Mke wangu ni HIV Positive

Mke wangu ni HIV Positive

Supervisor

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
559
Reaction score
208
Habari zenu wana JF.

Poleni na mihangaiko ya wiki nzima na leo hatimaye mmerejea kulijenga taifa. Jamani nimejitokeza leo kuwaeleza true story ya maisha yangu na kama kuna ushauri basi nitaupokea. Mimi nilioa kwa ndoa takatifu mwez Sept 2012. Ilipofika Nov 2012 Mke wangu alipata ujauzito na kila m2 kati yetu akawa na furaha.

Sasa ilipofikia muda wa kwenda clinic kama ilivyo ada mnatakiwa kuwa wote ili kuweza kupata nasaha na hatimaye kupima maambukizo ya HIV. Baada ya yote tukapima na yeye Mke wangu akakutwa anaishi na virus va UKIMWI na mimi niko salama kabisa. Kwel alilia sana na Nurse akapata shida sana ya kumbembeleza hatimaye akatulia na tukatoka akwa na uso wa tabasamu bandia.

Tulipofika nyumban kilio kilianza upya na mimi nikionekana usoni sina hata lepe la hofu wakati moyoni nilikuwa naumia sana. Baadae ucku akaniomba kuwa kwa sababu Kanisani tulifundishwa kuwa ndoa yaweza vunjwa kama mmoja wapo akionekana ni malaya. Ki ukwel mimi nilimkatalia nikamwambia Mi ni wake mpaka kifo kitakapo tutenganisha, wala hakuamini macho yake.

Kwa sasa anaonekana yuko at least normal ki akili na leo ameenda kazini. Yeye binafsi ni muumini mzuri na anapenda kwel kuimba na kumsifu Mungu.

Naomba ushauri wenu tafadhali.
 
Kapimeni tena na majibu yakiwa ni hivyo hivyo basi mnaweza kuachana. Ndoa inaweza vunjwa iwapo mmoja ana ugonjwa usiotibika.
 
mmh hebu kapimeni Angaza tena maana hivi viclinic hosp vinavyoanzishwa holera holera hata vipimo vyao ni headahce tu...usijekuta wamechakachua wakaharib ndoa yako bure
 
Supervisor, huu ni mtihani sana... Hasa kwa wale ambao ni wanandoa. Hata hivyo ushauri ambao unaomba hapa na jinsi ulivyowakilisha suala lako kidogo inakuwa haijakamilika.

Imeshapita miezi karibu 5 toka mpitie hilo suala; Maswali ya msingi kwako hapa ni wewe una msimamo upi? Yeye kuwa muathirika na wewe kutokuwa imekufanya ujisikie vipi/umfikirie vipi ukiwa na mtazamo wa maamuzi yepi?

Maswali mengine ni kuwa unadhani upo tayari kuwa nae siku zote kama mkeo (wacha suala la kusema mmefunga ndoa); nauliza kwa misingi ya uhalisia of what your really want to do na vile moyo wako unakusukuma.
 
Last edited by a moderator:
Ukiachana naye itasaidia nini? Je, mlioana bila kupima afya zenu (maana ndo taratibu za madhehebu mengi siku hizi)?
Ndoa na iheshimiwe, (kaupataje??????). Umechukua uamuzi sahihi kabisa kutoamua kuachana naye:yo:
 
Mkuu Supervisor kama imethibitika huyo mkeo ana Ukimwi, kwanini unadhani ni busara kuendelea na Ndoa?
Mm nakushauri vunja hiyo ndoa, halafu kama ni maswala mengine ya kusaidiana kimaisha yaendelee kama kawaida.
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu wana JF.

Poleni na mihangaiko ya wiki nzima na leo hatimaye mmerejea kulijenga taifa. Jamani nimejitokeza leo kuwaeleza true story ya maisha yangu na kama kuna ushauri basi nitaupokea. Mimi nilioa kwa ndoa takatifu mwez Sept 2012. Ilipofika Nov 2012 Mke wangu alipata ujauzito na kila m2 kati yetu akawa na furaha.

Sasa ilipofikia muda wa kwenda clinic kama ilivyo ada mnatakiwa kuwa wote ili kuweza kupata nasaha na hatimaye kupima maambukizo ya HIV. Baada ya yote tukapima na yeye Mke wangu akakutwa anaishi na virus va UKIMWI na mimi niko salama kabisa. Kwel alilia sana na Nurse akapata shida sana ya kumbembeleza hatimaye akatulia na tukatoka akwa na uso wa tabasamu bandia.

Tulipofika nyumban kilio kilianza upya na mimi nikionekana usoni sina hata lepe la hofu wakati moyoni nilikuwa naumia sana. Baadae ucku akaniomba kuwa kwa sababu Kanisani tulifundishwa kuwa ndoa yaweza vunjwa kama mmoja wapo akionekana ni malaya. Ki ukwel mimi nilimkatalia nikamwambia Mi ni wake mpaka kifo kitakapo tutenganisha, wala hakuamini macho yake.

Kwa sasa anaonekana yuko at least normal ki akili na leo ameenda kazini. Yeye binafsi ni muumini mzuri na anapenda kwel kuimba na kumsifu Mungu. Naomba ushauri wenu tafadhali.

Pole sana lakini hongera kwa ujasiri wako!Ningekuuliza maswali kadhaa,ila nahisi hayana maana kwa sasa!Hapa tusubiri wadau wengine watasemaje,ila kwa mimi cha kukushauri ni ni kupigia mstari uamuzi wako wa kuendelea kuishi na mkeo wa ndoa.Maadamu mmeshajua tatizo,ni kwenu sasa kukaa chini kumlinda mtoto aliyeko tumboni,na wewe ambaye hujaambukizwa.Amini inawezekana kuishi na mwenza aliyeathirika,bila athari,ilimradi mfuate nasaha za washauri.Na mkiishi kwa furaha,haya mkeo ataishi maisha marefu....
 
Kwanza mlifanya kosa kufunga ndoa tena takatifu bila kupima ukimwi labda kama mlikuwa tayari mlishandoana kabla ya kufunga ndoa, kama ni hivyo hiyo haikuwa ndoa takatifu but ilikuwa ni ndoa takafujo.
Pili, huo ni mzigo wako ukubali kama ulivyoukubali.
Tatu, katafute sababu ya kwa nini wewe usiambukizwe naye? Kama una aina fulani ya damu isiyopenyesha virusi basi endelea kula tunda kwa raha zako.
Nne, akijifungua salama ndo awe mtoto wenu wa kwanza na wa mwisho-usimpe mimba tena.
Tano, akipoteza uhai wakati wa kujifungua basi oa mwanamke mwingine baada ya kuwa umeshapima mara kadhaa na kugundua kuwa hujaambukizwa. Over
 
ishi nae lakini inabidi muwe karibu na wataalam wa afya,ili kuishi kwa matumaini na kufuata ushauri.pole sana ni mtihani mgumu sana
 
Pole sana lakini hongera kwa ujasiri wako!Ningekuuliza maswali kadhaa,ila nahisi hayana maana kwa sasa!Hapa tusubiri wadau wengine watasemaje,ila kwa mimi cha kukushauri ni ni kupigia mstari uamuzi wako wa kuendelea kuishi na mkeo wa ndoa.Maadamu mmeshajua tatizo,ni kwenu sasa kukaa chini kumlinda mtoto aliyeko tumboni,na wewe ambaye hujaambukizwa.Amini inawezekana kuishi na mwenza aliyeathirika,bila athari,ilimradi mfuate nasaha za washauri.Na mkiishi kwa furaha,haya mkeo ataishi maisha marefu....

Nakushukru sana kwa ushauri wako
 
pole kwa masaibu hayo makubwa
Mungu ndio amekulinda hadi leo
cha msingi mpende mkeo,mtunze vema na afuate shauri zote za kitabibu ili ajifungue mtoto asie na maambukizi
tumia kinga sasa kama condom, romance hizo acha
mpokee mkeo,usimnyanyapae au kumsema kwa watu.
kama mna family doctor mtafute kwa ushauri zaidi..
 
Kwanza mlifanya kosa kufunga ndoa tena takatifu bila kupima ukimwi labda kama mlikuwa tayari mlishandoana kabla ya kufunga ndoa, kama ni hivyo hiyo haikuwa ndoa takatifu but ilikuwa ni ndoa takafujo.
Pili, huo ni mzigo wako ukubali kama ulivyoukubali.
Tatu, katafute sababu ya kwa nini wewe usiambukizwe naye? Kama una aina fulani ya damu isiyopenyesha virusi basi endelea kula tunda kwa raha zako.
Nne, akijifungua salama ndo awe mtoto wenu wa kwanza na wa mwisho-usimpe mimba tena.
Tano, akipoteza uhai wakati wa kujifungua basi oa mwanamke mwingine baada ya kuwa umeshapima mara kadhaa na kugundua kuwa hujaambukizwa. Over

Mkuu BUCHANAGANDE, hebu naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hili.
 
Last edited by a moderator:
pole kwa masaibu hayo makubwa
Mungu ndio amekulinda hadi leo
cha msingi mpende mkeo,mtunze vema na afuate shauri zote za kitabibu ili ajifunge mtoto asie na maambukizi
tumia kinga sasa kama condom na romance hizo acha
mpokee mkeo,usimnyanyapae au kusema kwa watu.
kama mna family doctor mtafute kwa ushauri zaidi..

Thanks kwa ushauri mzuri ubarikiwe. Nurse pia alitoa ushauri huo
 
Kwani mke wako huyu mlikaa kama wachumba kwa muda gani? Je hamkuwahi kufanya mapenzi kabla ya kuoana?

Kwa uelewa wangu virusi vya ukimwi uchukua muda kujitokeza, si rahisi kujenga antibodies ya virusi vya ukimwi within two months i.e huwezi kuwa na uhakika kam wewe huko salama mpka muda upite. Vile kuna binadamu wengine wana kinga ya asili dhidi ya ukimwi, mwenzako anaweza kuwa na ukimwi lakini wewe ukabaki salama miaka yote hao wapo lakini ni wachache SANA.
 
pole sana, tulieni, kapimeni tena hospitali nyingine, shirikisheni walio kuwepo mkiungana, maamuzi yatafanyika baada ya hapo, kwani mkivunja ndoa watawaulizeni sababu ni nini, itachukua muda kuanza kujieleza upya, pole..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom