Mkojo wa mjamzito: Biashara nyingine ya siri isiyojulikana na wengi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
Mji mzito sana huu,

Kuna mambo yanaendelea kimyakimya na chini kwa chini huku baadhi wakibaki na vicheko baada ya kupiga pesa ya mabwege na huku wengine wakibaki na majuto na kujiapiza kutorudia tena.

Baadhi ya wanaume wenye macho juu Wamepigwa sana kwenye hili jambo. Naamini hata kati ya wasomaji watakaosoma hii mada ni wahanga wa hili jambo.

Ujumbe wa BABY NINA MIMBA YAKO huwachanganya sana mabazazi na wale wanaojiita mabaharia bila kuwasahau wazee wa mjini... Wazee wa bandari. Unapopata ujumbe kama huu toka kwa mchepuko wako ambaye anaweza kuwa mke wa mtu bandia au halisi, mwanafunzi (halisi au bandia) danga nk unachanganyikiwa kabisa.. Cha kwanza kuwaza ni mke wako nyumbani. Mpenzi wako, Kazi yako ama maisha yako.

Kuna wanawake siku hizi hii ndio biashara yao kubwa na inawalipa vizuri tu. Unakutana na binti au mdada mzuri kweli unatupa nyavu zinanasa kimasikhara kabisa lakini unapewa onyo mapema. Mimi ni mwanafunzi au mimi nina mtu wangu au mimi ni mke wa mtu. Bila kutafakari hilo onyo unasema utafanya siri. Unakubaliwa unakula mzigo kiboya kabisa.

Bila kujijua kuwa uko kwenye foleni ndefu ya kubambikiwa ujauzito feki mwanaume kidume wewe unajiachia kwa raha zako.. Ukimhitaji mtoto unampata unakula anasepa. Na anaweza kabisa awe hakusumbui kwa shida ndogo ndogo. Usijione mjanja ukadhani umepata. Tambua tu umepatikana.

Siku yako ya kupigwa ikifika unapata ujumbe mbaya wa ujauzito na unaambiwa wazi kabisa kuwa hayuko tayari kuzaa kwa wakati huo... Kwahiyo mzee inabidi udhamini mchezo. Na ili kukuaminisha mnaenda wote hospital kupima.. Kumbe tayari mwenzako ana kichupa chake cha mkojo wa mtu mwingine kabisa mwenye ujauzito amekificha kwenye chupi yake

Ni wazi hutamsindikiza mpaka chooni hata akikuomba sana sana utaishia mlangoni.. Yeye huko ndani atabadili tu mkojo toka kichupa alichokuja nacho kwenda alichopewa hospital. Majibu yakitoka Imooo .
Kifuatacho ni gharama za kutoa mimba tena anachagua Marie Stopes.. Ukikomaa kwenda naye mpaka daktari atapangwa.
Baada ya hapo unahudumia 'mgonjwa' na akipona unapigwa chini. Mchezo unaendelea kwa maboya wengine.

Wanaonunua mikojo ya waja wazito wengi wao sio kwa ajili ya ushirikina bali kwa ajili ya kuwapiga mabazazi. Najua umesoma huku ukikumbuka pesa ulizotoa kwa ajili ya abortion huku ukijisifu kwa wanaume mwenzako kuwa una mbegu Kali sana.. Ukigusa tu kitu na box unaibiwaaa
 
Back
Top Bottom