Mkoa wa Kilimanjaro unashangaza kidogo

Mkoa wa Kilimanjaro unashangaza kidogo

Wa kudis na ant Chagga Wakauja muda si mrefu! Nakumbuka enzi za kahawa ikiwa na soko zuri 1970's- 1999's wazee wengi wa kichaga walitumia fursa vizuri kusomesha watoro wao shule za binafsi!! Kumbuka kilimanjaro 68% ya shule zake ni za binafsi hivyo wazee walimudu kulipa ada vizuri tofauti na mikoa mingine. ....Ni kawaida sana kwa watoto wa mkoa kilimanjaro kusomeshwa na wazee mean babu zao kwa hela ya kahawa

Uwepo wa kahawa na mpaka wa Kenya ulifanya kilimanjaro kua soko zuri la bidhaa toka kenya kama KIMBO, JAMAA, KIWI, bia za kopo toka kenya hivyo mzunguko wa pesa ulikua vizuri! ......Hapa biashara ya magendo kwa kutumia Toyota Staut na Land Rover 109 zilinogesha sana biashara hii!
Kiukweli wakazi wa Kilimanjaro ni watumiaji wazuri wa fursa hasa bidhaa kutoka kenya,Utalii na madini mkoani Arusha!
 
IMG_3291.JPG
ukipiga chura teke unamuongezea mwendo!
 
Kijiografia ni Mkoa mdogo sana.
Kwa Tanzania bara, ndio unaofutia kuwa na eneo dogo baada ya Dar Es Salaam.

Huu mkoa una Wilaya Saba(regardless eneo lake).

Kingine huu mkoa mdogo una shule za Secondary 316.
Hakuna mkoa mwingine wenye Shule nyingi hivi, mingine hata ukiinganisha.

Huu mkoa ndio unaongoza kwa ufaulu. 2017/2018.

Huu mkoa Makao makuu yote ya wilaya zake yameunganishwa kwa barabara za lami.
Na barabara nyingi za kitarafa pia zina lami.
Barabara za kwenda wilaya ya Rombo ambayo iko pembezoni kidogo ni mbili na zote zina lami.

Naona kuna mengi yakujifunza Kilimanjaro.
Vijiji vya mkoa wa Kilimanjaro vina maendeleo kuliko vijiji vya mikoa mingine.

CCM na Serikali yake wanapaswa kuwekeza zaidi ndani ya Kilimanjaro, kwasababu ukiwekeza Kilimanjaro unaendeleza Tanzania.

Huu mkoa Ndio Lango la Tanzania...
Nawasilisha
Naomba nikusahihishe mkoa wa kilimanjaro Una wilaya sita na sio Saba, halmashauri Ndio ziko Saba, wilaya zake ni same, mwanga, siha, hai, rombo na moshi ambayo ina halmashauri mbili halmashauri ya manispaa ya moshi (moshi) na halmashauri ya Wilaya ya moshi (vijijini), kuna sehemu umeshauri ccm wawekeze kilimanjaro Kwani wakiwekeza huko watakua wameleta maendeleo tanzania, je hivi wakiwekeza sehemu nyingine watakua hawaleti maendeleo tanzania, by the way ccm haifanyi uwekezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijiografia ni Mkoa mdogo sana kwa Tanzania bara, ndio unaofutia kuwa na eneo dogo baada ya Dar Es Salaam huu mkoa una Wilaya Saba(regardless eneo lake).

Kingine huu mkoa mdogo una shule za Secondary 316 hakuna mkoa mwingine wenye Shule nyingi hivi, mingine hata ukiinganisha huu mkoa ndio unaongoza kwa ufaulu. 2017/2018.

Huu mkoa Makao makuu yote ya wilaya zake yameunganishwa kwa barabara za lami na barabara nyingi za kitarafa pia zina lami
barabara za kwenda wilaya ya Rombo ambayo iko pembezoni kidogo ni mbili na zote zina lami.

Naona kuna mengi yakujifunza Kilimanjaro vijiji vya mkoa wa Kilimanjaro vina maendeleo kuliko vijiji vya mikoa mingine.

CCM na Serikali yake wanapaswa kuwekeza zaidi ndani ya Kilimanjaro, kwasababu ukiwekeza Kilimanjaro unaendeleza Tanzania.

Huu mkoa Ndio Lango la Tanzania Nawasilisha
Kilimanjaro ni Lango la Tanzania? Sijakuelewa hebu fafanua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nazani tunapaswa kuwa nao karibu kisha kujifunza kutoa Kwao kujua wamewezaje kupiga hatua na kufika hapo walipo!
Mfano wenzetu kule kuamka alfajiri na kuanza kufanya kazi ni desturi yao!
Yani alfajiri unakuta kwenye migahawa kila kitu tayari!
Nenda mikoa mingine uone sasa ndipo utaiona tofauti!
Migahawani chai ukienda mapema unaambiwa bado hadi saa 4 [emoji87][emoji87]
Huo nimewapa mfano mdogo tu!
Halafu wale wanafanya kazi kama punda,
Hawajui kupumzika wala kulala mchana!
Si mtoto mdogo wala Mzee kikongwe ni watu wa kazi angalia mikono Yao hadi vidole vimepinda kwa kufanya kazi!
Wanajua nini maana ya kuchumia juani na Julia kivulini!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom