Mkoa wa Mara kulikoni, serikali imeusahau?

Mkoa wa Mara kulikoni, serikali imeusahau?

Unataka ziara za viongozi wenu hao waropokaji ili iweje? Sisi watu wa Mara huwa hatuvumilii kauli za kipuuzi wakija huku wasiongee kauli zao za kibabe tutawanyoosha.

By Kamanda wa KIRIBA kwa sasa ARUSHA

Wewe uko Arusha mambo ya Mara huwezi kuyajua vema
 
Watu wa Mara wanahitaji majibu ya maswali yao, kama mkuu wa kitengo toa majibu ili sie wengine tuache kukatisha tamaa la sivyo majibu yetu yataendelea kuwa majibu mujarabu
Mkuu hapo sijakusoma !!!!
 
Jk alikuwa anaenda mkoa mara lkn likizo ya kupumzika pale serengeti parks. Mh pombe sidhani atakanyaga mara. Maendeleo ndo hakuna kabisa airport ni mashimo tu. Rami ni pale mjini pekee ake. Wabunge wote wa mkoa vilaza kasoro Muhongo tu ila wote wehuu.kitu kingine tuna wabunge wengi wa upinzani serikali imetuzira. Mkoa umesahaurika.
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa. Wabunge wa upinzani kutoka Mkoa wa Mara hawajielewi kabisa, wanapiga domo la siasa, wakati Mbowe na wenzake huko Kilimanjaro, Arusha na Manyara wanawatu wanawasaidia kimaendeleo, pia kule walishapiga hatua miaka mingi. Mara jiongezeni kiakili kidogo ili muone mnavyotumika kudumiza maendeleo
 
Kwani Mara iko geita? Ama mmeambiwa ni sehemu ya Mwanza?
Baba wa Taifa hakubagua wala kupendelea. Ucha mungu na upendo wake kwa Watanzania wote ulimgharimu yeye binafsi na mkoa wa Mara. Nyumba tu ya kuishi alijengewa baada ya kustaafu. Hakupeleka miradi ya maendeleo alikotoka kiupendeleo kama tulivyoshudia ktk awamu za serikali zilzofuata na tunavyoendea kushuhudia sasa. Aliwazia Tanzania na Watanzania.
NGOs wakileta miradi ya maendeleo nchini, haielekezwi mkoa wa Mara. Mkoa mzima barabara pekee ya lami ni ile inayounganisha Tanzania na Kenya. Makao makuu ya wilaya zote sita hana lami kuacha kilomita chache tu zinaelekea "bomani".
Labda dhambi ya wananchi wa huko ni kuwa "ving'ang'anizi" wa haki zao. Wananchi wa Mikoa ya Kusini wamerudisha heshima baada ya kusema "haitoki". Mikoa ya Shinyanya na Mara ni tajiri wa madini lkn hawafaidiki nayo. Inachumwa tu na kuachwa bila miradi mikubwa ya maji wala barabara.
Maji yametoka Ziwa Victoria hadi Kahama kuhudumia migodi wananchi wa maeneo yalipopita mabomba wakiachwa bila maji. Wananchi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wasingestahili kuwa na shida ya maji.
Hapa si suala la kuchaguliwa wabunge kutoka upinzani. Serikali ya CCM inatumia hoja hiyo kuwajengea wananchi chuki dhidi ya vyama vya upinzani. Ni hoja ya kipuuzi. Vyama vya upinzanl vina chini ya miaka 25 tangu kuruhusiwa nchini. Kimahesabu vimeongoza kwa muda mfupi na sehemu ndogo sana nchi nzima ikilinganishwa na chama tawala.

Kuna madai ya kupatikana maendeleo makubwa tangu nchi ipate uhuru wa kujitawala. Tuseme imepiga hatua. Maendeleo yanayodaiwa kupatikana hayalingani na ya miaka 53 ya uhuru na utajiri tulio nao. Tunajilinganisha na nchi zipi? Kiongozi pekee aliyekuwa "visionary" ni Nyerere. Huyu aliyeko madarakani hujui anaelekea wapi!

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mkoa wa Mara alitoka Baba wa Taifa, ingawa ni Mkoa ulioko nyuma kimaendeleo.
Katika awamu hii bado sijasikia kiongozi wa serikali walau akiwa ziarani huko na walau kutoa ahadi ya kimaendeleo kwa mkoa. Mkoa unahitaji maji kwenye wilaya zote, barabara, uboreshaji wa elimu na afya, eneo la epz, umeme

Ndugu mkoa wa Mara una shida ya ndani ya mkoa wenyewe hata si serikali, unayotaka kuitupia lawama. Sasa mnatakaje maendeleo wakati mnafukuza wawekezaji? Kwa mfano wilaya ya Rorya na Bunda nimesikia kuna mwekezaji alikuja kuwekeza kwenye sekta ya Maji kwa kufufua miundombinu ya maji ya Shirati na Nyamuswa. Shirati alivyosaini makubaliano akaweka mkandarasi na kununua mabomba mkamfanyia mizengwe mpaka leo hii hajaanza kazi. Kwa upande wa Nyamuswa Bunda mwekezaji alifufua miundombinu maji yakaanza kutoka mmeanza kumfanyia vitimbwi vikiongozwa na mbunge wenu Boniface ili amtoe mwekezaji aweke kampuni yake kwa kushirikiana na mkurugenzi wa Halimashauri ya Bunda bwana Kusaja.
Halafu unakuja hapa JF kulia lia wakati mchawi ni wana Mara wenyewe.
Mkitaka maendeleo badilikeni acheni ujuaji na ujanja pori wa kusumbua wawekezaji.
 
Huyo mwekezaji gani mbona mimi sijamwona. Nipe details nifuatilie
 
Mkoa wa Mara alitoka Baba wa Taifa, ingawa ni Mkoa ulioko nyuma kimaendeleo.
Katika awamu hii bado sijasikia kiongozi wa serikali walau akiwa ziarani huko na walau kutoa ahadi ya kimaendeleo kwa mkoa. Mkoa unahitaji maji kwenye wilaya zote, barabara, uboreshaji wa elimu na afya, eneo la epz, umeme
Maendeleo yako jitahidi ujiletee wewe mwenyewe
 
Mkoa wa Mara alitoka Baba wa Taifa, ingawa ni Mkoa ulioko nyuma kimaendeleo.
Katika awamu hii bado sijasikia kiongozi wa serikali walau akiwa ziarani huko na walau kutoa ahadi ya kimaendeleo kwa mkoa. Mkoa unahitaji maji kwenye wilaya zote, barabara, uboreshaji wa elimu na afya, eneo la epz, umeme

Utasemaje Mkoa wetu wa ' Mara ' umesahaulika wakati kila kukicha Mzee Stephen Wassira anautangaza ' mubashara ' kupitia Rufaa zake dhidi ya Dada yetu Esther Bulaya? Unataka Mkoa wetu wa Mara utangazwe au ukumbukwe vipi uridhike?
 
Acha matusi vijana, msifikiri wote mmezaliwa Dar. Jifikirie vizuri mmetoka mikoani gani, japo mtaficha lakini wapo waliotokea Sumbawanga, Kigoma, Rukwa, Njombe, Songea n.k. karibia mikoa yote hali ni ngumu ukitoa majiji
Sana tata tambatembilia aba mura bayo
 
Wapiga Virungu Na Kwata Wengi Wanatoka Huko. Huenda Laana Ya Machozi Ya Wapigwaji Inautafuna Mkoa Huo.
 
Wanalima sana bangi wakiacha mkoa utakuwa na maendeleo
Afu Bange ina soko balaa. Nashangaa Serikali inawakomalia walime pamba ingali haina soko; bei cheee!

Wacha watu walime Bange bhana. Afu tuna park vzr tuna andika FOR EXPORT ONLY.
 
[
Huyo mwekezaji gani mbona mimi sijamwona. Nipe details nifuatilie
Boma2000 hauko fair. Nchi nzima wenye matatizo na wajuaji wasiostahili kupelekewa maendeleo ni watu wa mkoa wa mara. Unaishia kusema umesikia! Umesikia mangapi na yote uliyoyasikia ni ya kweli? Nahisi unatoka wilaya ya Chato ambayo itakuwa mkoa kabla ya 2020.
Nyerere angekuwa kiongozi mwenye ubinafsi na upendeleo kama watu wa kutoka sehemu za Chato, tusingekuwa tunaongelea maendeleo duni ya mkoa wa Mara.
 
Fanyeni kaz achen kulalama kama mademu na kumusingizia mwenye heri nyerere mwachen apumuzike

Maendeleo yanaletwa kwa kufanya kaz wala siyo kulalama lalama
 
Mlichezea nafasi kwa zaidi ya miaka 20 mlidhani watakaofuata watawakumbuka? Lakini hata kama mkipewa nafasi majungu, dharau, ujuaji, maringo tele huku vijiji mnakotoka vikiwa hooooi bin taaban. Poleni sana akika masika, mura, chikaka, mwamba, chikomati, jaduong, nk.
 
Utasemaje Mkoa wetu wa ' Mara ' umesahaulika wakati kila kukicha Mzee Stephen Wassira anautangaza ' mubashara ' kupitia Rufaa zake dhidi ya Dada yetu Esther Bulaya? Unataka Mkoa wetu wa Mara utangazwe au ukumbukwe vipi uridhike?

Naona wewe utakuwa mtu wa kanda ya Kaskazini, mmezui hata lami kupita serengeti kwa kisingizio cha wanyama. Nyie ni Wabinafsi sana.
 
Acha matusi vijana, msifikiri wote mmezaliwa Dar. Jifikirie vizuri mmetoka mikoani gani, japo mtaficha lakini wapo waliotokea Sumbawanga, Kigoma, Rukwa, Njombe, Songea n.k. karibia mikoa yote hali ni ngumu ukitoa majiji
Wewe unataka kufananisha Njombe na Mara umepotea mkuu.

Hebu nenda Njombe mkoa umeanzishwa miaka ya karibuni lakini haulingani na hio Mara yenu.

Watu wa Mara endelea kuisoma namba.
 
Back
Top Bottom