Mkimaliza Kuwaondoa Wamachinga muanze kampeni ya Kuondoa Nyumba za Zamani zilizopo Pembezoni Mwa barabara

Tunapambana na vitu tusivyovielewa.
Kwani maisha ni nini hasa?
Je muonekano bora unakidhi haja ya maisha bora?
 
Kiukweli nimepita mitaa ya Morogoro nyuma ya NMB na maeneo mengine kweli machinga ilikuwa tabu na uchafu mtupu. Pale soko kubwa wamepangwa vizuri sana na kwa mpangilio na kila mtu yuko happy, na mitaani kunapitika fresh kabisa.

Hongera sana Morogoro kwa kazi nzuri. Sasa nawashauri mgeukie pale maeneo ya Fire napo wapangwe vizuri. Wale wauza mbao wa Fire waondoeni muwatafutie eneo kubwa kule jirani na stend mpya ya Daladala. Pale na kwenyewe muwapange vizuri wamachinga kulingana na bidhaa zao.

Mwisho mkumbuke kwamba kwa sasa hapo Morogoro KIHONDA ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wakazi wengi sana, hivyo tafuteni maeneo jirani na Kihonda lijengwe soko/cetre ya biashara. Laweza kuwa Msamvu, pembeni ya Kituo cha umeme au Kihonda Kanisani kwenye uwanja jirani na zile fremu nyingi za Chambo. Hii itapunguza watu kukimbilia mjini kule sokoni Kingalu au Mawenzi.
 
Huwa nashangaa hoja za kupendezesha mji. Unapendezesha mji ili iweje?

Yaani utese watu kwa kuwabomolea nyumba zao ili upendezeshe mji. Umpendezeshee nani na kwa sababu gani?

Mawazo ya kishamba kabisa.
 
Hao ndio wapiga kura wa ccm wanaoweza kulaghai kila namna na hata wauzaji wa shahada za kupigia kura ni haohao!
Hivyo sidhani kama CCM itaafiki pendekezo hili zuri!
 
Serikali ikimalizana na kuwaondoa Wamachinga waazae Campaign ya Kuondoa nyumba zote chafu na za zaman ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na maeneo yauzwe kwa Watu wenye uwezo wa kuweka nyumba za kisasa.

Hii itasaidia sana majiji mengi hapa Tanzania kuwa safi na kuwa na Muonekano mzuri.

Pembezoni mwa barabara zimejaaa nyumba nyingi ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na zinafanya majiji kuonekana hakuna mipango miji.

Serikali ifanye Mpango wa kuongea na watu wenye hizo nyumba ikiwezekana wapewe maeneo mengine wakajenga na maeneo yao yauzwe kwa watu wenye uwezo wakujenge nyumba za kisasa.

Frankly speaking nyumba nyingi za zamani zilizochakaa zinaaribu sana mvuto wa jiji bora wenye hizo nyumba waziuze wakajenge sehemu zingine.

Wenye nyumba chafu za zamani ziuzeni mkanunue sehemu nyingine sio lazima kukomaa na jiji huku huwez kuboresha hata nyumba viwanja vimejaaa Kibaha, goba, Mapinga, Kigamboni, bagamoyo unanunua shamba kubwa tu unapata na sehemu ya bustani sio unakaa town unashindwa hata kulima mboga.

Mfano Kama kuna mtu ana nyumba sinza kuuza hata 200M inawezekana then akaenda kununua kiwanja kigamboni au Kibaha ambavyo vinauzwa (1.8M-2.5M) kwa hela hiyo anaweza kujenga bonge la mjengo na maisha yakaenda.
Huu ni uhaba wa fikra unabomoa nyumba ety zimechakaa wakati huo huo kuna madarasa ya skul hayafai kuwa madarasa na bado yanatumika tena n ya serikal wakitaka fanya ivyo watafute mji mpya waujenge upya uwe town kusiwe na nyumba chakavu kama india (waliiacha DELHI wakaenda jenga mji mpya wakauita NEW DELHI uliopangiliwa vizur)
 
Huwa nashangaa hoja za kupendezesha mji. Unapendezesha mji ili iweje?

Yaani utese watu kwa kuwabomolea nyumba zao ili upendezeshe mji. Umpendezeshee nani na kwa sababu gani?

Mawazo ya kishamba kabisa.
Ni suala la mazingira safi ambayo yataondoa uchafu mababarani, kunakopelekea kustawisha mazalio ya mbu na vyura wenye kelele kutwa kucha.

Mazingira safi huondoa uwezekano wa kutokea magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na homa ya malaria.

Nafahamu fika watania tu ila unaelewa anachomaanisha mleta mada.

Tuache mizaha.
 
Kuwaondoa machinga mijini ni kuwaonea kwani wao hawana haki ya kuwepo mjini.Machinga achafui mazingira kama akishirikishwa.
 
Serikali ikimalizana na kuwaondoa Wamachinga waazae Campaign ya Kuondoa nyumba zote chafu na za zaman ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na maeneo yauzwe kwa Watu wenye uwezo wa kuweka nyumba za kisasa.

Hii itasaidia sana majiji mengi hapa Tanzania kuwa safi na kuwa na Muonekano mzuri.

Pembezoni mwa barabara zimejaaa nyumba nyingi ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na zinafanya majiji kuonekana hakuna mipango miji.

Serikali ifanye Mpango wa kuongea na watu wenye hizo nyumba ikiwezekana wapewe maeneo mengine wakajenga na maeneo yao yauzwe kwa watu wenye uwezo wakujenge nyumba za kisasa.

Frankly speaking nyumba nyingi za zamani zilizochakaa zinaaribu sana mvuto wa jiji bora wenye hizo nyumba waziuze wakajenge sehemu zingine.

Wenye nyumba chafu za zamani ziuzeni mkanunue sehemu nyingine sio lazima kukomaa na jiji huku huwez kuboresha hata nyumba viwanja vimejaaa Kibaha, goba, Mapinga, Kigamboni, bagamoyo unanunua shamba kubwa tu unapata na sehemu ya bustani sio unakaa town unashindwa hata kulima mboga.

Mfano Kama kuna mtu ana nyumba sinza kuuza hata 200M inawezekana then akaenda kununua kiwanja kigamboni au Kibaha ambavyo vinauzwa (1.8M-2.5M) kwa hela hiyo anaweza kujenga bonge la mjengo na maisha yakaenda.
ACHA VISASI MKUU. HIZO NYUMBA NA ARDHI NI ZA WENYEWE. KAMA BABA YAKO ALIKUWA ANAKULA BATA HAKUCHUKUA KIWANJA KIZURI USITAFUTE VISA BALI TAFUTA HELA UVINUNUE WW UJENGE HIZO NYUMBA BORA NA ZA KISASA..
 
huu ni uhaba wa fikra unabomoa nyumba ety zimechakaa wakati huo huo kuna madarasa ya skul hayafai kuwa madarasa na bado yanatumika tena n ya serikal wakitaka fanya ivyo watafute mji mpya waujenge upya uwe town kusiwe na nyumba chakavu kama india (waliiacha DELHI wakaenda jenga mji mpya wakauita NEW DELHI uliopangiliwa vizur)
Mkuu, New delhi ulijengwa na wakoloni wa kiingereza kwa ajili ya shughuli zao za kikoloni khasa usafirishaji malighafi na ukawa mji kamili wa kibiashara mwaka 1931.

Mji huo haukujengwa na wahindi wenyewe na wala halikuwa wazo lao wahindi.
 
Wandae sheria kisha utekelezaji uanzie jijini Dar na Tanga mana kuna nyumba (magofu) nyingi za hovyohovyo tena katikati ya mji.
Nasema hivi. Tafuteni hela. Watu mnaoongea hapa hata mkipewa hivyo viwanja hamtajenga kitu. Akipewa Mo au Bakhreaa tutalaani wote. Ndio umaskini ulivyo. Tupambane kuutooomeza lakini sio kwa visa hivi.
 
Kabisa wajengewe nyumba pembezoni mwa miji huko waachie viwanja vya mjini vipewe wawekezaji hilo ni Big YES
Kwani nani kasema wawekezaji hawajapewa hivyo viwanja? Ni hela yako tu mkuu ukitaka kiwanja chochote na popote Tanzania unakipata baada ya kumnunua mtu na kumhamisha fasta. Na kama serikali ikiamua kuvichukua kwa nguvu pasipo kulipa fidia itakuwa ni UGAIDI WA HALI YA JUU.
 
Serikali ikimalizana na kuwaondoa Wamachinga waazae Campaign ya Kuondoa nyumba zote chafu na za zaman ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na maeneo yauzwe kwa Watu wenye uwezo wa kuweka nyumba za kisasa.

Hii itasaidia sana majiji mengi hapa Tanzania kuwa safi na kuwa na Muonekano mzuri.

Pembezoni mwa barabara zimejaaa nyumba nyingi ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na zinafanya majiji kuonekana hakuna mipango miji.

Serikali ifanye Mpango wa kuongea na watu wenye hizo nyumba ikiwezekana wapewe maeneo mengine wakajenga na maeneo yao yauzwe kwa watu wenye uwezo wakujenge nyumba za kisasa.

Frankly speaking nyumba nyingi za zamani zilizochakaa zinaaribu sana mvuto wa jiji bora wenye hizo nyumba waziuze wakajenge sehemu zingine.

Wenye nyumba chafu za zamani ziuzeni mkanunue sehemu nyingine sio lazima kukomaa na jiji huku huwez kuboresha hata nyumba viwanja vimejaaa Kibaha, goba, Mapinga, Kigamboni, bagamoyo unanunua shamba kubwa tu unapata na sehemu ya bustani sio unakaa town unashindwa hata kulima mboga.

Mfano Kama kuna mtu ana nyumba sinza kuuza hata 200M inawezekana then akaenda kununua kiwanja kigamboni au Kibaha ambavyo vinauzwa (1.8M-2.5M) kwa hela hiyo anaweza kujenga bonge la mjengo na maisha yakaenda.
Mkuu una wazo zuri lakini kwa kuwaondoa wenye mji hilo hapana.

Serikali za mitaa ndizo zenye wajibu wa kuendeleza miji na kuifanyia kitu chaitwa urban regeneration.

Hivyo hawa wenye nyumba ambazo zilijengwa kimpangilio tangu ukoloni watoto wao watakiwa kupewa facility ya mikopo yenye riba nafuu ili kuboresha nyumba hizo.

Serikali za mitaa zapaswa kuboresha miundombinu kama barabara na taa za mabarabarani na pia kutoa huduma zingine kama uzoaji taka.

Wamachinga wanaondolewa kwasababu wao ni wavamizi.

Ila naunga mkono kuondoa nyumba ambazo haikufuata sheria za mipango miji lakini kwa kufuata sheria na taratibu ikiwamo kulipa fidia au kuwatafutia maeneo mapya ya bure na kiasi fulani cha kuanzia ujenzi.

Kama kweli kuna nia ya kuboresha mji na kuupendezesha basi yatafutwe maeneo mengine yaanzishe miji mipya kabisa yenye kila kitu.

Nchi hii ina ardhi ya kutosha.
 
Wote mnaounga hoja acheni visa. Narudia. Acheni visa vya kishirikina aisee. Wamachinga sawa.. Waondolewe hata kwa viboko. Ardhi sio yao. Walivamia maeneo

Sasa kama wameshindwa kuziboresha si bora watolewe
 
Back
Top Bottom