Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Sina hakika saana kama huyo ni mke wako wa ndoa na si rahisi kumshitaki mahakaman na kesi ikawa simple chakufanya mweleze mkeo kwanin ulifanya hvo na jitahidi kumshirikisha mkeo kwa kila kitu
 
Mwili mmoja ni huko Ughaibuni sio Bongo! Hapa tu mnaonekana jinsi mitazamo yenu ilivyo selfish!

Uselfish mnauanza nyie wanaume,wewe tayari uko kwenye ndoa,unafanyaje baadhi ya miamala bila kumshirikisha mkeo? Na hiyo ndio sababu iliyomfanya akabe mawasiliano yako baada ya kuhisi hali sio shwari. Mkeo naye ana nafasi katika maamuzi yako,vinginevyo umetawaliwa na mfumo dume.
 
mi cdhan kama mpes no taarif ya cr kwa wanandoa.Mke umeish naye miaka 8 bado unaish kwa kijiiba kwamba humwamin au?
 
Kama kweli hana utalaanika huo wa mawasiliano basi jua ana reliable Na credible source kutoka kwa provider wa mtandao wa simu unayotumia! Sasa anzia hapo kuitafuta hiyo source! Jifunze umafia na wewe usiregee!
 
Kama kweli hana utalaanika huo wa mawasiliano basi jua ana reliable Na credible source kutoka kwa provider wa mtandao wa simu unayotumia! Sasa anzia hapo kuitafuta hiyo source! Jifunze umafia na wewe usiregee!
Sorry isomeke utalaam
 
Sina hakika saana kama huyo ni mke wako wa ndoa na si rahisi kumshitaki mahakaman na kesi ikawa simple chakufanya mweleze mkeo kwanin ulifanya hvo na jitahidi kumshirikisha mkeo kwa kila kitu
Mimi ndio ninayemtuhumu kwa kuingilia mawasiliano yangu bila idhini yangu, yeye yupo kwenye upande wa kuomba msamaha kuwa nisilifikishe hili suala kwenye vyombo vya sheria, kati yangu na yeye ni nani anatakiwa amueleze mwenzie sababu ya kufanya kilichofanyika?!!
 
Kwa hiyo maana ya ndoa ni kufanyiana ujasusi? Nijuavyo mimi ndoa ni UPENDO.
 
CHAPA MAKOFI, MWENYEWE ATAKUELEZA NJIA ALIYOTUMIA KUPATA HIZO TAARIFA ZAKO NA PIA MTU ALIYEMFANYIA HIYO KAZI. kUWA MWANAUME ACHA UBWEGE.
 
Je,una wazazi? Na mkeo ana wazazi? Kama kwako hilo limekiwa tatizo ni kwa nini usiwafikishie wazazi wenu ili m-malize tofauti zenu? Unachokitafuta wewe ni kusuluhisha au ni kuachana? Vinginevyo tuambie kuwa umemchoka huyo dada. Kama kweli unatafuta ushauri kwa ajili ya kutatua hilo suala basi washirikisheni wazazi wenu,au wajomba na mashangazi,si mahakamani. Watu mmeoana kwa ndoa,mnalala watupu kitandani,halafu mwisho wa siku mna simamishana mahakamani kama maadui? Haileti picha nzuri bhanaa.


 
Hahahaaa. ... mkisikia wake kuchepuka vinawauma kwelikweli,
Ila wanaume kuchepuka ni urijali.
Hahahaaa. .... ukigawa game nje lazima na yeye agawe game nje tuuu sabab hakuna namna nyingine
Hujatulia!
 
Kwa hiyo maana ya ndoa ni kufanyiana ujasusi? Nijuavyo mimi ndoa ni UPENDO.

Ndoa sio rahisi kama unavyotafsiri wewe, Upendo? Yaani kila siku upendo tu!! Ingekuwa hivyo watu wasingetalikiana,ndoa ni pamoja na hayo unayoyapitia sasa,ndio maana kila anayeshauri kuhusu ndoa haachi kutaja uvumilivu, Ninahisi suala la wewe kuishi mikoa tofauti na mkeo ndilo linaloigharimu ndoa yako. Ukame hapa lazima unahusika.
 
Hii comment imekomaa!
 
Hakuna povu bali ukweli tu.

Watu wasio waaminifu kwa wenza wao hupenda sana kulialia wakibambwa.

Kama jamaa hana baya afanyalo basi hana sababu ya kupatwa na kiwewe.
Uaminifu kwenye ndoa Afrika ni kitendawili usifikri wote tunabeba boksi.
 
Mwanamke haruhusiwi kuchepuka, ulisikia wapi kwenye historia ya Dunia hii mwanamke mmoja akaolewa na zaidi ya mwanaume mmoja? Ila sisi Masheikh mpaka sasa tunaoa hadi 4 teh teh teh!
Na yy huko nje kapata sheikh anayeruhusiwa kuoa wake wa 4. Hebu kaa na mkeo muyamalize. Jishushe uache michepuko. Ndoa sio mashindano. Fikiria na hao watoto
 
Hata kama umeoa naamini kuna mambo ambayo ni private na mojawapo ya mambo hayo ni simu za mikononi.Jaribu kubadili simu na chip pia
 
Hili nalo neno!! Atueleze vizuri
 
Naona makosa kadhaa kwa wanandoa hawa;
1. Ukimsaliti mwenzako kwa kutoka nje ya ndoa (nae akafahamu kuwa umemsaliti), usitegemee quick fix coz you've torn your partner's heart. Hilo linasababisha yeye kukosa imani na wewe, hivyo kupelekea kuangalia mapito yako (ikiwa ni pamoja na mawasiliano ya simu).
Huenda mke hakuwa na nia ya kufuatilia miamala yako, lakini you gave her a reason not to trust you. You need to fix that, na inachukua mda. Ukimsaliti mtu leo nae akasema amekusamehe, usifikiri kila kitu kitaishia hapo, atakumbuka...atakulaani...atafanya moyo mgumu..nk.
2. Kitendo cha wanandoa kuishi mbali either coz of education or work, kinaathiri na kudhoofisha sana ndoa coz hata mwenyezi Mungu alipowaumba Adam & Eve aliwaambia waambatane, kuwa pamoja au kuishi pamoja kunapunuza mengi sana,.. nadhani unaelewa hilo, hivyo yeye kufuatilia mawasiliano yako, kunaweza kuletwa na umbali mlio nao...she's protecting what belongs to her, usimlaumu sana.
3. Mke nae ana makosa yake, hakupaswa kufanya alichofanya hata kama ni wivu au kukubana ili usitume pesa ovyo kwa watu baki. Lakini unaposema (privacy yako), ukiwa na ndoa neno ''privacy'' halina nafasi kabisa. Unatakiwa kumshirikisha mke kwa kila unalotaka kufanya.

Mwisho, huna sababu za kumshtaki mwandani wako, kaa nae chini myaweke vizuri...ukimshitaki ujuwe unajishitaki...unless uniambie umeichoka ndoa yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…