Mkitaka Kuwatia Pingu Viongozi Waliopita Shindeni Uchaguzi

Mwanakijiji unamaanisha wapinzani wasimkosoe au kumshauri Rais mpaka waje washinde Urais? Kweli mzee wangu unazeeka vibaya.
 
Labda hujaelewa nilichosema; kwanini awashtaki viongozi ambao wamemjenga yeye? Wao ndio walimpa nafasi kutumikia leo mnataka kweli ageuke awaume hata kama anajua wana makosa? Atamshtaki Mkapa kwa "nia" gani? au Kikwete kwa lipi.

Ndiyo maana nikasema hana nia.

Magufuli atakuwaje na nia ya kumshtaki Mkapa, mtu aliyemuweka pale?

Binafsi ninaamini kama wengi ambao tumekuwa tukipigania mabadiliko ya nchi hii mtu kama Mkapa alitakiwa ashtakiwe miaka mingi sana nyuma, Kikwete ndio usiseme, Lowassa ndio duh! Miye sina tatizo kabisa na hawa wote kushtakiwa kwa makosa mbalimbali. Tatizo ni kwanini tusubiri kiongozi wa CCM aje afanye mambo ambayo ni ajenda ya upinzani?

Wanamtaka kiongozi wa CCM afanye hivyo kwa sababu serikali ya sasa inaongozwa na CCM.

Kwa sababu wanajenga ushawishi kwenye jamii kwamba CCM haifai, hata ikiambiwa kuwashtaki viongozi waliohusika, inaleta mchezo.Hata huyo Magufuli anayesifika analeta mchezo.

Kwa hiyo, ukisema wapinzani wanatakiwa kushinda uchaguzi,kumtaka Magufuli ashtaki wastaafu ni kujenga ushawishi kwamba Magufuli asipokubali, wananchi waone kwamba huyu hatufai na wachague wapinzani.

Kwa hiyo kumtaka Magufuli ashitaki marais wastaafu kunaweza kabisa kuwa ni sehemu ya kujenga ushawishi ili kushinda chaguzi.
 
Mzee mwanakijiji kutoka kuwa mtetezi wa wanyonge mpaka kuwa mtetezi wa wanyonyaji ni udini ni ukabila au tatizo ni nini
 
Mkuu Mwanakijiji hivyo unachotuambia ni kuwa sisi wananchi wa kawaida tusio na tiketi za vyama hatuna anayetusikiliza? Yaani hata tukiiomba serikali itujengee choo kwenye shule yetu ya kata basi Tushinde uchaguzi?? Yaani unatufundisha kuwa Ukishashinda uchaguzi basi unaweza kufanya chochote na kukataa chochote hata cha msingi? Hiyo ndiyo maana ya ule "Mfumo" tuliohubiriwa na "Wapinzani"? Ule uliomdhibiti Magufuli asifurukute kuunga mkono hoja za wapinzani ambazo leo anaonyesha wazi kuwa zilimkuna? Je akitekeleza hayo matakwa ya wapinzani(tayari baadhi) ccm watamfukuza kwa kosa la kutekeleza ilani isiyo yao? Kumbuka Magu Hapangiwi cha kufanya! Wewe unampangia!
 
Kitu kibaya zaidi ambacho mimi nawashangaa hawa wapinzani wenzangu ni kwamba eti wanataka Magufuli aje aombe msamaha kwa wapinzani kwa namna ccm ilivyosababisha mikataba mibovu kabla yake,,is it possible??? ? Yaani hata ajenda ya maana hawana hawa viongozi wetu,wamekaa kusubiri madhaifu ya ccm ili iwe ajenda.ndio maana wengine tumeamua tu kuwa waangaliaji ,
 
Kwa hiyo hata kuwasema tu majina yao huko mbeleni kutahitaji kushinda uchanguzi...............!!

Hilo sio swali bali hilo ndio ukweli wenyewe. Hata akitoka Magu akaingia Polepole, msimamo wao chama tawala ndio huo nao wanaapishana nao.
Kama mnataka kuwa shtaki shindeni uchaguzi. Hili lawezekana kwa njia 2: Kupata wabunge wengi wa upinzani waweze kuzizima kelele za Ndiyoooooo na kuzidisha za Hapanaaaaa. Nimesikiliza hoja ka 2 hivi juzi kati kule bungeni. Sauti za Hapanaaa zimeanza kupanda. Kumbukeni, bunge lililopita halikuwa na nguvu ka hili.
Njia ya pili, ni ushindi wa uraisi kitu ambacho ni ndoto. Rais ataondolewa tu na kutokuwa na imani naye.
 
Winning team? Ungejua sasa hivi nafikiria namna ya kuongoza upinzani na kuachana na wapinzani uchwara hujui tu. Huwezi kuwa na upinzani unaotaka kutawala kupitia CCM badala ya kushinda uchaguzi.


Sidhani kama upinzani wanataka kutawala kupitia CCM, hata kwa namna yeyote ile unayoweza kutafsiri neno "kutawala". Upinzani wanachokifanya ni kumshauri na kumkosoa Rais tu. Mengine unawasingizia.
 
Mkapa au kikwete hawawezi kukubali Upinzani ushike madaraka hata wakishianda kwa kura milioni 40 Kwa mambo waliyofanya nyuma wako tayari raia wafariki katiba ya warioba tusahau haiwezekani Tume huru nayo haiwezekani hii ndo Afrika
 
Kitu kibaya zaidi ambacho mimi nawashangaa hawa wapinzani wenzangu ni kwamba eti wanataka Magufuli aje aombe msamaha kwa wapinzani kwa namna ccm ilivyosababisha mikataba mibovu kabla yake,,is it possible??? ? Yaani hata ajenda ya maana hawana hawa viongozi wetu,wamekaa kusubiri madhaifu ya ccm ili iwe ajenda.ndio maana wengine tumeamua tu kuwa waangaliaji ,
Ndiyo kazi ya upinzani! Na wanalipwa ruzuku kwa kazi hiyo,kama ambavyo polisi anavyosubiri uvunje sheria akukamate!
 
Kwangu sijali nani anatawala. Ninajali kama mambo hayaendi sawa!!

Mbona jana watu wamepigwa mkwara kuyasema majina ya hao wakubwa ........ na leo gazeti limefungiwa!!
Huwezi kusemahujalinani anaendesha gari, unajali kamagari litapata ajali.

Wanasema kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa.

Usipojali nani anaendesha gari, utaendeshwa na kipofu na ajaliitakuwa haiepukiki.
 
Mzee wangu Magufuri Rais wangu anafanya anachokiweza awa Marais waliacha madudu makubwa mpaka mzee Magufuri anayajua sema basi ubinadamu unamjia anamua afanye lilipo ndani ya uwezo wake
 
Ajenda za chadema ndio uhalisia zinabeba uzalendo wa watanzania asipozitumia atawekwa pembeni
 
Mwanakijiji hajawahi kuwa mtu mwenye akili sawa sawa

Thats why tokea nimetokea kumfaham huyu kanjanja always nimekuwa namuona kituko.

Unataka ushindi upi wa upinzan kwa mfano kuliko ule wa kuchukua majority of votes kisha tume zenu za kuwabeba za kina jecha kuja kupindua matokeo?
 
Back
Top Bottom