Mkitaka Kuwatia Pingu Viongozi Waliopita Shindeni Uchaguzi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,131
2,000
M. M. Mwanakijiji

Kuna ndugu zetu kwenye upinzani pamoja na kumpinga na kumkataa kwao kote Magufuli wanapenda awe kama Rais aliyetoka upinzani! Kwamba, yeye abebe ajenda za upinzani na hivyo aanze kukata tawi alilokalia na kuongeza mafuta ya kujikaanga mwenyewe.

Nimesoma mara kadhaa siku hizi za karibuni za jinsi gani wanataka Rais kuonesha uthubutu wake basi afanye a, b, na c ili wajue kweli amepania! Wanasema "apitishe Katiba ya Warioba", aondoe kinga ya marais waliopita, awakamate viongozi waliopita n.k Yaani, awe kama Rais aliyetoka kwenye upinzani akiwa na ajenda ya total reform ambayo mara nyingi hubebwa na chama cha upinzani.

Sasa huku ni kutokuwa wa kweli katika siasa. Hata sisi tuliomuunga mkono Magufuli hatukumuunga kwa sababu alikuwa amebeba ajenda ya upinzani; Magufuli hakuuza ajenda ya upinzani wala sidhani kama ana maslahi nayo. Sasa hili si la ajabu. yeye ametokana na chama tawala; chama ambacho - kama nitakavyoonesha na nilivyowahi kuonesha huku nyuma - kinahusika moja kwa moja na matatizo yetu mengi ya kiutawala leo hii. Yeye ni zao la chama hicho, yeye ametumikia serikali ya chama hicho, na yupo hapo alipo kwa sababu kubwa ya chama hicho.

Sasa kumdhania kuwa atakuwa ni Rais wa upinzani inashangaza. CHADEMA na wapinzani ambao wana ajenda yao ambayo wangependa waione inatokea ikiwemo Katiba Mpya, uwajibikaji, mabadiliko makubwa ya sheria na mifumo wasimtegemee Magufuli kuwafanyia kazi yao. Huo utakuwa ni uvivu na itakuwa ni sawa na kutafuta njia nyingine ya mkato ya kuingia madarakani!

Yaani, wao wawe wapiga kelele tu miaka nenda rudi, lakini wasishinde uchaguzi. Wasichukue Bunge, serikali za mitaa wala Urais lakini ajenda zao zitekelezwe tu! huu ni uvivu wa kisiasa na tusipoangalia ni unyonyaji wa aina fulani! Yaani, wao wao wawe wanasema tuu, wanasifiwa kwa kusema tu linapokuja la kufanya wajivuruge wenyewe halafu wategemee kiongozi wa CCM abebe ajenda yao, atekeleze ili wao waridhike!

Ombi langu ndugu znagu ni kuwa ili kutekeleza ajenda mbalimbali ikiwemo hata kuondoa kinga za Marais (kitu ambacho hakiwezekani labda kuiwekea mipaka mipya); kuwashtaki viongozi waliopita wakiwemo Marais n.k yanaweza kufanyika na kufanikiwa tu endapo itakuwa ni ajenda ya chama cha upinzani kilichoshinda Bunge!

Sasa, kama nilivyoandika juzi; hakuna njia ya mkato. Mkitaka kupitia mikataba yote, mkitaka kuwafunga wote, mkitaka kufanya yote ambayo wapinzani wanalalamikia njia rahisi na yenye kunyooka kama mstari - ni KUSHINDA UCHAGUZI.

Hakuna kubadili safari angani, hakubadili gia angani, na wala hakuna kubadili chombo cha usafiri! Shindeni uchaguzi vinginevyo endeleeni kuombea kiongozi wa CCM aje kuwaokoa kama mlivyofanya 2015 na mnavyoonekana kuendelea kufanya sasa 2017 na inavyowezekana mtafanya 2020!

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,921
2,000
Magufuli kama ana nia ya kushtaki marais waliopita hahitaji hata kuondoa kinga ya marais, kwa Kikwete anyway.

Kikwete alisaini mikataba ya ajabu tangu akiwa Wizara ya Madini. Hakuwa rais.Kinga ya mambo aliyoyafanya kama rais hairudikwenye uwaziri.

Tatizo Magufuli hana nia. Ameshasema atawalinda marais wastaafu.

Kitu kinachotuonyesha haya makelele yake yote ni mchezo wa kuigiza tu.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,778
2,000
Upinzani huu wa akina Tundu Lissu wa kupayuka hauwezi kuingia ikulu labda baada ya miaka 100
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,602
2,000
Anafurahia kujiunga na the winning team
hata kama hiyo winning team ni timu ya kibabe isiyofuata sheria
Huu sio ubabe bali ni ujinga uliokubuhu,
Ni wajinga tu!!
Itakuja siku ambayo mimi na wewe hatuijui ambapo wataomba ardhi iwafunike.
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,717
2,000
Upinzani upi utakachukua dola???? Hakuna upinzani wa kweli tz labda waganga njaa
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,131
2,000
Tatizo Magufuli hana nia. Ameshasema atawalinda marais wastaafu.

Kitu kinachotuonyesha haya makelele yake yote ni mchezo wa kuigiza tu.

Labda hujaelewa nilichosema; kwanini awashtaki viongozi ambao wamemjenga yeye? Wao ndio walimpa nafasi kutumikia leo mnataka kweli ageuke awaume hata kama anajua wana makosa? Atamshtaki Mkapa kwa "nia" gani? au Kikwete kwa lipi.

Binafsi ninaamini kama wengi ambao tumekuwa tukipigania mabadiliko ya nchi hii mtu kama Mkapa alitakiwa ashtakiwe miaka mingi sana nyuma, Kikwete ndio usiseme, Lowassa ndio duh! Miye sina tatizo kabisa na hawa wote kushtakiwa kwa makosa mbalimbali. Tatizo ni kwanini tusubiri kiongozi wa CCM aje afanye mambo ambayo ni ajenda ya upinzani?
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,808
2,000
Kwa hiyo hata kuwasema tu majina yao huko mbeleni kutahitaji kushinda uchanguzi...............!!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,131
2,000
Kwa hiyo hata kuwasema tu majina yao huko mbeleni kutahitaji kushinda uchanguzi...............!!
Kama lengo ni 'kusema tu majina yao" imetusaidia nini? Tumetaja majina yao miaka nenda rudi. Hatua zote mbalimbali zimechukuliwa na watu hawa hawa wa CCM. Daniel Yona, Basil Mramba, na wengine wengi wamefikishwa mahakamani na hawa hawa. Ndio hicho upinzani unataka? Kwamba wao wawe wapiga kelele tu lakini wasitawale!

Leo hii Chenge akikamatwa, Karamagi akitiwa pingu upinzani utafurahia kuwa "tumefanikiwa"?
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,808
2,000
Labda hujaelewa nilichosema; kwanini awashtaki viongozi ambao wamemjenga yeye? Wao ndio walimpa nafasi kutumikia leo mnataka kweli ageuke awaume hata kama anajua wana makosa? Atamshtaki Mkapa kwa "nia" gani? au Kikwete kwa lipi.

Binafsi ninaamini kama wengi ambao tumekuwa tukipigania mabadiliko ya nchi hii mtu kama Mkapa alitakiwa ashtakiwe miaka mingi sana nyuma, Kikwete ndio usiseme, Lowassa ndio duh! Miye sina tatizo kabisa na hawa wote kushtakiwa kwa makosa mbalimbali. Tatizo ni kwanini tusubiri kiongozi wa CCM aje afanye mambo ambayo ni ajenda ya upinzani?
Mbona Mwanawasa alimshitaki Chilumba ...............!!?

Ni maswala ya Principles tu!! Tanzania bado tuko kwenye HANGOVER ya ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI!!
 
Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,833
2,000
Labda hujaelewa nilichosema; kwanini awashtaki viongozi ambao wamemjenga yeye? Wao ndio walimpa nafasi kutumikia leo mnataka kweli ageuke awaume hata kama anajua wana makosa? Atamshtaki Mkapa kwa "nia" gani? au Kikwete kwa lipi.

Binafsi ninaamini kama wengi ambao tumekuwa tukipigania mabadiliko ya nchi hii mtu kama Mkapa alitakiwa ashtakiwe miaka mingi sana nyuma, Kikwete ndio usiseme, Lowassa ndio duh! Miye sina tatizo kabisa na hawa wote kushtakiwa kwa makosa mbalimbali. Tatizo ni kwanini tusubiri kiongozi wa CCM aje afanye mambo ambayo ni ajenda ya upinzani?
Kwa sababu upinzani kushinda ni ndoto......
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,808
2,000
Kama lengo ni 'kusema tu majina yao" imetusaidia nini? Tumetaja majina yao miaka nenda rudi. Hatua zote mbalimbali zimechukuliwa na watu hawa hawa wa CCM. Daniel Yona, Basil Mramba, na wengine wengi wamefikishwa mahakamani na hawa hawa. Ndio hicho upinzani unataka? Kwamba wao wawe wapiga kelele tu lakini wasitawale!

Leo hii Chenge akikamatwa, Karamagi akitiwa pingu upinzani utafurahia kuwa "tumefanikiwa"?
Kwangu sijali nani anatawala. Ninajali kama mambo hayaendi sawa!!

Mbona jana watu wamepigwa mkwara kuyasema majina ya hao wakubwa ........ na leo gazeti limefungiwa!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom