Mke wangu mchoyo anapika chakula kidogo sishibi kabisa

Mke wangu mchoyo anapika chakula kidogo sishibi kabisa

Nimeoa nina miezi 5 sasa ila tatizo kubwa ni kwamba mke wangu anapika chakula kidogo mno yani sishibi kabisa na namuachia hela ya matumizi ya kutosha ila sielewi nini kinamsumbua

Mpaka inafika kipindi kabla sijarudi nyumbani nipitie hotelini nile kwanza halafu ndio niende kwangu
Nimeongea nae sana lakini anaacha siku kadhaa halafu anarudia tena tabia yake
Ushauri wenu wakuu nimuache au nimfanye nini?
Mkuu, kwanza naona kama unamdhalilisha mkeo hapa. Na pia inaonyesha ni jinsi gani ulivyo mwanaume laini tena mwenye kupenda kulalamika.
Kwanza hauoni haya/aibu kuja hapa jf kumsema mkeo vibaya, ilhali bado ni mkeo...[emoji53] [emoji53]
Kisha ukimaliza kumuandika huyo mkeo hapa, alafu unaenda kula tena chakula chake na kujifunika nae shuka moja...[emoji45]
Ebu badilika mkuu, yaani jambo dogo kama hili unashindwa kulitolea maamuzi kama baba.... je siku ukija kumfumania hata kwenye sms sindio utajinyonga kabisa...[emoji46] [emoji46]
Wanaume wa Dar mna matatizo zana aiseeee..... na skuizi mnalalamika kuliko hata dada zenu...[emoji16] [emoji16]
 
nia ya jamaa sio kuelez matatizo ya mkewe bali kuomba msaada wa yanayomsibu so ungejikita kwenye kumsaidia zaidi kuliko kumbeza!!!1
Nyinyi wavulana wa mikoani mnashindwa kushika nafasi zenu kama wababa kwenye familia, hili jambo mfumbuzi wake ni yeye mwenyewe vinginevyo anipe number ya huyo bidada nimpigie simu
 
Huyo dawa yake mdogo mbona.usiwe unakula nyumbani uwe unakula hukohuko hotelini na wewe unaonekana unapenda kubust sana?
 
Niliambiwa hivi.. ukiiona unamwelekeza mwanamke jambo na hakuelewi basi juwa ni tabia yake hivyo jipange kumkubali na uendane nae
Sawa mkuu
 
Nimeoa nina miezi 5 sasa ila tatizo kubwa ni kwamba mke wangu anapika chakula kidogo mno yani sishibi kabisa na namuachia hela ya matumizi ya kutosha ila sielewi nini kinamsumbua

Mpaka inafika kipindi kabla sijarudi nyumbani nipitie hotelini nile kwanza halafu ndio niende kwangu
Nimeongea nae sana lakini anaacha siku kadhaa halafu anarudia tena tabia yake
Ushauri wenu wakuu nimuache au nimfanye nini?
Kula hotelini kila siku sio suluhisho maana kumbuka pia huyo ni mtu ambae auntakuwa nae for the rest of your lives so hutoweza kuwa unaenda kula hotelini kila siku labda kama ni mara moja moja, je umewahi kumuuliza kwanini anapika chakula kidogo ilhali ushamwambia hakikutoshi? pia kama ni mimi ningekuwa namrudisha jikoni hasa ukizingatia mara nyingi wanawake wengi kama ameshapika kamaliza ktenga huwa hawafurahii kurudi jikoni kupika tena so usumbufu ambao angekuwa anaupata kupika mara mbili mbili ungeweza kumfanya apike chakula cha kutosha maana atakuwa anajua bwana yule asiposhiba tu ntarudi jikoni tena esp chakula cha usiku, vipi na kile chakula kingine cha uzima unapewa kweli maana najaribu kufiria hiki unachokinunua kila siku unapewa kidogo hicho kingine unaweza kuta toka miezi mitano ya ndoa umepewa mara mbili tu!!!
 
Ninaomba ushauri tu mkuu
Ushauri hauombwi kwa style hiyo, kichwa cha habari "Mke Wangu Mchoyo" hiyo ni taarifa unaitoa ili tujue. Ungesema naombeni ushauri nifanyaje ili mke wangu anipikie nishibe hapo sasa kweli ungekua unaomba ushauri.
 
Nyinyi wavulana wa mikoani mnashindwa kushika nafasi zenu kama wababa kwenye familia, hili jambo mfumbuzi wake ni yeye mwenyewe vinginevyo anipe number ya huyo bidada nimpigie simu
ni kweli kaka hapo mfumbuzi ni yeye mwenyewe lakini pengine hajajua kama yeye ndo mtatuzi hivyo unaweza kumsaidia pia kwa kumwelewesha afanyeje, pia kuna faida za kushare vitu maana unaweza kuuliza ukakutana na mwenzio aliyepitia hali kama hiyo mkashare uzoefu wake yeye alifanyaje ikakusaidia japo sio kila njia inayomsaidia huyu ukii-apply kwa mwingine pia ikafanya kazi!!!!
 
Unaporudi uje na mazaga zaga kama matunda n.k. yawezekana yeye amelelewa zile familia mboga saba kwa hiyo hajazoea maugali makuubwa bali mapocho pocho kibao.
Najitahidi kwa hilo lakini mwenzangu ananiangusha
 
Mrudishe jikoni. Usiposhiba muambie mke wangu sijashiba. Pika tena. Akisharudia mara kadhaa ataelewa.

Ndoa sio maigizo. Utakula barabarani hadi lini? Funguka
Nitajaribu kufanya hivo
 
Back
Top Bottom