Mkojo wa mjamzito: Biashara nyingine ya siri isiyojulikana na wengi

Kweli nikupe ongera kwa kufikiria na kupata hili na kupost pia.
Ulichopost kina ukweli ndani yake wako wengi wakina mama wa aina hiyo ya kihuni.
Wako na wengine mimba moja baba wa mimba hiyo wako (10) na wote wanaitumikia hiyo mimba na wajuani na kadi za clinic ya mimba zina kuwepo idadi hiyo kila anaetaka aone kadi hupewa ilioandikwa jina lake.
Na vituo vya huduma viko sawa na idadi ya baba wa hiyo mimba hapo upo?
Na mtoto akiisha kuzaliwa anatambulishwa kwa mababa wote hao 10 ki roho safi kabisa?
 
Na mtoto akiisha kuzaliwa anatambulishwa kwa mababa wote hao 10 ki roho safi kabisa?
Mara nyingi ni baba wasio zidi wawili... Mimi jamaa yangu yalishamtokea... Nilimpeleka kwa shemeji akasalimie mwanawe aliyekuwa anamhudumia huduma zote
Hakutoa taarifa siku hiyo kama anakwenda.. Tulikutana na baba mwingine anaitwa Rich... Demu alitimua mbio tukabaki wanaume tupu... Ikabidi tu sasa wayajenge kiroho safi... Kumbe kila mmojawao alikuwa anatambulishwa kama kaka binamu kila demu alipoulizwa fulani ninani
 
Mkuu umefikiria sana. Ilitokea juz juz jamaa mmoja. Kaenda na demu kamkubalia wakati wa kufanya jamaa akataka a withdraw demu akakataa. Baada ya mwezi kamwambia anamimba na hajajiandaa itabidi akatoe. Akalambwa hela ya kutolea. Aka kaa wiki akamwambia anaumwa anaenda kicheki akamwambia haikutoka anahitaji dawa tena akalambwa hela tena. Akakaa kdogo akamwambia hali mbaya uchafu unatoka anahitaiji kusafishwa akalamba hela ya kusafishia. Haka kamchezo kabaya sana. Hapa mkuu umefungua macho wengi sana
 
Achana na hiyo kuna hio ya kutegeshewa mimba maksudi kisa tu life lako liko vizuri miradi unayo halafu ajue uko bachelor hauna hata mtoto wa kusingiziwa
 
Mkuu umefikiria sana. Ilitokea juz juz jamaa mmoja. Kaenda na demu kamkubalia wakati wa kufanya jamaa akataka a withdraw demu akakataa. Baada ya mwezi kamwambia anamimba na hajajiandaa itabidi akatoe. Akalambwa hela ya kutolea. Aka kaa wiki akamwambia anaumwa anaenda kicheki akamwambia haikutoka anahitaji dawa tena akalambwa hela tena. Akakaa kdogo akamwambia hali mbaya uchafu unatoka anahitaiji kusafishwa akalamba hela ya kusafishia. Haka kamchezo kabaya sana. Hapa mkuu umefungua macho wengi sana
kila ikitolewa imoooo
 
Mji mzito sana huu
Kuna mambo yanaendelea kimyakimya na chini kwa chini huku baadhi wakibaki na vicheko baada ya kupiga pesa ya mabwege na huku wengine wakibaki na majuto na kujiapiza kutorudia tena.

Baadhi ya wanaume wenye macho juu Wamepigwa sana kwenye hili jambo.. Naamini hata kati ya wasomaji watakaosoma hii mada ni wahanga wa hili jambo.

Ujumbe wa BABY NINA MIMBA YAKO.. huwachanganya sana mabazazi na wale wanaojiita mabaharia bila kuwasahau wazee wa mjini... Wazee wa bandari... Unapopata ujumbe kama huu toka kwa mchepuko wako ambaye anaweza kuwa mke wa mtu bandia au halisi, mwanafunzi (halisi au bandia) danga nk unachanganyikiwa kabisa.. Cha kwanza kuwaza ni mke wako nyumbani... Mpenzi wako... Kazi yako ama maisha yako.

Kuna wanawake siku hizi hii ndio biashara yao kubwa na inawalipa vizuri tu .. Unakutana na binti au mdada mzuri kweli unatupa nyavu zinanasa kimasikhara kabisa lakini unapewa onyo mapema... Mimi ni mwanafunzi au mimi nina mtu wangu au mimi ni mke wa mtu.... Bila kutafakari hilo onyo unasema utafanya siri.. Unakubaliwa unakula mzigo kiboya kabisa

Bila kujijua kuwa uko kwenye foleni ndefu ya kubambikiwa ujauzito feki mwanaume kidume wewe unajiachia kwa raha zako.. Ukimhitaji mtoto unampata unakula anasepa. Na anaweza kabisa awe hakusumbui kwa shida ndogo ndogo.... Usijione mjanja ukadhani umepata... Tambua tu umepatikana

Siku yako ya kupigwa ikifika unapata ujumbe mbaya wa ujauzito na unaambiwa wazi kabisa kuwa hayuko tayari kuzaa kwa wakati huo... Kwahiyo mzee inabidi udhamini mchezo... Na ili kukuaminisha mnaenda wote hospital kupima.. Kumbe tayari mwenzako ana kichupa chake cha mkojo wa mtu mwingine kabisa mwenye ujauzito amekificha kwenye chupi yake

Ni wazi hutamsindikiza mpaka chooni hata akikuomba.. Sana sana utaishia mlangoni.. Yeye huko ndani atabadili tu mkojo toka kichupa alichokuja nacho kwenda alichopewa hospital... Majibu yakitoka... Imooo.. ...
Kifuatacho ni gharama za kutoa mimba tena anachagua Marie Stopes.. Ukikomaa kwenda naye mpaka daktari atapangwa...
Baada ya hapo unahudumia 'mgonjwa' na akipona unapigwa chini.. Mchezo unaendelea kwa maboya wengine....

Wanaonunua mikojo ya waja wazito wengi wao sio kwa ajili ya ushirikina bali kwa ajili ya kuwapiga mabazazi... Najua umesoma huku ukikumbuka pesa ulizotoa kwa ajili ya abortion huku ukijisifu kwa wanaume mwenzako kuwa una mbegu Kali sana.. Ukigusa tu kitu na box... unaibiwaaa...Boya WEWE
Natamani kutag mtu humu ila policy hainiruhusu aliniingiza king ila ilifeli jamani tuheshimu wazee wetu kwani kwa akili yangu pekee niliingia king nashukuru akili ya shangazi nikabaki salama
 
Mkuu Mshana Jr hili ni kweli nishawahi kushuhudia kisa kama hiki! Tena kuna wengine wameenda mbali zaidi mpaka kuandaa fumanizi feki kwa mke au mtoto! Unakutana na dogo mtaani anakudanganya mwanafunzi na picha juu..siku ya kwenda kumla anakutengenezea mazingira ushikwe then wanakuchomoa hela.

Hawa watu ni professional wanaijua kazi yao vizuri na wengine ndio kazi zinazowaweka mjini..watu wanafunga mpaka P.O.P feki na vyetu juu..ukiwa mwepesi unapigwa vizuri tu!
Hilo la mafumanizi feki wala siyo mjini tu...

nenda vijiji vya Ruangwa tu pale yaani watu waliachana muda sana (pengine wawe hata hawakuoana kabisa) lakini ukijiingiza imekula kwako utashangaa umefumaniwa eti na (tena kama ni boyaboya) unachomolewa hela ndefu ndefu tu

Madent wanafeli shule wapo mtaani wanafanya umalaya tu lakini ukajiingiza wewe mlengwa (namaanisha mwenye kutagetiwa kuliwa hela) basi unaundiwa "kafumaniwa akiwa na mwanafunzi"

Ishu nyingine ambayo kwa mimi naona ndiyo kali kuliko ni pale ambapo mtu anaenda kufanya kila namna aolewe na fulani ila kwa lengo la ~waishi muda fulani kisha aombe talaka ili wakiachana mali igawanywe pasu kwa pasu ajipatie mtaji wa kusongesha maisha yake... imefikia washkaji wanajenga nyumba mbilimbili na anakwambia kabisa hii nyingine ni kwajili ya mke wangu siku tukitengana!!!
 
Yupo mdada mmoja alishawahi nlitea hizo za mimba hewa, nlichomjibu kuwa mimi huwa sitoi mimba na siwezi gharamia mauaji alinirudi kwa matusi makali na mazito nikamwambia huo ndo msimamo wangu kama una mimba utazaa mimi sitoshiriki kutoa,tena tule tudude twa kupimia si vipo dukani tu, nikirudi tutapima wote :D:D muda si muda mimba haipo
Toka hapo niilmvua vyeo vyote, ni takribani miaka kumi na moja iyopita hawajaanza leo wapo toka enzi:D:D
 
Jamaa unanifurahisha sana wewe comments zako ni fupi fupi tu
ngoja niingie gym kwanza
Ngoja niingie dobi kwanza
Ngoja ni... kwanza

Yaani hunaga kucomplicate mambo nachekaga sana
Asante sana braza.
Karibu mihogo na maziwa mtindi
 
Back
Top Bottom