Mkojo hurutubisha ngozi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkojo hurutubisha ngozi?

Discussion in 'JF Doctor' started by Rutashubanyuma, Feb 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Mkojo hurutubisha ngozi
  [​IMG]

  Haji Kalili

  [​IMG] ZIPO hadithi nyingi za kale zinazoelezea matumizi ya mkojo wa binadamu na baadhi ya wanyama kwamba ni tiba mbadala.
  Wapo watu waliokuwa wakitumia tiba mbadala hiyo kupata nafuu au kupona kabisa maradhi tofauti yaliyokuwa yakiwasumbua.
  Hadithi iliyopokewa na Imamu Bukhari, mmoja wa wasaidizi wa Mtume, inaeleza kwamba baadhi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kwamba unywaji wa mkojo wa ngamia ni dawa.
  Katika hadithi nyingine ya Bukhari, Volume 7, kitabu cha 71, Ukurasa nambari 590: “ Anasimulia Anas: Hali ya hewa ya Medina enzi ya Mtume Muhammad (SAW), ilikuwa haiwakubali baadhi ya watu, kwa hiyo Mtume aliwaamuru kufuata muongozo alioutoa wa kunywa maziwa na mkojo wa ngamia kama tiba.
  Walimtii na kuanza kunywa maziwa na mkojo wa ngamia hadi afya zao ziliporekebishika.
  Katika hadithi nyingine ya Bukhari Volume 8, Kitabu cha 82, namba 797:
  “Anas Ibn Malik, anaendelea katika volume 8, kitabu cha 82 ukurasa namba 797: Kulikuwa na kundi la watu kutoka ukoo wa kikuraishi (au ‘Uraina’) walikuja Medina na wakaugua, Mtume Muhammad aliamuru watibiwe kwa maziwa na mkojo wa ngamia. Afya zao zilirudi kama zilivyokuwa awali.
  Katika mapokeo mengi kutoka kwa Bukhari na baadaye waandishi wengine tofauti tofauti, iligundulika kwamba mkojo ni tiba iliyokuwa ikitumika katika baadhi ya jamii nyingi zilizopita na katika miaka ya hivi karibuni kuna baadhi ya watu wameanza kutumia tiba hiyo ingawa si kwa kiwango kikubwa.
  Tamaduni nyingine zinavyoitafsiri tiba hiyo
  Nchini China, mkojo wa watoto wadogo unachukuliwa kama tiba mbadala.
  Kusini mwa Uchina, watoto wachanga wanaoshwa uso na mkojo ili kuipa ngozi kinga kutokana na mionzi mbalimbali mara wanapozaliwa.
  Nchini Ufaransa, kuna aina fulani ya soksi inayotumbukizwa kwenye mkojo na kuzungushwa shingoni mwa binadamu kama njia ya kurekebisha mwenendo wa koo.
  Mnamo karne ya 17, kulikuwa na aina ya kabila la wanawake wenye kipato kikubwa wa Kifaransa waliokuwa wakioga kwa kutumia mkojo ili kujiongezea mvuto.
  Katika mji wa Sierra Madre, ulioko Mexico, wakulima huwa wanaandaa mchanganyiko wa mifupa ya wanyama na mikojo ya watoto, na baadaye hujipaka mchanganyiko huo kwenye ngozi kama tiba mbadala ya kurutubisha ngozi na kuikinga na magonjwa.
  Kwa wakazi wa kale katika Jiji la Roma, Italia, mkojo ulikuwa ukitumika kung’arisha meno, hata kama utatumika mkojo ambao si wako.
  Mwandishi John Henry Clarke wa jarida moja nchini Marekani aliandika, “…binadamu ambaye ngozi yake imeathirika, anywe mkojo wake wa kwanza anapoamka asubuhi.
  “Kama dalili zinaonyesha ameathirika sana na amekuwa dhaifu, mkojo utamsaidia kurudi katika hali yake ya awali”.
  Historia inatukumbusha kwamba tiba mbadala ya mkojo imetumika sana nchini China miaka ya nyuma.
  Watabibu wa kale wa Kichina walitibu majeraha kwa kutumia mikojo kwa kumwagia kwenye vidonda vipya na utabibu huo inaelezwa ulienea kwa haraka
  Mashariki ya Mbali.

  Mkojo pia unarahisisha usagaji wa chakula unaponywewa mapema asubuhi.
  Una virutubisho gani?
  Watumiaji wa tiba mbadala ya mkojo wanasema yanapatikana maji na urea ndani yake. Mkojo pia una mamilioni ya chembechembe za homoni, metaboliti na corticosteroidi.
  Mkojo pia una virutubisho vingine vingi kama Vitamini C.
  Katika simulizi tofauti tofauti inaelezwa kuwa mkojo na urea kwa wanaotumia kama tiba mbadala inasaidia kupunguza maambukizi ya saratani mwilini.
  Vimelea vya kansa vinaweza kusafirishwa kwa njia ya mkojo, sasa kwa kutumia mkojo kama kinywaji, vimelea hivi vinaweza kuingia kwenye mfumo wa kinga mwilini na kusaidia urutubishwaji wa kinga mwilini ‘(antibodies)’.
  Ushahidi wa watumiaji
  Mwaka 1978, aliyekuwa Waziri Mkuu wa India, Morarji Desai, mmoja wa watumiaji wa muda mrefu wa tiba mbadala hii, katika mazungumzo yake na mwandishi Dan Rather katika dakika 60 alielezea faida walizozipata mamilioni ya Wahindi waliojitibu kwa tiba mbadala hiyo.
  Mcheza filamu wa Kiingereza, Sarah Miles, alikunywa mkojo wake kwa zaidi ya miaka 30 akiamini kwamba unamsaidia kujenga afya siku hadi siku.
  Mcheza baseball Moisés Alou, alikuwa akiikojolea mikono yake akiamini itamsaidia kutoteleza kwenye mpira mara anapoukamata.
  Mwanamuziki Lady Madonna yeye akihojiwa katika kipindi cha ‘Talk Show’ alielezea jinsi alivyoweza kujitibu majeraha ya miguuni mara anapomaliza kufanya mazoezi ya kukimbia.
  Mpiganaji wa michezo tofauti (Mixed Martial Arts), Lyoto Machida, alikiri katika mahojiano kwamba anakunywa mkojo wake.
  Mwanamasumbwi Juan Manuel Marquez alikuwa akinywa mkojo wake wakati akijiandaa na mpambano baina yake na Floyd Mayweather.
  Mchezaji bingwa wa taekwondo wa Marekani, Adam Paolino, naye ni mtumiaji mzuri wa mkojo wake akiamini unamsaidia kutibu majeraha anayoyapata akiwa mazoezini.
  Ushauri kuhusu tiba hii
  Inashauriwa unapoamka asubuhi kabla ya jua kutoka, unaweza ukanywa japo glasi moja ya mkojo, inasaidia kuimarisha afya.
  Wahindu wa kale walishauri unywaji wa mkojo kabla ya jua kutoka kama njia moja ya kuimarisha afya mwilini.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  This is a piece of bulshit........................haiwezekani mkojo uliorindima na uchafu uwe tiba bila ya kudhuru figo...........................be smart and stay away from this baloney...................
   
 3. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  kaka amini usiamini. hiyo ni dawa ya ukweli.
   
 4. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pia mkojo ni dawa ya vidonda vya tumbo! Jaribu kama unavyo asubuhi piga hiyo glasi unayoitoa na uendelee utaona!
   
 5. kasopa

  kasopa JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu mbarikiwe sana kwanza kabisa nawatahazarisha na vitabu kuna watu wanachafua hii dunialia kuna mitume wamekuja wauongo hili kila mtu analifaham chakushangaza Dini ya Islam inasema mkojo ni najisi niuchafu iweje mtume wa mungu leo awaambie waumini zake wanywe mkojo ilihali mungu wake amesema ni uchafu sikuhizi kumekuwa na kila namna ya udanganyifu watu wanatumia sana dini kufankisha mambo yao sizani hata kwenye dini ya Kristo inakuba hili sikuhisi nikuwa makini sana na hawa jamaa, chakushangaza viongzi wa madhehebu wanaangalia tu hawkemei dini za ajabuajabu zinaibuka watu wanatepeliwa inatakiwa vitabu kama hivi isiruhusiwe katolewa mungu katuumba kwamfumo wa kusafisha mwili kwa njia ya haja ndogo na haja kubwa leo unaambiwa dawa hee, kazikwelkwel
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mwili umeumbwa kutupa uchafu nje kwa njia ya haja kubwa na mkojo. Kwa hakika ni kinyume cha maumbile (nature) kunywa mkojo au kula kinyesi - eti ni dawa za maradhi fulani!
   
 7. JANGWANK

  JANGWANK Member

  #7
  Sep 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachofahamu mkojo ni uchafu (najis) Nitafanya utafiti juu la hili swala! Kwa sasa siegemei upande wowote!
   
 8. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,978
  Likes Received: 6,621
  Trophy Points: 280
  amin usiamin mkojo unatibu ngozi.mia
   
 9. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Unatibuje?
   
Loading...