Mkuu Supervisor,
Nimesoma post yako hakika ni jambo la ujasiri kulileta hapa na kuomba ushauri hapa JF. Hakika wapo watu wana utaalam hapa na nina hakika mwisho wa siku utapata ushauri wa kuwasaidia. Ila fahamu kuwa uamuzi wa mwisho ni wenu, wewe na mke wako.
1. Kwanza mshukuru Mungu sana kwa kuwa wewe huna VVU. Fikiria mkeo wako mnaishi wote na kutimiza tendo la ndoa ila Mungu akakunusuru wewe. Huenda huo ni mpango wa Mungu kukupima imani yako kuhusu mkeo na pia inawezekana pia umekuwa mzima ili uweze kuonyesha upendo na kumtunza mke wako hadi siku zake za duniani zimalizike. Kwa mantiki hii huna sababu ya kupata mawazo toka kwako au hapa kuwa eti vunja ndoa, nasema hapana ishi na mkeo hadi kifo kiwatenganishe.
2. Naamimini hata Clinic mmefundishwa kuwa unaweza kuwa na VVU na ukazaa watoto salama kwa kufuata masharti ya wataalam wa afya. Hata wewe na mkeo bado mnaweza kuzaa watoto wengine wa kutosha tu na kwa kuwa mna uhakika wa kuwatunza kwa kuwa wewe ni huna VVU. Kuna rafiki zangu wengi mmoja alikutwa na maambukizi miaka ya 2000 kati na mwingine karibuni na wamezaa watoto wazima kabisa bila maambukizi na wana afya njema kwa kuwa walielewesha jinsi ya kumlea mtoto akiwa mchanga na alipatiwa mama dawa kabla ya kujifungua na mtoto punde alipozaliwa. Wanaishi ndoa za furaha wakati mmoja wao hana maambukizi. Namaanisha mnakuwa mnatumia condom ila siku mnataka kupata mtoto mnafundishwa jinsi ya kufanya tendo kwa usalama bila condom na hakuna maambukizi hata chembe.
3. Bado mke wako ni mzuri, mpende sana na mtie moyo sana. Kumpenda kwako na kumtia moyo kutamfanya CD4 ziwe za kutosha na kidonge hatakimeza kabisa kwa muda mrefu sana. Jua kama akikubali hali na akiishi kwa upendo toka kwako anaweza kuishi zaidi ya miaka 10 bila kumeza kidonge na kama akianza kumeza kidonge ana uhakika wa kuishi another 10 to 20 years. Sasa hapo hamjawa wazee? Fahamu kuna maisha baada ya kupata VVU.
4. Mkuu Supervisor, naamini umewahi kuwa na ndugu au rafiki ambaye ameugua ugonjwa wa Cancer au Sukari ya kuzidi sana. Magonjwa haya yanaua haraka sana hasa kama huna uwezo kifedha kwa ajili ya dawa na chakula. Cancer inategemea na kuwa iko damuni, ndani ya mwili kama tumboni, ubongo, mapafu, utumbo, kizazi, etc Cancer za aina hii kama huna uwezo hata miaka 3 ukiishi ni bahati sana. Tumour za nje ya mwili kidongo ndizo unaweza kuishi muda ila nayo inategemena matunzo na dawa. Kwa hali hii kama mtu ana Cancer kuishi miaka 5-10 ni kitendawili sana (japo wachache wenye hela wameweza). Kwa hali hii nasema ni bora uwe na VVU ufahamu mapema uwe unakula balanced diet na kufuata masharti mengine ya wataalam na utaishi over 30-40 years na virusi plus ya ujana kwa hiyo waweza kufa at 60-70 years and above. Kuna mifano hai. Nina uncle wangu alikufa miaka ya 90 na mke yupo tena kijijini chuma cha pua hafi leo wala kesho. Hana wasiwasi. Nina rafiki mwingine ana miaka 10 hata kidonge hajagusa na CD4 ni zaidi ya 1000. Wapo wengi wa aina hii na wameikubali hali.
5. Ninajua unawaza kwa kuwa ungetamani ufanye tendo la ndoa bila kinga, hakika ni kweli. Lakini fahamu si lazima sana. Zipo condom nzuri na ikivaa ladha ni murua tu. Tumia condom kwa usahihi, jitahidi kufanya romance za kissing maeneo ya nje ya mwili na yapo mengi ya kusisimua tu si lazima deep kissing (toungue na kule kunako kwenu wote). Nina hakika utaridhika tu. Mbona tunatembea na vicheche tangu tukiwa vijana miaka na miaka hadi mtu unapooa? Kwani kuna madhara gani. Binafsi sijaona tabu ya kutumia condom.
6. Narudia tena mpende mke wako, mpe nafasi katika maisha na maendeleao yenu, fanyeni siri na mwisho wa siku utavikwa medani ya upendo na kujali.
Ninakutakia kila la heri na usikubali kuachana na mke wako, atapata shida na atakufa haraka utabaki na kovu la kumnyanyapaa maisha yako yote.
Dedicted Love forever!!!