Mkristo anaangukaje katika zinaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkristo anaangukaje katika zinaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 21, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,593
  Trophy Points: 280
  MKRISTO ANAANGUKAJE KATIKA ZINAA?
  Kila mara nilipopata habari za watu wa Mungu walioanguka katika dhambi ya zinaa nilikuwa najikuta najiuliza swali hili, “Hivi wanapataje ujasiri wa kutenda tendo hilo
  Akili yangu ilikuwa inakataa kabisa kuamini kuwa mtu aliyeokoka (na wakati mwingine amejazwa Roho Mtakatifu) anaweza kuanguka kwenye dhambi ya zinaa. Lakini hata hivyo bado nikawa naendelea kusikia majina ninayoyafahamu ya watu wa Mungu waliookoka waliokubwa na dhambi ya zinaa.
  “Wanafanyaje mpaka wanaanguka katika zinaa”? Hili swali lilinisumbua kwa muda mrefu. Na siku moja nilikuwa nyumbani kwangu nikijiuliza swali hili moyoni, nikasikia Roho Mtakatifu akiniuliza ndani ya moyo wangu, akisema, “ Kwani Daudi aliangukaje? Je! Umesahau ya kuwa naye alikuwa mtu wangu, mtumishi wangu niliyempaka mafuta?
  Niliposikia swali hili, nilichukua biblia na kusoma maneno yanayoeleza kuanguka kwa Mfalme Daudi katika dhambi ya zinaa na mke wa mmoja wa askari wake.
  Mambo niliyoyasoma yalinifungua macho kuona jinsi ambavyo hata hivi leo watu wa Mungu wanavyoanguka au wanavyoweza kuanguka katika dhambi ya zinaa.
  Chukua biblia yako na usome habari hizi katika 2 Samweli 11:1-27 na 2 Samweli 12:1-25.
  Chanzo cha kuanguka kwa Mfalme Daudi katika dhambi ya Zinaa, ni KUTOKWENDA VITANI PAMOJA NA ASKARI WAKE.
  “Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote, wakaangamiza wana wa Amoni, wakakuhusuru Raba. LAKINI DAUDI MWENYEWE AKAKAA YERUSALEMU”. (2 Samweli 11:1)
  Kama kiongozi wao, Daudi alitakiwa kuongozana na watu wake vitani, lakini yeye aliamua kubaki Yerusalemu asiende vitani, na akamtuma mtu mwingine amwakilishe. Na jambo hili lilimpa nafasi nzuri sana ibilisi ya kumpa Daudi kazi nyingine ya kufanya. Ni kazi gani hiyo?
  “Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, AKATEMBEA JUU YA DARI ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke ANAOGA; naye huyo mwanamke alikuwa MZURI SANA WA KUPENDEZA MACHO”. (2 Samweli 11:2)
  Ni kitu gani kilimfanya Mfalme Daudi aamue kutembea juu ya dari ya jumba lake badala ya kwenda vitani pamoja na watu wake? Na alipomwaona Bathsbeba, mkewe Uria akioga alishindwa kujizuia, mwisho wake ni kuzini naye na huyo mama kupata mimba!
  Wakristo wengi wamejikuta wameingia katika mtego wa zinaa kwa sababu ya kutokwenda ‘Vitani’ wakati wanapotakiwa kufanya hivyo. Vita tunavyovisema, si vita vya kimwili.
  “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili, maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo”. (2 Wakorintho 10:3,4)
  Na pia imeandikwa; “ Kwa maana kushindani kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya, katika ulimwengu wa roho”. (Waefeso 6:11)
  Ndiyo maana Yesu Kristo alisema; “ Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.” (Mathayo 26:41)
  Usipovipiga vita katika maombi, inakuwa ni rahisi sana kuangushwa na majaribu unapokutana nayo. Wakristo wakipoa katika maombi inakuwa rahisi kuanguka katika dhambi, si katika zinaa peke yake, bali katika mtego wowote ambao shetani anauweka mbele yao!
  Kutokuwa mwombaji, ni sawa na kutokwenda vitani na wenzako, kama vile Mfalme Daudi alivyofanya.
  Kwa hiyo unaona ya kuwa ingawa Mfalme Daudi alikuwa mtu wa Mungu, mtumishi wake, na mpakwa mafuta wake, alianguka katika zinaa. Na hata hivi leo kuna wakristo, tena wameokoka, na kupakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu, wanaonguka katika dhambi ya zinaa. Kwa nini? Kwa kuwa hawavipigi vita vya kiroho na wenzao, na wamepoa katika kumtumikia Bwana.
  Je! Lutu aliangukaje?
  Hili ni swali ambalo Roho Mtakatifu aliniuliza baada ya kunieleza habari za Mfalme Daudi. Ingawa Lutu alikuwa mtu wa Mungu, na licha ya kuwa alikuwa anabebwa kwa maombi ya Ndugu yake Ibrahimu, bado alianguka katika zinaa.
  Roho Mtakatifu alikuwa anaendelea kunijibu swali nililokuwa najiuliza ya kuwa, watu waliookoka wanaangukaje katika zinaa?
  Habari za kuanguka kwa Lutu zimeandikwa katika kitabu cha Mwanzo 19:30-38.
  Lutu alizini na watoto wake wawili wa kike baada ya kuleweshwa mvinyo.
  Na ukiisoma habari hii inasikitisha sana. Shetani alipata nafasi ya kumwangusha Lutu si kwa sababu ya binti zake kumlewesha mvinyo, bali kwa kuwa MKE WAKE HAKUWA PAMOJA NAYE. Unadhani mke wake angekuwapo hawa watoto wangepata nafasi ya kumlaghai baba yao? Hapana! Kwa nini?
  Kwa maana “ Bwana ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume.” (Yeremia 31:22)
  Unaweza kujiuliza ni kwa njia gani mke atalimnda mume wake. Kumbuka imeandikwa mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana. Kazi moja ya busara iliyo ndani ya mke ni kumlinda mume kutokana na mashambulizi ya Malaya! Soma Mithali 2:11-22.
  Hata hivi leo ndoa ambazo mume na mke hawakai vizuri, huwa ni rahisi kwa wao kuanguka katika dhambi ya zinaa hata kama wameokoka. Na huu siyo ushuhuda mzuri.
  Tunamshukuru Mungu kwa wale ambao wamesimama katika ushuhuda ingawa ndoa zao zina matatizo.
  Jambo la kujifunza zaidi
  Roho Mtakatifu alipokuwa anaendelea kunifundisha akasema ndani ya moyo wangu hivi; “Watu wengi wanadhani zinaa ni tendo la kimwili tu linalofanywa kati ya mwanaume na mwanamke nje ya ndoa, lakinikuna namna zaidi ya moja unayoweza kuanguka katika zinaa.”
  Niliposikia hivyo moyoni mwangu, niliichukua biblia na nikaanza kuisoma upya juu ya zinaa na nikaona kuna namna nne ambazo zinaa inatajwa:-
  1. KATIKA MWILI:
  “….Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya Kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? …. Ikimbieni zinaa, kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” (1 Wakorintho 6:13-20)
  2. KUTAMANI KWA MACHO. Yesu Kristo alisema;
  “Mmesikia kwamba imenenwa Usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu AMTAZAMAYE MWANAMKE KWA KUMTAMANI, amekwisha KUZINI NAYE MOYONI MWAKE.” (Mathayo 5:27,28)
  3. KUACHA MKE NA KUOA MWINGINE
  Yesu Kristo alisema;
  “Kila amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine azini ……” (Luka 16:18)
  4. KUOA ALIYEACHWA. Yesu Kristo alisema;
  “Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; NAYE AMWOAYE YEYE ALIYEACHWA NA MUMEWE AZINI.” (Luka 16:18)
  Kila mtu na ajipime katika hayo; ikiwa umefanya mambo kama hayo niliyoyataja, biblia inasema UMEZINI! Je Hakuna waliokoka wanaofanya mambo ya jinsi hii? Wanaowaacha wake zao halali? – Wanaooa walioachwa? – na wanaozini katika mwili?
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  MZEE umeokoka nin?!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyu Pdiddy ni bingwa wa copy and paste, embu angalia mabandiko yake yote ya leo...all fictions!
  Bt simlaumu, si wakati wake huu!
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahaha!jioni njema bwana pj.TUPO PAMOJA!ngoja nikabuy time na familia
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuna watu tangu wajiunge JF hawajawahi kutoa mawazo yao wanabandua mawazo ya wengine na kukandika hapa :confused:
   
 6. October

  October JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nguli I like your signature.
   
 7. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwani zina na ulezi zimekatazwa ndani ya Ukiristo?
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hiyo ilikuwa karne ya 19, sikuhizi na wanawake wana wake pia!
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siku hizi ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa na kanisa yaani wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume.
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,200
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Maneno yako ni mazuri pJ ila kwa mtu aliyewahi kumfuatilia Mwakasege haya ni mahubiri yake uliyoya-copy na kuya-paste hapa jamvini. Tatizo la zinaa lipo katika mapokeo ya wanadini mfano -baazi husema mke akiachwa na kupewa talaka ni halali aoewe. -wengine husema ukioa kabla hujaokoka na ukaingia ktk imani ya kilokole basi unatakiwa uoe maana hukua na agano lililo sahihi. -wenginene hesema waweza kuoa ndoa ya mapatano ya mda maalumu na kisha kila mmoja akachukua time zake na mnyinginezo nyingi. Sasa hebu jiulize kama kila mmoja ameaminishwa kwa jinsi yake na anafunga na kukesha ktk kuomba kuvuviwa nguvu za hiyo imani mambo yatakuwa je?. Na kila mwalime wa hizo deen anajinadi kuwa ni roho mtakatifu kamfunulia? Kuna kisa kimoja ambapo jamaa alitoa kwa kusema alijaliwa kukutana na Roho mtakatifu na alimkuta na huzuni nyingi na alipouliza kulikoni RM alimweleza ni kwa sababu ya masingizio ya wanadamu yaani kila mtu na pokeo lake ananisingizia mimi kuwa ndie niliyempa. Alipotoka hapo alibahatika kukutana na Shetani nae alikuwa na huzuni nyingi, na alipouliza kulikoni shetani alijibu ni kwa sababu ya masingizio ya wanadamu. Kila uvu analofanya akifumaniwa tu anasema jamani sio mimi ni shetani ameniingia. Ni kweli watu wana njaa na kiu, sii njaa ya chakula bali ya kweli ya Mungu. Ni nani atawapa neno lisiloghoshiwa? Mungu hahitaji sana kufasiriza zaidi ya jinsi anavyoweza kujifasiri yeye mwenyewe kwa Roho yake. Watumishi wanatakiwa kuwapa watu Yesu nae angewaongoza katika kweli yote badala yake sasa kuna kujipeana wao wenyewe kwa watu na hivyo kusababisha kundi la watu waombao na kukesha katika mambo ambayo Mungu hakuwahi kuyaagiza na wala sii ya adili. ZINAA IPO YA KIMWILI NA YA KIROHO PIA NA HII YA KIMWILI NI MATOKEO YA ILE YA KIROHO AMBAYO IMEKWISHA TENDEKA KATIKA ROHO KWANZA!
   
Loading...