Mkoa wa Tabora upunguzwe ukubwa

Mkoa wa Tabora upunguzwe ukubwa

Ili kuharakisha maendeleo, utazamwe uwezekano wa wilaya ya Iramba, Nzega na Igunga kuunda mkoa mpya. Mkoa wa Igunga.
 
Kuanzisha mkoa mpya ni gharama, hasa ukizingatia mkoa unaoanzishwa na mkoa unaomegwa una vyanzo gan vya mapato,vitakavyo tosheleza kuendesha shughuli za kimkoa.mi nazani igunga ihamishiwe singida au shinyanga,Nzega,urlyankhulu ya kaliua na eneo dogo la uyui zihamie kahama.
 
Ili kuharakisha maendeleo, utazamwe uwezekano wa wilaya ya Iramba, Nzega na Igunga kuunda mkoa mpya. Mkoa wa Igunga.
Wenzetu burundi wanapunguza mikoa kutoka 18 ya sasa hadi mitano sisi tuna waza kuongeza.utakuja mtu na hoja burundi nindogo sawa na mkoa mmoja wa tanzania,nikweli.lakini kama tuna ongeza tuzingatie population,uwezo wa kiuchumi,geographia na isiwe utash wakisiasa pekee kama ilivyo zoeleka.
 
Vip Barbara za moro mfano huko mlimba zinapitika kweli? Tuweke probox zetu
Mkuu ni baadhi ya vipande korofi,syo haba serikali imejenga lami na kumwaga changarawe. noah ndyo usafiri mzuri na wa haraka kwa maeneo yale.
 
Hivi morogoro mnaijua vizuri kweli wadau? Kutoka moro mjini mpaka mlimba ni kilomita 395.hapo utaona namna gani watu wanapata ugum wa kufuata huduma za kijamii. waangalie na huu mkoa ase
Cha muhimu ni kufikisha huduma kwa wananchi bila kubagua kutokana na mahitaji yao. Badala ya kugawa mikoa mimi naamini twende na sera ya kuunganisha mikoa na kuja na mfumo wa utawala wa MAJIMBO. Tuwe na majimbo 8-10 na kila jimbo na serikali yake vyote chini ya serikali kuu.
 
Mkuu ni baadhi ya vipande korofi,syo haba serikali imejenga lami na kumwaga changarawe. noah ndyo usafiri mzuri na wa haraka kwa maeneo yale.
Lami imewekwa lini kwenye barabara ya Mlimba ?
 
Mkoa wa Tabora ni mkubwa sana! Kuna vijiji hata mkuu wa mkoa amalize muda wake kuvifikia ni ngumu.

Mkoa wa Tabora mkiupunguza na kutengeneza mikoa mtasaidia kufikisha huduma, leo nimeshangaa kuona watu Tabora kama Kaliua wakija Kahama kupata huduma ya afya.

Tabora kuna wahamiaji wengi wamejificha huko ususani warundi, wanyaruanda na wakongo, kuna vijiji na mapori mengi mpaka kuna sehemu huduma ni ngumu kufikia.

Serikali tambueni ili.
Naomba kidogo nipingane na wewe maana nilikuwa Tabora ktk mradi wa maji nafikiri utendaji wawatendaji wetu ndio changamoto, sababu ya mtu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine kupata huduma hiyo sio changamoto ya ukubwa wa eneo hayo nimapungufu ya upatikanaji wa huduma stahiki.

Kwa mfano kuna watu wanatoka Mbozi songwe kwenda kutibiwa Ikonda Hospital Njombe sasa hapo shida ni ukubwa au huduma? Mimi ningalifikiri kwanz akuboreshwe utendaji na miundo mbinu hafafu ndio tuone changamoto ya kieneo, au Nchi ikatwe kimajimbo itasaidia kuboresha usimamizi ktk utendaji wa watendaji, kusema ukweli uwajibikaji wa kiserekali umekuwa na uzembe sana kuliko tunavyo aminishwa na wana siasa amabao ndio wamekuwa na nguvu kuliko watendaji.
 
Ok,kwaio hamna jinsi probox itapiga Kazi maeneo ya huko
Mkuu ni baadhi ya vipande korofi,syo haba serikali imejenga lami na kumwaga changarawe. noah ndyo usafiri mzuri na wa haraka kwa maeneo yale.
 
Mwisho wa siku tungekuwa tu na mfumo wa majimbo, ili kuchochea maendeleo. Maana kila Jimbo litakuwa na Kiongozi wake wa kuchaguliwa na wananchi wa Jimbo husika. Kuendelea kugawa maeneo ya kiutawala, kunaongeza tu mzigo kwa walipa kodi.

Maana hao Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Ma RAS, DAS, wa kusimamia hiyo Mimo na Wilaya mpya, watatakiwa kulipwa mishahara minono, kupewa magari ya kifahari ya kutembelea, nyumba za bure za kuishi! nK. Huku vyeo vyenyewe vikiwa ni vya kisiasa tu.
 
Mkoa wa Tabora ni mkubwa sana! Kuna vijiji hata mkuu wa mkoa amalize muda wake kuvifikia ni ngumu.

Mkoa wa Tabora mkiupunguza na kutengeneza mikoa mtasaidia kufikisha huduma, leo nimeshangaa kuona watu Tabora kama Kaliua wakija Kahama kupata huduma ya afya.

Tabora kuna wahamiaji wengi wamejificha huko ususani warundi, wanyaruanda na wakongo, kuna vijiji na mapori mengi mpaka kuna sehemu huduma ni ngumu kufikia.

Serikali tambueni ili.
Basi toa mapendekezo!!!!!
 
Hivi unajua hata hii SGR Mwanza-Isaka (Kahama) wala haiishii Isaka bali inaishia Iboja kata ya Sigili (Nzega).

Nahisi sehemu ya Nzega DC inaenda kumegwa iwe Msalala DC (Kahama).

Juzi Dr Mpango kaenda kuweka jiwe la msingi SGR Isaka-Tabora pale mji wa Isaka viwanja vya parking ambako reli hata halitafika.

Kwenye karatasi station itakuwa Isaka-Kahama ila kinachoendelea site,station itajengwa Iboja-Nzega na maeneo yameshatwaliwa.

Je hakutakuwepo mgogoro ukusanyaji mapato kati ya Nzega DC na Msalala DC kwa station kujengwa Nzega huku kwenye makaratasi station ipo Msalala?
 
Wenzetu burundi wanapunguza mikoa kutoka 18 ya sasa hadi mitano sisi tuna waza kuongeza.utakuja mtu na hoja burundi nindogo sawa na mkoa mmoja wa tanzania,nikweli.lakini kama tuna ongeza tuzingatie population,uwezo wa kiuchumi,geographia na isiwe utash wakisiasa pekee kama ilivyo zoeleka.
Ni Sawa kwa Burundi kupunguza mikoa maana kwa nchi ya Burundi hakuna barabara yenye umbali wa km zaidi ya 250 ukizidi hapo ujue upo nje ya Burundi...

Sasa mikoa yote 18 ya nn?
 
Back
Top Bottom