Mke wangu ni HIV Positive

Mke wangu ni HIV Positive

Ni bora mwende mkapime tena hususani mara tatu yaani kila baada ya ya miezi mitatu..pengine nawe waweza kuwa umeathilika..

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Pole sana Supervisor. Naona wengi wanakushauri umwache lakini nina swali moja tu; nalo ni ingekuwaje kama ingekuwa kinyume chake, yaani wewe unao yeye hana? Ungefurahia kuachwa?
Halafu nina maswali kadhaa na ushauri. Mlioana Septemba 2012, mimba ina umri gani hadi sasa, na kwa matarajio mkeo atajifungua lini?
Kuna jambo moja la kuzingatia, nalo ni kwamba si kila familia yenye mwenza muathirika ni lazima wote wawe wameambukizwa. Kuna baadhi ya watu hawaambukizwi licha ya kushiriki mara kadhaa tendo la ndoa bila ya kinga! Hawa wanajulikana kama 'Discordant couples' Unaweza kuwa mmojawapo. Unatakiwa upime tena baada ya miezi mitatu bila ya kujamiiana ili uweze kuwa na uhakika kwamba hujaathirika.
Binafsi nakushauri:
I. Usimwache kabisa mkeo madamu ulishafanya kosa la kuoana bila kupima.
ii. Kwa sasa juhudi zielekezwe kwa mtoto mtarajiwa. Kwa njia zilizoko siku hizi kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuzaliwa bila virusi.
iii. Mshauri mkeo apime CD4 ili kuelewa kiwango alichoathirika na aanze ARTs (Anti Retrovirals) mapema. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa yeye kukuambukiza maana sasa ni wazi, ni vigumu kwa wanaotumia ARTs kuwaambukiza wenza wao.
iv. Ni suala la muda tu kwani inavyoelekea siku zijazo hakutakuwa na hatari kubwa kama ilivyo sasa kwa kujamiiana na wenza walioathirika.
Mnaweza tumia vizuizi kama condom na kama atakuwa katika ARVs uwezekano wa wewe kuambukizwa utakuwa mfinyu kabisa.
 
Kwani mke wako huyu mlikaa kama wachumba kwa muda gani? Je hamkuwahi kufanya mapenzi kabla ya kuoana?

Kwa uelewa wangu virusi vya ukimwi uchukua muda kujitokeza, si rahisi kujenga antibodies ya virusi vya ukimwi within two months i.e huwezi kuwa na uhakika kam wewe huko salama mpka muda upite. Vile kuna binadamu wengine wana kinga ya asili dhidi ya ukimwi, mwenzako anaweza kuwa na ukimwi lakini wewe ukabaki salama miaka yote hao wapo lakini ni wachache SANA.

Kweli, kwenye ukoo wa baba wanaishi maisha marefu hadi 100, UKIMWI ulipoingia wamezika wake na waume kibao lakini ukoo huo wanakufa kwa ajal mfano, radi, kuanguka, nyoka, pikipiki, gari, mabasi lakini si magonjwa hamwezi amini.
 
Kabla ya ndoa mnapima mara moja lakini kuna kipindi cha mpito miezi mitatu
Hiyo hali isikupe tabu maana sio ninyi wa kwanza wapo wengine pia imewatokea ila mtumie zana wakati wa kushiriki na pia mkitaka kuongeza mtoto sababu ni haki yenu kabisa unamuaandaa mama vya kutosha ili kuwe na maji yakutosha ili msipate michubuko inayosabishwa na friction basi hutumii kinga kwa siku hiyo najua mtatumia kalenda ya mama ili mtaimu yai litakapokuwa limetoka
mlimde mkeo asipate maambukizi mapya maana kirusi kinabadilika badilika
pia atumie dawa za kumzuia mtoto asipate maambukizi kuanzia wiki ya kumi na nne mtoto atazaliwa salama huna haja ya kumwacha inawezekana kabisa kuishi na mtu aliyeathirika ukimwi wa siku hizi si kama zamani ambapo watu walikuwa wanakonda na kuharisha weee! Hamna labda asitumie dawa
 
Pole sana Supervisor. Naona wengi wanakushauri umwache lakini nina swali moja tu; nalo ni ingekuwaje kama ingekuwa kinyume chake, yaani wewe unao yeye hana? Ungefurahia kuachwa?
Halafu nina maswali kadhaa na ushauri. Mlioana Septemba 2012, mimba ina umri gani hadi sasa, na kwa matarajio mkeo atajifungua lini?
Kuna jambo moja la kuzingatia, nalo ni kwamba si kila familia yenye mwenza muathirika ni lazima wote wawe wameambukizwa. Kuna baadhi ya watu hawaambukizwi licha ya kushiriki mara kadhaa tendo la ndoa bila ya kinga! Hawa wanajulikana kama 'Discordant couples' Unaweza kuwa mmojawapo. Unatakiwa upime tena baada ya miezi mitatu bila ya kujamiiana ili uweze kuwa na uhakika kwamba hujaathirika.
Binafsi nakushauri:
I. Usimwache kabisa mkeo madamu ulishafanya kosa la kuoana bila kupima.
ii. Kwa sasa juhudi zielekezwe kwa mtoto mtarajiwa. Kwa njia zilizoko siku hizi kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuzaliwa bila virusi.
iii. Mshauri mkeo apime CD4 ili kuelewa kiwango alichoathirika na aanze ARTs (Anti Retrovirals) mapema. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa yeye kukuambukiza maana sasa ni wazi, ni vigumu kwa wanaotumia ARTs kuwaambukiza wenza wao.
iv. Ni suala la muda tu kwani inavyoelekea siku zijazo hakutakuwa na hatari kubwa kama ilivyo sasa kwa kujamiiana na wenza walioathirika.
Mnaweza tumia vizuizi kama condom na kama atakuwa katika ARVs uwezekano wa wewe kuambukizwa utakuwa mfinyu kabisa.

Ndg yangu Luhala nashukru kwa ushauri wako na inaonesha una uelewa mkubwa na issue hii. Mke ana ujauzito wa miezi minne na tayari amekwisha anza kupata intensive care ya ma nurse ili asiweze kudhuru mtoto
 
Your ma hero Natalia! Keep it up

Hebu ni in box nitakupa no au facebook ya mtu akusaidie .Ana historia Kama ya mkeo ila huyo dada alikuja kuzalia Huku baada ya kuona anao .Ukizalia Huku watahakikisha mtoto yupo safe na ataanza matibabu kwa njia hiyo .
 
Pole sana lakini hongera kwa ujasiri wako!Ningekuuliza maswali kadhaa,ila nahisi hayana maana kwa sasa!Hapa tusubiri wadau wengine watasemaje,ila kwa mimi cha kukushauri ni ni kupigia mstari uamuzi wako wa kuendelea kuishi na mkeo wa ndoa.Maadamu mmeshajua tatizo,ni kwenu sasa kukaa chini kumlinda mtoto aliyeko tumboni,na wewe ambaye hujaambukizwa.Amini inawezekana kuishi na mwenza aliyeathirika,bila athari,ilimradi mfuate nasaha za washauri.Na mkiishi kwa furaha,haya mkeo ataishi maisha marefu....

''NONI'' unatosha kuwa MSHAURI NASAHA,hongera sana,bro fuata ushauri huo wake,usimuache mkeo!
 
Hebu ni in box nitakupa no au facebook ya mtu akusaidie .Ana historia Kama ya mkeo ila huyo dada alikuja kuzalia Huku baada ya kuona anao .Ukizalia Huku watahakikisha mtoto yupo safe na ataanza matibabu kwa
So unataka mshawishi aje ulaya..huku kwenyew wanazaa fresh na hamna maambukizi..bongo tumeendelea
 
Pole sana
huo nao ni mtihani wako katika maisha yako
kama ukiufanya vizuri utapata "A" na ukifanya kosa moja tu utapata "F"
 
Komaa nae NGOMA kwa kipande hii SIO MAJANGA, MTU WANGU,Mkaushie ila kula SEBENE KIAINA,mwendo wa Chameleon,sio kujifanya fundi,kisha never kula NDIZI NYAMA,i.e kitu live
 
Kweli, kwenye ukoo wa baba wanaishi maisha marefu hadi 100, UKIMWI ulipoingia wamezika wake na waume kibao lakini ukoo huo wanakufa kwa ajal mfano, radi, kuanguka, nyoka, pikipiki, gari, mabasi lakini si magonjwa hamwezi amini.

Emekwisha kuwa proved kisayansi kwamba kuishi muda mrefu kuna tegemea na ukoo uliyo zaliwa!! Kitu kingine umenikumbusha RADI za Bukoba - nimebahatika kutembelea nchi nyingi lakini kwa upande wa RADI nafikili Bukoba haina mfanowe, hapa kwetu usema Mbeya na Sumbawanga sina uhakika kama zinazidi Bukoba!!
 
sasa mbona maamuzi yako ni mazuri tu,ushauri wa nn tena?sana sana ungeomba elimu ya kuishi na mwenye hiv
 
Pole sana,Inshallah Mungu akupe moyo mstahmilivu wakuhimili...
 
U make me cry( ma eyes are full of tears) real umenitoa chozi Superman. Hapana mi siko DSM niko Mkoani lkn kwel tulienda Goverment hospital kupima na cjui nawezaje kuendelea kupata ushauri kutoka kwako. Nauhitaji kwel

mi pia nimelia,pole sn mkuu.
 
Pole sana Supervisor. Naona wengi wanakushauri umwache lakini nina swali moja tu; nalo ni ingekuwaje kama ingekuwa kinyume chake, yaani wewe unao yeye hana? Ungefurahia kuachwa?
Halafu nina maswali kadhaa na ushauri. Mlioana Septemba 2012, mimba ina umri gani hadi sasa, na kwa matarajio mkeo atajifungua lini?
Kuna jambo moja la kuzingatia, nalo ni kwamba si kila familia yenye mwenza muathirika ni lazima wote wawe wameambukizwa. Kuna baadhi ya watu hawaambukizwi licha ya kushiriki mara kadhaa tendo la ndoa bila ya kinga! Hawa wanajulikana kama 'Discordant couples' Unaweza kuwa mmojawapo. Unatakiwa upime tena baada ya miezi mitatu bila ya kujamiiana ili uweze kuwa na uhakika kwamba hujaathirika.
Binafsi nakushauri:
I. Usimwache kabisa mkeo madamu ulishafanya kosa la kuoana bila kupima.
ii. Kwa sasa juhudi zielekezwe kwa mtoto mtarajiwa. Kwa njia zilizoko siku hizi kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuzaliwa bila virusi.
iii. Mshauri mkeo apime CD4 ili kuelewa kiwango alichoathirika na aanze ARTs (Anti Retrovirals) mapema. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa yeye kukuambukiza maana sasa ni wazi, ni vigumu kwa wanaotumia ARTs kuwaambukiza wenza wao.
iv. Ni suala la muda tu kwani inavyoelekea siku zijazo hakutakuwa na hatari kubwa kama ilivyo sasa kwa kujamiiana na wenza walioathirika.
Mnaweza tumia vizuizi kama condom na kama atakuwa katika ARVs uwezekano wa wewe kuambukizwa utakuwa mfinyu kabisa.

Wataalam au wewe mkuu luhala hebu tufafanulie zaidi kuhusu kuwa wanaotumia ARV hawawezi kuambukiza tena VVU kwa lover partners wao. Wataalam wa masuala ya VVU, ARVs na AIDS please tunaomba msaada wa kina hapa. Kwa upande wangu ninaweza kusema ni jambo la kwanza kwangu kusikia kuhusu VVU na ARV na maambukizi. Tuko na wengine mlipo please, help.
 
Supervisor, inaeleweka kabisa jinsi jambo hili limekuweka katika mazingira magumu. Nakubaliana kabisa na Luhala, usimwache mkeo. Hilo ondoa katika option zako. Hutakaa upate amani kwa kumwacha! Nafikiri mliapa mkimaanisha katika shida na raha, ugonjwa na hali ya kuwa na afya... Sasa ni wakati wa kuyatimiza hayo. Muhimu ni kutafuta njia sahihi za kuishi na hii hali. Kuwa wazi kuelezana woga na wasiwasi mlio nao na pia kuongozana na kulindana. Wapo wataalamu kama hao wanaomsaidia mwenzio sasa, ni wewe kuwa nae jirani kutalinda mwanao na kumtunza mkeo mpenzi.
Hayo maswali unaulizwa ya kwa nini hukupima kabla hayatabadili wala kusaidia lolote sasa, na wala usilifikirie hili swali only wakati utakapokuwa unashauri wengine.

Hili si jepesi ila yote yatawezekana katika yeye atutiae nguvu.
 
Mwacheni Mungu aitwe Mungu simamia ndoa yako kiapo chenu cha kanisani hakika ndio msingi wa maisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom