Upandikizaji mkojo ni inakuaje?

Upandikizaji mkojo ni inakuaje?

Apiwe

Member
Joined
Jul 12, 2026
Posts
8
Reaction score
15
Asubuhi

Kuna jamaa amepata dharula hapa mtaani na kukimbizwa hospital na baada ya uchunguzi jamaa amegundulika kuwa kibovu cha mkojo kimeziba.

Katika tiba ikawa kama inashindikana kutokana na gharama za matibabu na wafanisi wetu wa tiba hiyo hii imetokea hapa Dar.

Ndugu wa jamaa wakawa wanahusisha jambo hilo na Imani potofu , ikabidi wamuwaishe kwao Mwanza so atapelekwa hospital za huko, nasikia jamaa anakojoa vimkojo vyeusi na anatapika maji meusi mwanzo madoctor walidhani ni limonia lakini sio.

Wakuu nilikuwa nauliza dalili hizi zinaweza kuwa matatizo hayo yanasababishwa na Nini? Kibofu cha mkojo kuziba na hili la kupandikizwa mkojo ni nini? Hasa sababu na inakuaje? Kuaje? Kupandikizwa mkojo.

Kwa ambao wamewahi kusikia ugonjwa huyo na wanaojua tu usizue taharuki.

Asante
 
Suala la jamaa yako linaweza kueleweka kwa kuzingatia dalili zake na umri.
Kuna mambo mengi kwenye njia ya mkojo yanayoweza kusababisha mkojo usitoke:
1: uwepo wa vijiwe kwenye njia ya mkojo
2: makovu ya maambukizi ya siku za nyuma hasa kutokana na magonjwa ya zinaa au ajali ndani ya njia ya mkojo.
3: uwepo wa damu iiyoganda kwenye njia ya mkojo
4: maambukizi ya kibofu cha mkojo
5: Tezi dume
6: Uwepo wa mayai ya minyoo inayosababisha kichocho
7: Nk.

Upandikizaji wa mkojo ni kitendo cha kuuchukua mkojo na kuuweka kwenye kiotea/medium ili wadudu walioko kwe mkojo husika waweze kuzaliana. Kiotea husika huwekwa kwenye mazingira ya kuwawezesha wadudu hao kuota/kuzaliana. Baada ya hapo, wadudu husika hutambuliwa kitaalamu na kufanyiwa majaribio ili kugundua kama wana usugu na dawa yoyote na ni dawa ipi inayoweza kuwaangamiza/kuwaua.
 
Back
Top Bottom