Mkoa maskini kuliko yote Tanzania


Haya bana, wewe subiri tu mpaka mzungu aje akwambie. Jitahidi uchanganye na zako kidogo. Kuna vigezo vichache tu ambavyo vingekusaidia: kipato cha kaya, kipato cha mtu mmoja mmoja, upatikanaji wa huduma muhim katika mkoa, mfano, maji, afya, elimu, bara bara nk!
 
Hivi kigezo cha umaskini ni kutokuwa na bahari au maghorofa? For me singida beat almost a half of all regions In tz
 
Kudadeki..!
 

Asee niko njema. Tumia vigezo hivyo hivyo kuijadili shinyanga na utoe mifano halisi. Yaani nyie pamoja na kukamua mafuta ya pamba,samli, kutumia wanyama kwenye kilimo kwa kiasi kikubwa, miji na vituo vya biashara za ndani na nje still unasema shy is poorer. Kama ni huduma za jamii zitolewazo na serikali kama maji,hospitali na shule niambie penye nafuu ukiacha miundombinu ya mkoloni.
 
Kwa upande wangu nafikiri ni mkoa wa Pwani..kwani si umasikini wa chakula tu bali hata huduma za kia
afya na elimu..kama sisi pwani ya mwambao tunaishi kwa kutegemea bahari..
 
Wengine mtashangaa lakini ndivyo ilivyo. Kwa mujibu wa vigezo vya serikali miaka michache ilopita mikoa 5 masikini zaidi ni Kagera, Kigoma, Pwani, Singida, na Dodoma. Dodoma ndio uliotajwa kuwa Mkoa masikini zaidi na vigezo hivyo havikutajwa.
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina mikoa 32. Ukipanga mikoa kimaendeleo ni lazima utapata wa kwanza na wa mwisho.
Mi nadhani cha msingi ni kujadili kama mipango ya kuikwamua nchi kutoka kwenye umaskini uliokithiri inafanikiwa au la. Ni vizuri tukaelewa kuwa hata kwenye mkoa tajiri kuliko yote, maskini hohehahe wapo lukuki. Kazi ni kwako!!!
 
Arusha make wananchi wake hawana hata mavazi wanaishia kujifunika shuka
 

Kwa hiyo wewe ndio Tabora nzima?

Unaweza ukajaza ukurasa lkn bado suala likarudi pale pale kuwa naizungumzia Tabora na si mtu mmoja. Mimi sina dharau nimesema ukweli tu. Wewe umekurupuka mbio, ooh mimi nafuga samaki. Sawa, wewe mmoja ukiwa na gitaa nyumbani kwako ndio tupigie mstari kuwa watu wa Tabora woote ni wanakwaya?

Halafu mimi sina HELA dogo slow down, mimi nina FEDHA. Hela zinakaa mfukoni na mimi sina mfuko nina akaunti
 
Singida,Lindi na Mtwara sidhani kama watakosa kuingia top 5,ikifuatiwa na Dom.Hawa ndiyo mama wa umaskini tz waliko wekeza magamba.

mbona hi ulotaja ni mikoa ya watu flani wa pale mashariki ya kati
 
Hivi kuna mtu aliwahi kutembelea mkoa wa kusini pemba....nenda huko ndo utajua umasikini ni nini.
 
Tuache chuki jamani mkoa wa pwani unatia huruma!shime jamani tuwasaidie wenzetu hawa!!
 
Mkoa wa Kagera unaongoza kwa umaskini. Wahaya wanaishi kwa kula ndizi siku zote hawana hata mifugo kama mikoa mingine.
 
mbona watu wanakuwa defensive na offensive sana? mtu alie anzisha thread anatafuta maoni ya watu kuhusiana na mikoa ambayo ina shida ambazo zinatatulika kwa njia za siasa, meaning that a good political intervention may most likely result in a betterment of the lives of the people in that particular area. so bearing this in mind, let us contribute towards that with a positive outlook.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…