Mkopo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkopo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAGL, Apr 14, 2011.

 1. G

  GAGL Senior Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani mwenzenu toka nihitimu chuo sijapata kazi. Ila nimeamua kujiingiza kwenye ujasiriamali. Nataka kuendesha mradi wa internet cafe' ambapo ninahitaji kuwa na mil 3, nimeandika mchanganuo wa biashara hii. Ninaomba mtu yeyote jamvini hapa mwenye moyo wa huruma anisaidie kunikopesha hela hii nifanye biashara, ajira hakuna jamani. Nina uhakika wa kuirudisha hiyo fedha, na kama atahitaji wadhamini ninao wengi na wa uhakika. Tafadhari napatikana hapa 0786 046 484 au gagl2010@yahoo.com
   
 2. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yale mabilion ya JK. yangewafaa watu kama hawa.
   
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  We wa kiume au wa kike?
   
 4. G

  GAGL Senior Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wa kiume ndugu, ila naomba usiangalie ujinsia maana haileti picha nzuri.
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  dah! Sijaelewa mantiki ya hili swali.
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unataka kulipa kwa interest ya ngapi hivi? are you interested in partenership?
   
 7. k

  kituro Senior Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ndugu yangu nina nia yakukusaidia sana tu naomba ujibu maswali haya
  1. ulihitimu elimu ya chuo gani (BA au BSc., Diproma, certificate, MA au MSc, au PhD)
  2. Ulihitimu chuo gani na kozi gani
  3.mwaka gani uliohitimu

  ndugu yangu naomba unijibu nitakusaidia kwa kadri nitakavyoweza si lazima nikusaidie utakavyo bali nitakavyoweza kukusaidia.
   
 8. G

  GAGL Senior Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimehitimu shahada ya sheria, mwaka 2009 chuo kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam.
   
 9. G

  GAGL Senior Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuhusu interest itakuwa ni makubaliano kati yangu mimi na wewe kwa sababu wewe kama ni mtoa mkopo utakuwa na terms zako. pia nipo tayari kuwa katika partnership
   
 10. duda

  duda Senior Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good idea, pia nina idea kama yako Mungu akinijalia, lakini Mil3 naona mbona ni ndogo sana? coz unatakiwa uwe na vitu kama printers, photocopy machine, binding, laminating machine nk ndo utakua unaingiza pesa nyingi kidogo kuliko internet pekeake.(kwa budget yangu mie 5mil nadhani ndo poa) anyway pia unaweza ongeza vitu baada ya kuanza biashara yako.
  Mungu akusaidie upate wa kukusaidia na kwa moyo huo utafika mbali
  All the best
   
 11. K

  Kichikapua Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu pole na matatizo ya ajira, hili ni janga la kitaifa. Ila nakushauri upate ushauri wa kijasiriamali kwanza kabla ya kuanza kazi ya internet. Unajua siku hizi makampuni ya simu yanatoa internet services kwa bei ya chini sasa, na yanacompete thus bei itazidi kuwa chini. kwa hiyo unaweza kuanzisha kitu kabla hujaanza kupata faida kikwa redundant
   
 12. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Huo ujasiriamali hauendani na taaluma uliyosomea yamkini ukachemsha na kushindwa kurudisha mkopo .Jaribu kufungua akili zaidi uende kwenye ujasiriamali ulioenda shule.Hata mie ticha wako nikikukuta hapo niseme kijana unaona mbali.Kwa ujumla wa Tz tunatakiwa kuamka na kuona kuwa mitaala ya elimu tuliyonayo haitusaidii kujiajiri bali kuajiriwa tuu.Shime vyombo vinavyohusika viandae mitaala yenye tija kwa walengwa zaidi kuliko Shahada za mapambo tu.
   
 13. K

  Kidume faru New Member

  #13
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye Blue vp mkuu!!
   
 14. k

  kituro Senior Member

  #14
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nashukuru kwa kunikosoa nimejifunza inaandikwa diploma na si diproma nashukuru sana mkuu! ingawa mhusika ujumbe amepata.
   
 15. k

  kituro Senior Member

  #15
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sasa ndugu yangu nakushauri kama ifuatavyo,
  kwanza jifanye kama huna shahada ingawa unayo, lakini jione kama ni leseni yakupatia hela. pili tafuta kazi yoyote mfano kufundisha kiswahili, kingereza, historia, jografia, uraia, au masomo yoyote matatu ambayo unaweza kuyafundisha hata kama hupendi wewe nenda uwe unafanya kazi huku ukiwa unatafuta ajira unayoitaka.
  kumbuka huwezi kupata dili kirahisi kama huna dili!.
  kufundisha ni ajira ambayo inapatikana kwa urahisi ila usiende sehemu ambako hakuna mawasiliano!
  ukiwa unafanya kazi utaweza kuyasoma mazingira ukiwa kama raia siyo ukiwa mwanafunzi.
  au tafuta ajira hata ya uafisa utumishi hata kwenye mashirika ili uweze kupata sehemu ya kujishikiza kwenza, ukipata sehemu ya kujishikiza itakuwa rahisi sana hata kupata ajira sehemu nyingine.

  kitu kingine uende kwa mawakili wa kujitegemea omba kujishikiza hata kwa bure kwanjia hiyo utajurikana badae itakuwa rahisi kuajiriwa hata na watu binafsi na ikitangazwa serikalini ndiyo mambo itakuwa rahisi kwakuwa unauzoefu!.
   
 16. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #16
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata hii nayo kama haijakaa vizuri sana, yaani hivyo ndani ya mabano ndo vyuo gani?
   
 17. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu watu wengi waliosoma sheria wanachagua kazi, nakushauri uombe kazi yoyote ile, hata bank industry wanapokea watu washeria kwa kuwatumia kama credit office or bank clerk and teller. Usikubali kutoka kwenda mkoani kabla ya kupata kazi ya uhakika.Pia jaribu kila ofisi unayoiona peleka CV.
   
 18. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kuuliza ni wajinsia gani? unataka nini kutoka kwake au ulifikiri kuna nafasi yakudai takrima?
   
 19. k

  kituro Senior Member

  #19
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nimeandika kwenyemabano elimu zinazotolewa na vyuo tofauti mfano BA ni
  Bachelor of art
  BSc. ni Bachelor of Science MA masters of art MSc. Masters of science mengine uliza kwa jirani yako yeyote aliesoma chuo chochote atakusaidia. nashukuru kwa kuwa muwazi, mungu akubariki!.
   
 20. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mkuu binafsi naamini una fikira potofu. Unamjua mwanzilishi wa kampuni ya Apple inayotamba kwa kutengeneza computer, simu za iphone n.k? Unadhani alisomea vitu hivyo vilivyomletea utajiri? Najua maana yako ni kwamba daktari aanzishe hospitali, mfamasia aanzishe famasi, mwanasheria aanzishe firm ya sheria. Lakini hilo si sahihi. Cha muhimu ni kama una upevu wa kuijua biashara husika. Mimi ni daktari wa binadamu, lakini nafanya vizuri tu kwenye biashara zisizohusu profession yangu.
  Ndugu yangu mwenye wazo la biashara, binafsi nisingependa kufungua internet cafe (sikukatishi tamaa) katika Tanzania hii ya sasa, ambayo kila kukicha internet inazidi kuwa rahisi kuipata. Najua bado utapata wateja, lakini sidhani kama biashara hii itakuwa sustainable. Ukibahatika kupata msaada wa kiasi hicho cha pesa, yamkini utakuja ku assess mwelekeo wa biashara na kufanya maamuzi sahihi.
   
Loading...