Mkopo mdogo wa fasta

Together
 
Umenikumbusha ndugu, kuna kipindi nilikuwa na ela ndani sijaipeleka bank baada ya kufanya biashara flan.
Basi kuna jamaa rafiki yangu alikuwaga anafunga mifumo flani kwenye nyumba na alikuwa anapenda kweli kujitangaza kwenye jukwaa hili ila siku hizi kaacha.
Akanipigia akaniambia nimsaidie laki nane atarudisha ndani ya siku tatu kakwama na ana kazi anahitaji vifaa.
Nikamtumia kwa simu.
Kesho yake akapiga tena nimuongezee lak na nusu eti badala ya kurudisha lak tisa na nusu atanipa milion moja na laki moja akimaliza kazi within two days mimi nikamjibu nakuongeza ila unirudishie kiasi nilichokupatia sitaki riba yako wewe rafiki yangu.
kesho yake jirani yangu naye akawa anadaiwa kodi mwenye nyumba kamkaba hatari akanifuata jamani nisaidie kama una lak tano ntakurudishia ilikuwa mwezi wa nne akasema atairudisha mwezi wa sita, nikaona mbali ila nikapiga moyo konde nikampatia mwenye nyumba maana alikuwa nje anamsubiri.
Sasa baada ya hapo yule wa laki tisa na nusu huyo hata simu zangu alikuwa hapokei.
Jirani yeye kila nikimkubusha anapiga sound mara nina mgonjwa mara hivi ukimtxt anajibu ok.
Siku akanipatia laki ilikuwa mwezi wa saba nadhani baada ya hapo kimya.
Nikaja sikia kachukua loan ya 24 mils nikasema now nalipwa kuja kumdai eti oh nilisahau nimenunua kiwanja sasa hivi sina ela.
Nikasema basi sidai tena na kuhama nilishahama ilikuwa mwaka jana.
Ila ajabu wote hao wawili wa laki tisa kuna siku kankpigia anaomba nimsaidie 50,000 nikamjibu sina huyo aliyekuwa jirani yeye ndiye kila mara anataka msaada sijui amesahau.
Nilipohamia sasa nikamkuta bwana bonge la msabato full dini nimekaa miezi miwili siku moja akaniomba nimsaidie laki tatu ilikuwa mwaka huu mwezi wa pili.
Nilimpatia lakini mpaka leo hajarudisha na hapa kahama msg hajibu simu hapokei.
Nimeamua kuacha kudai, natamani niwe na roho ya kutosaidia lakini mtu akiwa na shida na ela ninayo najikuta namsaidia.
Watu wengi si waaminifu
 
Some people are always negative and they'll always be negative..........
 
do you think this is how good Samaritans behaves ......

haaaa haaaa

this thread has been started by ring of early birth conmen

Mark my words
I dont think so... jf kuna watu wengi kind na kutoa ni moyo unaweza ona 20,000 nyingi lakini aliyesaidiwa leo huwezi jua alikuwa na shida gani na in future anaweza kuja mfanyia jambo kubwa aliyemsaidia
 
...Wanasahau kuna kesho,wanasahau shida Haina mwenyewe.
hapa nadaiwa laki 3 Ila week ya 2 naisaka bila mafanikio na njee kuna hela yangu nyingi.

Hili ni tatizo sugu sasa hivi, ndio maana kila mara nawaambia watu kulipa madeni ni kipaji na sio kila mtu kajaliwa. Mtu anakopa alaf anataka arudishe akipata pesa ya ziada ambayo hana kazi nayo, nani kakwambia kuna pesa haina kazi?
Hata pale unapoamua kumsaidia mtu ni ile tu huruma sio kwamba hauna kazi na pesa. Unaazima mtu pesa alaf wewe ndio unaingia kwenye matatizo. Very sad, pole sana. Ayway we are on the same boat ila naogopa kuweka details za watu hapa wasijekuona nimeamua kuwaanika ila u SAMARIA umeniponza.
 
Dah ninanvyoona humu watu kutokulipwa ndo naamin sina nuksi aisee basi tu, mie nimekopesha watu wengine had mil. Na nusu alafu nilidunduliza tu kahela kaboom na vibiashara ninavyofanya uje uwe mtaji lol, yani mtu hana huruma unadai wala hajal kama nawe una shida ya hiyo hela wala maumivu. Imebid nikope hela ya mtaji nianze moja. Lakini siwasamehi ila nitajifunza roho Mbaya maana wasivo haya mtu anaendelea kuomba umkopeshe. Mie naona aibu kudaiwa sana nimeanza kulipa deni kadri biashara inavotoka...Mniungishe tofali jaman nami nisiwe mdaiwa sugu
 
Me naungana na member fulani hapa bado na mashaka na hii move, wa Tanzania sisi ni wajanja saaaaana nikikumbuka watu walivyo tapeliwa ki mtindo hata nikikuhadithia utashangaa sana, hebu tuone kwanza itakuaje baadae...
 
.....salaaaleee;PUMBA!....aliekopeshwa ni active member humu toka 2008,kwa mwenye akili anajua what that means!
..we baki na hisia mfu na roho yako ya kimaskini!
 
.....salaaaleee;PUMBA!....aliekopeshwa ni active member humu toka 2008,kwa mwenye akili anajua what that means!
..we baki na hisia mfu na roho yako ya kimaskini!

ASANTE. Nadhani wewe umemaliza kila kitu. Ni muhimu pia kujua ni haki yake huyo mtu kufikiria negative, by the way nashukuru msaada nilipata na nilirudisha mengine ni kawaida tu kwani humu ndani kuna watu wengi wa kila aina. kama nilivyotegemeaa kupata msaada na pia nilitegemea kupata challenges kama hizo.
Tusonge mbele daima, pia nawashauri watu kutokuficha matatizo kwa kuogopa watu watawacheka au kuwaona matapeli, muhimu tu ni uaminifu.
 
 
Pole sana hiyo ni changamoto ila isikufanye kushindwa kumsaidia mtu pale unapoweza kumsaidia kwani Mungu ni mwema atakulipa
 
Ukweli kulipa ni mtihani na huyo unaye mkopesha ukiwa na shida hakukopeshi hudhani utapunguza ktk deni lako.
Ukweli ni Dawa ya deni ni kulipa
 
Mkuu unamwandikisha shemeji yako.. Doh
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…