Mkimzingua ataunda chama chake

Kila mtu anahaki ya kutoa maoni yake. Kumpinga mtu kwa jambo fulani sio kumchukia. Kikubwa ni kuzingatia maslai ya Taifa.

Hili kundi limeibuka na kumkejeli Rais Samia Suluhu kwa kila hatua anayofanya. Uwepo wake ni takwa la kikatiba; sasa mlitakaje?
 
Hao vijana watapambana na sisi raia. Mama asiwe na presha nao. Sisi ndio tutakua ngao yake Mama yetu kipenzi, yeye apige kazi tu.

Mama yetu ambaye toka ameshika madaraka hata hajamaliza mwezi mmoja ila raia tuna amani tele moyoni (Hajagawa hela barabarani, hajaongeza mishahara wala hajaajiri waalimu bado). Ila roho zetu zimepata utulivu na mapumziko.

Tutapambana nao kama tulivyo pambana na Marehemu Mzee Wao, mpaka akapata stroke. Ikibidi hata kuwakeketa bila ganzi tutawakeketa tu.

Hii nchi ilikua imeshaangamia, ilifika hatua kiongozi wa serikali anageuza kanisa kuwa sehemu ya kwenda kuwachamba waongoza ibada mbele ya waumini wao. Mpaka unajiuliza huyu amekwenda kufanya ibada au amekwenda kuwashushua Ma Askofu au kwenda kusambaza propaganda???
 
Sasa mama ndio Rais na mwenye mamlaka yote... Wakae watulie.. Kama anaifanyia kazi manifesto ya CHADEMA kwa asilimia 100 ni kwa faida ya wote... Mkizidi kumzingua ataivunja serikali aunde chama chake agombee upya ..ASHINDE KWA KISHINDO awazingue vizuri sasa.... !!!!
Akifanya hivi atakuwa amezingua hasa!

Namwona Samia kama yule Joyce wa Malawi mwingine.

Amekosa subira sana.

Alitakiwa ajipange vizuri, na aanze na yale mabovu kabisa ya Magufuli kabla ya kujihusisha na haya yatakayomletea shida kubwa sana, na kufanya kazi yake iwe ngumu zaidi.

Nauliza: Haraka yote ni ya nini, si anayo miaka minne na ushee kujiimarisha vyema?

Lakini kuna somo kubwa kwetu hapa katika haya na Magufuli na Samia. Mfumo wetu wa utawala wa nchi ni mbaya kweli kweli. Yaani mtu mmoja anaingia, anabadilisha chochote anavyotaka, bila ya vikao wala nini?

Hii ni nchi au ni jalala?
 
acha mikwara mbuzi wewe eti kuna watu wamepewa hela nyooka raia hawataki kuona tunarudi tulikotoka kwenye utawala wa upigaji wa enzi hizo wameshaonjeshwa utamu wa kujitegemea na matokeo chanya kuonekana kwa vitendo na siyo maneno

enzi za porojo ziliisha enzi za jk sasa hivi watu wanataka matokeo
 
acha mikwara mbuzi wewe eti kuna watu wamepewa hela nyooka raia hawataki kuona tunarudi tulikotoka kwenye utawala wa upigaji wa enzi hizo wameshaonjeshwa utamu wa kujitegemea na matokeo chanya kuonekana kwa vitendo na siyo maneno

enzi za porojo ziliisha enzi za jk sasa hivi watu wanataka matokeo
Na wewe ni mmojawapo? Maana hata ulichoandika hakiakisi mada husika
 
Yatima hadeki
IMG_20210328_150940.jpg
 
Back
Top Bottom