Mke wangu ni HIV Positive

Mke wangu ni HIV Positive

Supervisor; Upo DSM?

Kuna vipimo vya namna 2 au 3 vya HIV. Nadhani Capilary na Determine. The second is more accurate and effective. Kama upo DSM nashauru kwanza uende Hospitali zinazoaminika. Ukipenda tunaweza kuwasiliana kwa hilo nikakusaidia.

Juu ya ushauri unaohitaji, kuna mambo mengi ya kimsingi ya kuzingatia:

1. Ipime nafsi yako na kuwa mwaminifu kwako mwenyewe ni nini unahitaji. You are the boss of your life and in control. Unajua furaha yako na amani yako inahitaji nini.

2. Angalia Mtazamo wako wa Kiroho unakuongoza vipi katika hili.

3. Je akili yako inakuambiaje? Unajitambua? Mke wako ana nafasi gani katika malengo yako na maisha yako kwa ujumla? Jibu unalo wewe.

4. Lakini pia unayo changamoto juu ya afya yako ya mwili. Ni namna gani utaishi na mkeo bila kuathiri furaha yenu na afya zenu.

5. Kuna suala zima la mtoto atakayezaliwa. Unalichukulia vipi? Utapenda mtoto apate mapenzi ya wazazi wote? Je Mke wako anakupenda kweli? Na kama ndivyo ni nini kilisababisha akawa HIV Positive na wewe negative. Je wewe ni mwaminifu katika ndoa yako?

6. Juu ya kiapato na mali: Je mkeo anachangia au amechangia kiasi gani katika mafanikio ya familia. Je unajua kuwa ana haki ya kugawana mali nawe kama mkiachana no matter what? Je ana msaada kiasi gani katika kufanikisha malengo yako ya kupata fedha na mali?

7. Vipi kuhusu maendeleo yako ya kazini na ya kwako wewe binafsi? Anao msaada wowote?

8. Unao ndugu; jamaa na marafiki; wapo wanajamii na wanajuiya unaoishi nao na pia majirani. Ukiweka katika mizani unalionaje hili?

9. Na vipi kuhusu suala zima na burudani na relaxation k. je anayonafasi gani?

10. Mwishoni, ni nini malengo yako makuu katika maisha? Ni nini unkihitaji? Je unajitambua? Unatambua maana halisi ya maisha?

Huitaji kutujibu maswali haya, lakini yatakusaidia wewe katika kufikia maaumzi yako.

Good luck na tunakuombea. Ukihitaji ushauri wangu zaidi au kuniona kwa jambo lolote au kusaidiana kihali na mali, tafadhali ni PM.

U make me cry( ma eyes are full of tears) real umenitoa chozi Superman. Hapana mi siko DSM niko Mkoani lkn kwel tulienda Goverment hospital kupima na cjui nawezaje kuendelea kupata ushauri kutoka kwako. Nauhitaji kwel
 
Last edited by a moderator:
Mtihani unapokufika ndugu yangu,mshukuru Mungu na maisha yaendelee.As you have said there no option for death.Songa mbele mkuu kwa amani na furaha tele ukidumu sana katika maombi na kumtumainia Mungu.Mpende sana mkeo.
 
Habari zenu wana JF.

Poleni na mihangaiko ya wiki nzima na leo hatimaye mmerejea kulijenga taifa. Jamani nimejitokeza leo kuwaeleza true story ya maisha yangu na kama kuna ushauri basi nitaupokea. Mimi nilioa kwa ndoa takatifu mwez Sept 2012. Ilipofika Nov 2012 Mke wangu alipata ujauzito na kila m2 kati yetu akawa na furaha.

Sasa ilipofikia muda wa kwenda clinic kama ilivyo ada mnatakiwa kuwa wote ili kuweza kupata nasaha na hatimaye kupima maambukizo ya HIV. Baada ya yote tukapima na yeye Mke wangu akakutwa anaishi na virus va UKIMWI na mimi niko salama kabisa. Kwel alilia sana na Nurse akapata shida sana ya kumbembeleza hatimaye akatulia na tukatoka akwa na uso wa tabasamu bandia.

Tulipofika nyumban kilio kilianza upya na mimi nikionekana usoni sina hata lepe la hofu wakati moyoni nilikuwa naumia sana. Baadae ucku akaniomba kuwa kwa sababu Kanisani tulifundishwa kuwa ndoa yaweza vunjwa kama mmoja wapo akionekana ni malaya. Ki ukwel mimi nilimkatalia nikamwambia Mi ni wake mpaka kifo kitakapo tutenganisha, wala hakuamini macho yake.

Kwa sasa anaonekana yuko at least normal ki akili na leo ameenda kazini. Yeye binafsi ni muumini mzuri na anapenda kwel kuimba na kumsifu Mungu. Naomba ushauri wenu tafadhali.

Kupima MARA MOJA HIV siyo conclusive. Ni lazima upime zaidi ya mara tatu kwa vipindi tofatuti. Hii ya mara moja haiuambii cho chote.
 
Mtihani unapokufika ndugu yangu,mshukuru Mungu na maisha yaendelee.As you have said there no option for death.Songa mbele mkuu kwa amani na furaha tele ukidumu sana katika maombi na kumtumainia Mungu.Mpende sana mkeo.

Thanks twende kazi
 
kumbuka kiapo kwa maradhi kwa ugonjwa! kaa nae mtunze na mtoto wenu
ila tendo la ndoa inabidi uwe padri maaka ukienda nje ni uzinzi huo
 
pole kwa masaibu hayo makubwa
Mungu ndio amekulinda hadi leo
cha msingi mpende mkeo,mtunze vema na afuate shauri zote za kitabibu ili ajifunge mtoto asie na maambukizi
tumia kinga sasa kama condom na romance hizo acha
mpokee mkeo,usimnyanyapae au kusema kwa watu.
kama mna family doctor mtafute kwa ushauri zaidi..
Hilo nalo neno!
 
I wish kama ningekuwa karib na ww kwa ushauri zaid. U know what? ilitaka hata asitumie dawa ya kinga ili afe yeye na mtoto maana haoni faida ya kuishi na anajuta kuwa amenipotezea malengo lkn nikamwambia malengo yangu yako Mbinguni na sio Duniani nikamwambia kufa sio option either unaumwa au mzima

Oooh no...sI hivyo..try kumpa moyo halafu kitu kimoja ningekushauri...apatiwe counselling zile za wanaoishi na virusi vya ukimwi zitampa nguvu ya ajabu..esp hospital za serikalu huwa kuna counselling nzuri...wala asiwe na pressure....huyo nnae mzungumzia their kid is 11 now....very healthy..mpe moyo mpe update info kuhusu status yake n atazoea..ukizingatia nae alijigundua alivyokwenda clinic ya ujauzito...same story
 
mkuu supervisor pole sanana nakuombea uweze kuvuka haya majaribu yaliyokukuta salama.
Ushauri wangu usimuache mkeo na naomba umfanye awe na furaha kwa kuwa ulishaapa kanisani utaishi naye kwa shida na raha.
Kuhusu suala la yeye kuwa HIV+ na wewe kuwa HIV- usishangae kwa kuwa HIV hauenezwi kwa kujamiiana tu zipo njia nyingine pia, naomba utambue kuwa ili mtu apate virusi vya ukimwi ni lazima awe na receptors wa kupokelea vidudu hivyo. Kuna uwezekano mkubwa ww huna receptors wa HIV ndio maana mkeo anao ww huna, haya ni maumbile tu ila naomba usimnyanyapae kabisa kwa kuwa Mungu atakuwa na kusudio lake hapo.
 
The best way ilikua ni kupima kabla ya ndoa sasa huku mlikofikia sijui itakuaje bt kama wewe mwenyewe uko comfortable na hali yake mwaweza endelea tu ila wewe usiache kujikinga.
 
Bro pole sana,,, amini Mungu yupo na anakupenda sana,,, hakikisha unamtunza mkeo kwa nguvu , mali na akili zako zote...
 
Supervisor; Upo DSM?

Kuna vipimo vya namna 2 au 3 vya HIV. Nadhani Capilary na Determine. The second is more accurate and effective. Kama upo DSM nashauru kwanza uende Hospitali zinazoaminika. Ukipenda tunaweza kuwasiliana kwa hilo nikakusaidia.

Juu ya ushauri unaohitaji, kuna mambo mengi ya kimsingi ya kuzingatia:

1. Ipime nafsi yako na kuwa mwaminifu kwako mwenyewe ni nini unahitaji. You are the boss of your life and in control. Unajua furaha yako na amani yako inahitaji nini.

2. Angalia Mtazamo wako wa Kiroho unakuongoza vipi katika hili.

3. Je akili yako inakuambiaje? Unajitambua? Mke wako ana nafasi gani katika malengo yako na maisha yako kwa ujumla? Jibu unalo wewe.

4. Lakini pia unayo changamoto juu ya afya yako ya mwili. Ni namna gani utaishi na mkeo bila kuathiri furaha yenu na afya zenu.

5. Kuna suala zima la mtoto atakayezaliwa. Unalichukulia vipi? Utapenda mtoto apate mapenzi ya wazazi wote? Je Mke wako anakupenda kweli? Na kama ndivyo ni nini kilisababisha akawa HIV Positive na wewe negative. Je wewe ni mwaminifu katika ndoa yako?

6. Juu ya kiapato na mali: Je mkeo anachangia au amechangia kiasi gani katika mafanikio ya familia. Je unajua kuwa ana haki ya kugawana mali nawe kama mkiachana no matter what? Je ana msaada kiasi gani katika kufanikisha malengo yako ya kupata fedha na mali?

7. Vipi kuhusu maendeleo yako ya kazini na ya kwako wewe binafsi? Anao msaada wowote?

8. Unao ndugu; jamaa na marafiki; wapo wanajamii na wanajuiya unaoishi nao na pia majirani. Ukiweka katika mizani unalionaje hili?

9. Na vipi kuhusu suala zima na burudani na relaxation k. je anayonafasi gani?

10. Mwishoni, ni nini malengo yako makuu katika maisha? Ni nini unkihitaji? Je unajitambua? Unatambua maana halisi ya maisha?

Huitaji kutujibu maswali haya, lakini yatakusaidia wewe katika kufikia maaumzi yako.

Good luck na tunakuombea. Ukihitaji ushauri wangu zaidi au kuniona kwa jambo lolote au kusaidiana kihali na mali, tafadhali ni PM.

Kukumbushia Final conclusion inatolewa na kipimo cha UNIGOLD..baada ya determine. ...
 
Last edited by a moderator:
mkuu supervisor pole sanana nakuombea uweze kuvuka haya majaribu yaliyokukuta salama.
Ushauri wangu usimuache mkeo na naomba umfanye awe na furaha kwa kuwa ulishaapa kanisani utaishi naye kwa shida na raha.
Kuhusu suala la yeye kuwa HIV+ na wewe kuwa HIV- usishangae kwa kuwa HIV hauenezwi kwa kujamiiana tu zipo njia nyingine pia, naomba utambue kuwa ili mtu apate virusi vya ukimwi ni lazima awe na receptors wa kupokelea vidudu hivyo. Kuna uwezekano mkubwa ww huna receptors wa HIV ndio maana mkeo anao ww huna, haya ni maumbile tu ila naomba usimnyanyapae kabisa kwa kuwa Mungu atakuwa na kusudio lake hapo.

Thanks mrere+tofali+superman ni zaidi ya ushauri jaman mbarikiwe najiona mwenye furaha
 
kwani hamkupima kabla ya ndoa.......?

Inaonekana alikuwa mpenzi wake wa muda mrefu sana na katika mapenzi yao hakuwa wanatumia kinga so hawakuona kama kuna haja ya vipimo (hajasema hayo, ila ni mtizamo wangu maana wapo wengi sana ambao tunadoo sana ila ikifika wakati wa kutaka kufunga ndoa tunapima na wengine ndio hivyo tena nk)

Any yamekwisha tokea, anaitaji ushauri tumsaidie tu bila ya kuangalia ya nyuma, so if you something which can help him please angusha maushauri mwanana hapa jukwaani dada.
 
Mkuu Supervisor kama imethibitika huyo mkeo ana Ukimwi, kwanini unadhani ni busara kuendelea na Ndoa?
Mm nakushauri vunja hiyo ndoa, halafu kama ni maswala mengine ya kusaidiana kimaisha yaendelee kama kawaida.
Kati ya topic ngumu kuchangia ni kama hizi. Inatia huruma sana kumwacha mwenzako kwa kuwa tu amekutwa positive na tayari ana mimba yako. Kuamua kumuacha ni dhahiri kwamba itabidi uwatangazie watu wote kwamba mkeo ni positive. Ilihali katika hali ya kawaida mngependa hiyo habari iwe siri yenu na utunze heshima na sifa ya mkeo. Katika mazingira kama haya ukimuacha yupo likely kujiua maana atatambua wazi kwamba hiyo ni aibu kubwa kwake. Uamuzi huu unaweza kuwa mgumu sana. Ni bora mara mia muendelee na ndoa lakini mkatumia kondomu through out. Si vibaya kununua mabox na mabox. But kumwacha hata mimi nadhani ningeshindwa.
 
Nawaombea kwa MUNGU awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu but kama kweli uliapa kanisani basi kuwa nae hata katika shida hiii kubwa
 
ukisikia mtihani ndio huo sasa ukimuacha tu atajiua hata kama makosa ni yake na ukiendelea kuwa nae mijitu itawaita wote waathirika duu..

komaa tu ndio maisha hayo mkuu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom