Mkienda Zaire Muwe Makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkienda Zaire Muwe Makini

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Duduwasha, Jan 7, 2012.

 1. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Kuna Jamaa alienda Congo (Zaire) Katika Kutembezwa na Mwenyeji wake katika Jiji la Kinshansa wakakatiza katika mitaa karibu na soko kulikuwa na Njia ndogo na kwa mbele ya ile Njia kulikuwa na Mtu anaimba 27, 27, 27, 27, 27, 27, huku anazunguka Shimo lililokuwa mbele yake pia akilichungulia kwa ndani .. Jamaa akavutiwa Sana na ile hali ya Jamaa alivyokuwa akicheza huku analizunguka na kuchungulia lile Shimo, Mwenyeji wake akamuambia achana nae yule wakampuuza...

  Baada ya mizunguko zaidi mjini pale wakawa wanarejea kwenye maskani yao walipofikia huku wakipita Njia ile ile karibu na Soko... jamaa alikuwa akimuwazia yule Mtu alivyokuwa akicheza kwani alivutiwa nae, ndipo walipofika maeneo ya karibu pale muimbaji alishabadili wimbo tena akiimba 28, 28, 28, 28 ,28 bila kuachia Pumzi, Jamaa akamsogelea Yule muimbaji achungulie ndani kuna nini Ghafla yule jamaa akaacha kuimba na akamsokomeza Mjamaa Ndani ya Shimo then akaanza kuimba tena 29, 29, 29, 29, 29, huku akilichungulia lile Shimo... Mwenyeji alibaki kaduwaa
   
 2. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Imetulia mkuu.
   
 3. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  [FONT=times new roman,helvetica]
  Padri Dents Aliingia Ghafla Jolly Club Hafla, Kisha akaanza kumuuliza Kijana wa Kwanza aliyekutana nae,

  Padri: Utanaka kwenda Mbinguni''?

  Kijana Akajibu'' Ndio Nataka Padri''

  Padri Akajmuambia Nenda kasimame pale karibu na ukuta''

  Padri akamuuliza Kijana wa Pili''

  Padri : Unataka kwenda Mbinguni''?

  Kijana akajibu Ndio Padri mie Vile vile Nataka Kwenda Mbinguni''

  Padri akamuambia Simama Pale karibu na Ukuta''

  Padri akamfuata Jamaa wa Tatu na Kumuuliza

  Unataka kwenda Mbinguni''?

  Kijana Akamjibu Hapana'' Padri''

  Padri akasema Siamini usemayo.Yaani unataka kuniambia hutaki kwenda Mbinguni Siku Ukifa?''

  Jamaa akajibu aah Kumbe Nikifa ! Ndio Nataka ila nilidhania unakusanya Kundi la Watu Kwenda Mbinguni Sasa hivi''

  [/FONT]
   
Loading...