Labda itakua vigumu kueleweka lakini nimeonelea ni bora nikatoa ushauri kwa manispaa na halmashauri zetu kuwaondoa mama lishe, Wamachinga na vibanda vya kuuza kadi na kusajili simu vilivyoko mabarabarani. Sababu kuu ni kuwa utakuta wanauza chakula, matunda n.k kwenye vumbi na zinaponyesha mvua ndio kabisa.
Hali hii itatuletea kipindupindu (cholera), homa ya matumbo(Typhoid) n.k. sitoshe watembea kwa miguu inatubidi tutembee mabarabarani maana kwenye maeneo ya kupita watu (pedestrian pavements) wamejaa machinga na kutandaza bidhaa zao. Hili linasababisha watu hasa WANAFUNZI kugongwa na bajaji, bodaboda, daladala na hatari magari.
Tusiingize siasa kwenye suala hili. Wamachinga kama zilivyo nchi zingine nyingi wanawekewa maeneo makubwa saizi ya eneo lote la mfano Kibaha. Wanavyofanya wenzetu Afrika na nchi zingine hili eneo linakuwa makhsusi kwa ajili ya machinga. Kila aina ya bidhaa na vyakula na mpaka spea za magari unazikuta huko. Yaani unatoka kwenda huko unapata unachokitaka mpaka yanauzwa magari yaliyotumika. Miji inakuwa misafi inapendeza, wananchi wapo salama na machinga pia wanafanya biashara.
Niliwahi kuitembelea nchi ya Tunisia ikawauliza wenyeji hivi hapa Tunis hakuna machinga? Wakanijibu wapo ila tutakupeleka. Kwa kweli ilibidi nistaajabu kwani hilo eneo ni kubwa na unapata unachokitaka. Huduma zote zipo. Naomba wizara zinazohusika zitume wataalam wao nje wakaone wenzetu wanavyojipanga. HAKUNA SIASA KWENYE HILI. Maana tatizo letu Watanzania ni kulalamika tu, Tubadilike pamoja na umasikini wetu. Isitoshe inasikitisha kuwaona baadhi ya kina mama wanauza zambarau hivi najiuliza huyu anaungua juani kutwa nzima anapata nini kuendesha maisha yake?
Ni bora akaenda kulima kijijini. Kwahiyo hata watembea kwa miguu nao wana haki.
#Salaam za Jamhuri Ya Muungano waTanzania# Kaziiendelee