Mkichat kila wakati "Niambie"

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,180
Reaction score
24,798
Hivi hili neno "niambie" mbona linapendwa sana kutumika hasa na wadada kwenye kuchati, tena kifupi sana...!!?
Unakuta bint anakutext au unamtext sms ya pili yeye kujibu ni neno "niambie"
Sometime neno hilo me nahisi huwa linawakera wengi tu ila wanashindwa kuwafungukia hao wanaowajibu hivyo...
Mbaya zaidi ni kila wakati hata iwe umepiga simu utasikia " niambie"...
Kwangu me ukiwa unalirudia rudia hili neno wala siendelei kuchat!
Naona hata kama kuna mwanaume anapenda kutumia hilo neno mara kwa mara abadilike!
Mapovu ruksa...
Matusi marufuku, mods wapo kazini leo wamekula pilau makinikia!
 
Mi mwenyewe nakapenda hako ka neno sema sio kazuri
 
Mapovu ruksa...
Matusi marufuku, mods wapo kazini leo wamekula pilau makinikia!

Nimecheka hiki kipande aiseeeew duh!!!
Mie napenda kulitumia huko neno ikiwa nmempigia au kumtext mtu,nikaekeza mambo yangu nikimaliza then nitamuanbia niambie in case ana lolote akinambia hamna jipya basi tunamaliza mazungumzo.
 
Mi sipend mtu aniambie usiwaze,usikonde !!yaani nayachukia hayo maneno ..unamuuloza kitu anakwmbia usiwaze,jamani vijana tuache hya maneno.🙂.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…