazee wa umri wake wengi hapo.
 
Msikosoe sana jamani, muwe mnatoa mawazo mbadala ya kuboresha.

Sasa tunawaponda TLP lakini hatuelezi wangepaswa kufanya nini ili tuwapende.

Inawezekana matatizo Tanzania yanasababisha na watu wanaochukizwa na jambo halafu wanakaa kimya.
 
Mwenyekiti makini Fomu anachukua lini?
 
Watia nia wa chama gani tena? Hikihiki au kilekile... ina maana hajaunga mkono juhudi kama alivyosema?
 
Usiku huu kwa kua nina muda nimeamua kuangalia hiyo video. Nimeishia kucheka sana.

TLP ni chama cha siasa au genge la vichekesho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…