..."'Mke Wangu'/'Mume Wangu!'"...Tafsiri!

..."'Mke Wangu'/'Mume Wangu!'"...Tafsiri!

Soulmate mimi nitaungana na Babu Dark City, hayo makaratasi, hati, sijui mali ni sehemu au upande mwingine wa shilingi. Maamuzi yoyote ya kumchangua mwenzi wa maisha huambatana na vigezo 'vingine' ambavyo havihusiani na mapenzi ingawa vinacomplement kigezo cha mapenzi. So hata hayo makaratasi yanawezakuwa (au yasiwe) ni sehemu inayokamilisha u-mume au mke wangu.

.....soulmate MwanajamiiOne hebu acha kuuma uma maneno mpz wangu,
What ticks all the boxes for you mpaka unampa mtu cheo stahili kwamba huyu ndiye MUME WANGU....😊😊😊
 
Last edited by a moderator:
Saaafi kabisa kajukuuu.....

Eti makaratasi? Yana tofauti gani nna vinyago vya kuchonga vya wale jamaa wa pale Mwenge??

Mie nilimwambia Bibi kwamba ndoa yetu ilifungwa (deep in our hearts) siku ile tulipokubaliana kwamba hatuna sababu ya kuendelea kutafuta wengine...kwamba tulishafika Kigoma mwisho wa reli....

Makaratasi hata hayana maana zaidi ya kukidhi matakwa ya kisheria na mambo mengine mengine madogo madogo...

Babu DC!!

.....swahiba Dark City hiyo inaitwa kijikinaisha nae.... Kwamba hakunaga mwingine zaidi ya yeye "hata iweje!"

Phewww,
Wewe kweli mzee wa #busara
 
Last edited by a moderator:
wangu maana yule ninaemmiliki

Kihalali

Wangu aliyechukua nusu ya maisha yangu

Wangu maana ya mwili mmoja

Wangu kwa maana kiasili binadamu tunataka/penda kumiliki

Wangu maana nimeweka mipaka hapo kwamba ni territory yangu

Wangu maana mtu asinisogelee pande zangu

Wangu maana ndo alochukua moyo wangu

Wangu kwa maana ni sehemu yangu

Ya mwili wangu

Ya moyo wangu

Wangu kwa maana ya faraja yangu, furaha yangu, kicheko changu,

.....naam, naam BADILI TABIA, tiririka kaka... Funguka zaidi!
Kuna sifa gani kuu zinazomkubalisha yeye kuwa Mke Wako!?

Nimeligeuza swali hapo kutokana na majibu yako.
 
Last edited by a moderator:
.......saaaaafi sana! Masuke....
Tafsiri yako nzuri sana, ila je?
Utakubaliana nami kwamba bila mapenzi na urafiki haki moja baada ya nyingine hukiukwa?!

....ukikubaliana nami, ina maana "UNAWAJIBIKA" pia kwake....

Mimi niliandika hivyo kwa sababu ni mwanamume, kwa wanawake nao itabidi iwe hivyo hivyo na pale palipo mke waweke mume na palipo mwanamke waweke mwanamume na mengine yabaki kama yalivyo; kimsingi kila mmoja anakuwa na haki na wajibu kwa mwenzake kijamii na kisheria.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hivi Babu Dark City..............hauna rafiki yako wa mwaka 47 kama wewe unimegee pande mjukuu wako? Najiona kama nimepitwa na wakati kwa Dot com sipo wala kwa sikinde...........naelea tu angani. Hebu ntafutie mzee nimlee ! (Soulmate hii post (haihusiani na thread - USISOME)


Duuuuuuuuuuuuuuhhhhhhhhhhhhhhh,

Nakuonea huruma sana mjukuu wangu ila ndo hivyo tena...ingekuwa na sie wa 1947 tunaruhusiwa kupiga match ya watu zaidi ya wawili ningekualika home kwa bibi....Ila sasa wenzio tunadumisha mila....

Na bahati mbaya, Babu ni kama vile alikuwa mtoto pekee kwa baba ambaye hakuwa na makali...

Ipo siku kitakuja kibabu kijimilikishe na kukukabidhi pensheni yote ufanye mazoezi ya ku-manage mafweza..lol!!



Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
haki zote? Ufafanuz plz.. Inamana kubakwa,kupigwa,kunyanyaswa pia ni haki ?jamii na sheria vinaruhuru kwa huyo mwanamke unayemmiliki?

Munkari unajua maana ya haki lakini? ndo maana nikasema haki na wajibu na viendane na sheria za nchi pamoja na taratibu za jamii unapoishi, hakuna sheria inayoruhusu kubaka, hakuna sheria inayoruhusu kupiga wala hakuna sheria inayoruhusu kunyanyasa. lakini yote hayo watu wanafanya kutokana na mgandamizo ulioko ndani ya mtu mwenyewe, ukiona mtu anabaka usifikiri yuko sawa lazima kuna msukumo kutoka ndani unaomfanya aone kubaka ni sawa, na ukiona mtu anapiga vile vile hayuko sawa inaweza kuwa ni mgandamizo uliopo ndani yake na mara nyingi ni hasira hata kunyanyasa pia lazima kuwe na mgandamizo pia uliopo ndani ianweza kuwa ni msongo wa mawazo au hasira au naye alinyanyaswa wakati akiwa mdogo lakini kwa ujumla ukiona mtu anafanya yote uliyoyataja jua kwamba hayuko sawa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom