Mkimaliza Kuwaondoa Wamachinga muanze kampeni ya Kuondoa Nyumba za Zamani zilizopo Pembezoni Mwa barabara

Naunga mkonyo hoja, Shaurimoyo Manzese, Tandale Buguruni Vingunguti, Ubungo maji kwa kuanzia wavunje vibanda umiza vyote nyumba za hovyo mabati yamejaa kutu tupu kama huamini shuka na ndege uone Dar ilivyo mbaya
Ukiwa unatua Dar na ndege hususana kuanzia saa moja jioni unaona mji ulivyokuwa ni kituko kupitia taa ....
Vile vile tua Jo'burg usiku au Nairobi utaona tofauti ya Mbingu na Ardhi kati ya hiyo miji na Jiji la aDar es salaam
 
Acha akil za kimaskin
Ukute hapo hujawahi kumiliki kitu kinachoitwa "chako'
Mzee wakushirikisha ndugu kwenye kila gumu.
kwa sauti PAMBANA UBORESHE KWAKO UKIMALIZA MSAIDIE JIRANI KUBORESHA MAZINGIRA!
mji utakuwa safi kabisa!
 
Jamii forum kama hauna nyumba ya kisasa na ndinga kali ni wewe tu umebaki...wengine wote tunazo...hahahaaaa
 
Serikali ikimalizana na kuwaondoa Wamachinga waazae Campaign ya Kuondoa nyumba zote chafu na za zaman ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na maeneo yauzwe kwa Watu wenye uwezo wa kuweka nyumba za kisasa.

Hii itasaidia sana majiji mengi hapa Tanzania kuwa safi na kuwa na Muonekano mzuri.

Pembezoni mwa barabara zimejaaa nyumba nyingi ambazo watu wake wameshindwa kuziboresha na zinafanya majiji kuonekana hakuna mipango miji.

Serikali ifanye Mpango wa kuongea na watu wenye hizo nyumba ikiwezekana wapewe maeneo mengine wakajenga na maeneo yao yauzwe kwa watu wenye uwezo wakujenge nyumba za kisasa.

Frankly speaking nyumba nyingi za zamani zilizochakaa zinaaribu sana mvuto wa jiji bora wenye hizo nyumba waziuze wakajenge sehemu zingine.

Wenye nyumba chafu za zamani ziuzeni mkanunue sehemu nyingine sio lazima kukomaa na jiji huku huwez kuboresha hata nyumba viwanja vimejaaa Kibaha, goba, Mapinga, Kigamboni, bagamoyo unanunua shamba kubwa tu unapata na sehemu ya bustani sio unakaa town unashindwa hata kulima mboga.

Mfano Kama kuna mtu ana nyumba sinza kuuza hata 200M inawezekana then akaenda kununua kiwanja kigamboni au Kibaha ambavyo vinauzwa (1.8M-2.5M) kwa hela hiyo anaweza kujenga bonge la mjengo na maisha yakaenda.
Wakimaliza hapo, waje warudishe mali zote za wananchi zilizoporwa na Chama cha Mapinduzi
 
Ukute hapo hujawahi kumiliki kitu kinachoitwa "chako'
Mzee wakushirikisha ndugu kwenye kila gumu.
kwa sauti PAMBANA UBORESHE KWAKO UKIMALIZA MSAIDIE JIRANI KUBORESHA MAZINGIRA!
mji utakuwa safi kabisa!

Usikute hadi wewe nakumiliki
 
Ukiwa unatua Dar na ndege hususana kuanzia saa moja jioni unaona mji ulivyokuwa ni kituko kupitia taa ....
Vile vile tua Jo'burg usiku au Nairobi utaona tofauti ya Mbingu na Ardhi kati ya hiyo miji na Jiji la aDar es salaam

 
Back
Top Bottom