Mkoa gani unaongoza kwa mbu Tanzania?

Mkoa gani unaongoza kwa mbu Tanzania?

Mtalaam mmoja kutoka kituo cha utafiti wa malaria IFAKARA anasema hiyo ndiyo wilaya yenye mbu wengi kuliko zote Tanzania.
Anasema kabla kituo hicho hakijajengwa mahali hapo utafiti ulionyesha kuwa mkazi mmoja wa mji huo aling"atwa na mbu alfu 30 kwa usiku mmoja.

Baada kujengwa kwa kituo hicho hivi sasa angalau mtu mmoja anang'atwa na mbu alf 5 kwa usiku mmoja.
Hiyo ni baada ya kupewa elimu ya kupunguza mazalia ya mbu, msaada wa madawa na usafi wa mazingira.
Hukk ni hatari
 
Wadau, tunaomba kujua ni Mikoa ipi Inaongoza Kwa Mbu wengi TANZANIA. Mtu wangu wa Karibu AMECHOKA na MBU WA DAR, anataka Kuhama, sasa ili asije ruka Mkojo akakanyaga mavi, hebu changia Mikoa Mitatu hadi Mitano ili aiepuke.

Asanteni wadau.
MBU KWATAI
 
Dodoma nae muongeze

Pia tabora
Dodoma sijakaa sana hasa wakati wa masika, Tabora napo wapo wa kutosha Ila wa msimu wa mvua kwa Mjini mitaa ya Mwinyi, Kanyenye, Isevya na Ipuli mtaa wa Freemason mbu mwaka mzima
 
Dar kuna mbu mpk ukiwa na stress mnaweza kupiga story kusogeza muda..!! 😹
 
Jangwani Dar waulize wachezaji wa Yanga au wakaribie uone alama za kujikuna
 
Arusha hakuna mbu kihivyo na unaweza usiwaone . Hata ugonjwa wa malaria haupo sana, na mara nyingi ukiupata inakuwa ulitoka safari mkoa nwingibe umeupatia huko
Mikoa iliyoko kwenye miinuko mara nyingi haina mbu wengi or pengine wakawa nadra sana
Unless kuwa na madimbwi
 
Ifakara...

1756239003769.png

1756239023192.png
 
Wadau, tunaomba kujua ni Mikoa ipi Inaongoza Kwa Mbu wengi TANZANIA. MtoMtu wangu wa Karibu AMECHOKA na MBU WA DAR, anataka Kuhama, sasa ili asije ruka Mkojo akakanyaga mavi, hebu changia Mikoa Mitatu hadi Mitano ili aiepuke.

Asanteni wadau.
Mto wa Mmbu
 
Mkoa ambao kuna Mbu balaa ni Dar,Pwani ,Lindi na Mtwara baadhi ya maeneo.

Kama hutaki Mbu kaishi mikoa yenye baridi kali hasa Njombe (mjini,makete) ,Iringa (mufindi ,mafinga)
 
Back
Top Bottom