Mkimaliza Kuwaondoa Wamachinga muanze kampeni ya Kuondoa Nyumba za Zamani zilizopo Pembezoni Mwa barabara

Mayunga234

JF-Expert Member
Feb 17, 2017
1,374
2,000
Serikali ikimalizana na kuwaondoa Wamachinga waazae Campaign ya Kuondoa nyumba zote chafu na za zaman ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na maeneo yauzwe kwa Watu wenye uwezo wa kuweka nyumba za kisasa.

Hii itasaidia sana majiji mengi hapa Tanzania kuwa safi na kuwa na Muonekano mzuri.

Pembezoni mwa barabara zimejaaa nyumba nyingi ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na zinafanya majiji kuonekana hakuna mipango miji.

Serikali ifanye Mpango wa kuongea na watu wenye hizo nyumba ikiwezekana wapewe maeneo mengine wakajenga na maeneo yao yauzwe kwa watu wenye uwezo wakujenge nyumba za kisasa.

Frankly speaking nyumba nyingi za zamani zilizochakaa zinaaribu sana mvuto wa jiji bora wenye hizo nyumba waziuze wakajenge sehemu zingine.

Wenye nyumba chafu za zamani ziuzeni mkanunue sehemu nyingine sio lazima kukomaa na jiji huku huwez kuboresha hata nyumba viwanja vimejaaa Kibaha, goba, Mapinga, Kigamboni, bagamoyo unanunua shamba kubwa tu unapata na sehemu ya bustani sio unakaa town unashindwa hata kulima mboga.

Mfano Kama kuna mtu ana nyumba sinza kuuza hata 200M inawezekana then akaenda kununua kiwanja kigamboni au Kibaha ambavyo vinauzwa (1.8M-2.5M) kwa hela hiyo anaweza kujenga bonge la mjengo na maisha yakaenda.
 

msigara

Member
Feb 10, 2017
6
45
Nyumba kuukuu ni sehemu ya kumbukumbu kihistoria. Zitaondoka taratibu isipokuwa kwa Miradi maalum kama ile ya Prof Anna Tibaijuka na UNHabitat ya kuboresha Slams kama ilivyokuwa kwa Manzese. Aidha, baada ya Machinga kuondolewa sambamba na Sheria ya Mipango Miji ifuatie na Uboreshaji wa Maeneo yote yaliyopimwa, kuwa na ramani iliyoidhinishwa na Kamishina lakini yamendekezwa kiholela pasipo kufuata Ramani husika, kuvamia maeneo ya barabara za mitaa na viwanja vya wazi kwa huduma za umma (ibada,soko, shule, hospital au michezo).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom