Mkopo wa kujikimu PSPF

Oxpower

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,161
3,054
Wanajukwaa habari za majukumu.

Mimi ni nmeajiriwa hiv karibuni.
pspf wanadai wanatoa mkopo wa kujikimu kwa wafanyakazi wanaoanza maisha kama pesa ya kujikimu.

Sifa za kupata mkopo.Uwe umechangia mfuko kwa miezi 6 na isizid miezi12 na mkopo wanatoa mara3 ya basic salary yako na riba ni 7.5% kwa mwaka.

Kabla sijaanza mchakato naomben msaada kwa wazoef kazini

1:Je kweli hizo pesa wanatoa?
2:Je riba yake ni hyo hyo 7.5 kwa mwaka kama ilivoandikwa au ni figa ya ukanjanja
3:hiyo ya kujikim inatofauti gani na mikopo mingine
4:kero zao ni zipi
 
Hii mifuko ni majipu. Kuna cku nilikuwa apo HQ kwa shida zangu tofaut niliskia wakimwambia memba mmoja alietaka kupata mkopo wa kwenda shule eti aende uko shule kuchukua fomu afu akaandikishe mkopo benki walizokubaliana nazo wao afu benk itampa mkopo kwa riba ya benki (wao wanatoa guarantii kwa benk ikuamini), nilichoka mwenyew! Nawaona hawa jamaa ni majambawaz tofaut yao wanakaba mchana na kuvaa tai. Km uko dar watembelee pale posta mpya usisikie la kuambiwa.
 
Ni wababaishaji, hata LAPF wanatoa hiyo mikopo ya kujikimu tatizo wanalazimisha eti mpaka mshahara wako uwe unapitia NMB, lakini kipindi ninajiunga hilo sharti halikuwepo.Kwahiyo wote ambao mishahara inapitia benki zingine tofauti na NMB hatuwezi kupata mkopo wa kujikimu kutoka LAPF.
 
Mi nataka kujua kama ukipata huo mkopo unaurejesha je? Ni kwamba unakuwa unakatwa kwenye mshaara au kwenye mafao yako?
 
hii mifuko cjui inawaza vipi miezi 6 halafu unaitwa mkopo wa kujikim??!!! sasa waseme wanatoa mkopo tu kuliko kusema ni wakujikim.
 
PSPF nao ni wahuni wanadai ili upate mkopo huu lazima ufungua account na Bank ya Posta. Na walikuwa wanauza viwanja meter sqr moja 30,000Tsh
 
Hii mifuko ni kama wagombea wa vyama vya siasa ukimpigia kura basi biashara inaishia hapo kifuatacho ni kua mtumwa wao,wewe ukijaza fomu angalia tabasamu la wakala wa mfuko utagundua tayari kakutia nyavuni.
 
Mm pia waliniambia ukitaka funiture za ndani baada ya kuanza kukatwa tu utapewa ila nilivyoenda ofisn kwao kuulizia wakaniambia mpka uwe umechangia mika 5 nilichoka.
 
Hii mifuko ni majipu. Kuna cku nilikuwa apo HQ kwa shida zangu tofaut niliskia wakimwambia memba mmoja alietaka kupata mkopo wa kwenda shule eti aende uko shule kuchukua fomu afu akaandikishe mkopo benki walizokubaliana nazo wao afu benk itampa mkopo kwa riba ya benki (wao wanatoa guarantii kwa benk ikuamini), nilichoka mwenyew! Nawaona hawa jamaa ni majambawaz tofaut yao wanakaba mchana na kuvaa tai. Km uko dar watembelee pale posta mpya usisikie la kuambiwa.
mkuu, hii mifuko ni majanga makubwa. hata mie niliwahi kwendapo PSPF nikakuta kitu hiki. haya majitu ni masengerema kuliko mnavyoweza kudhani.
 
Wanakata kwenye mshahara, riba nafikiri 13%
huu mkopo ni wa kijinga na kipuuzi sana. kwanini hasa wanalazimisha kihivi? kule PSPF wanalazimisha watu wajiunge na benki ya posta. wajinga sana hawa wapuuzy!
 
Dah yani nmejikuta nmechoka,walijinad kwa mbwembwe sana.lakini je ni mfuko gani ambao angalau hauna usanii mwingi
 
Dah yani nmejikuta nmechoka,walijinad kwa mbwembwe sana.lakini je ni mfuko gani ambao angalau hauna usanii mwingi

Mifuko yote ni watoto wa baba na mama mmoja. Hakuna wenye unafuu, kazi yao ni kunyonya wafanyakazi.
 
LAPF walijinasibu wanatoa mkopo wa kujikimu mara3 ya basic salary na unarudisha kwa miaka miwili, lakini jana nimeenda ofisini kwao wanasema mkopo utarudishwa ndani ya mwaka mmoja na sio miwili tena. riba 13%
 
Zile nyumba kule chanika je? Hawa watu wanachekesha sana vijumba Kama vibanda vya simu za TTCL sijui Kwa mtazamo upi hadi wakajenge vile vituko PSPF shikamooni
 
Back
Top Bottom