Mke wangu kachelewa kurudi kisa foleni

Mke wangu kachelewa kurudi kisa foleni

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,373
Saa kumi na moja jana jioni nilimwacha Ubungo nikaenda Mwenge, kisha kutoka Mwenge nikafika Tabata tunapoishi saa tatu.

Yeye kuanzia saa kumi na moja toka Ubungo kwenda Tabata mpaka sasa saa saba kamili usiku yupo kwenye foleni.

Kuja tu kawahi bafuni anaoga yaani hapa jazba zimenipanda natetemeka navibrate nikisimama chaji ndo inapanda.

Nipeni ushauri nitatulizaje hasira ?
 
Toka jana hasira haijaisha? Sasa inakuwaje; mnaongea au umemchunia? Kama anakuchiti utajua kwa sababu ni mkeo...hakuna mtu yeyote humu JF anayeweza kukupa jibu sahihi kuliko wewe mwenyewe...

Mfano mimi sijaona kama kuoga ni issue...maana haiwezekani alale bila kuoga...na kama ilikuwa saa saba ni lazima aoge alale...

Wewe jibu unalo...anachiti au achiti?
 
Kweli iyo folen? Embu muulize vizuri na kwa akili utajua tu kama ni foleni au la!! Dah jamani? Pole lakini.
 
Inawezekana, wanawake wanachomekewa sana kwenye foleni. Kama kugongewa utagongewa mchana, siyo usiku hivyo.
 
Wamjua mkeo, hivyo jiulize maswali na majibu utakuwanayo. Mfano: je ana tabia ya kuchelewa nyumbani angalau? Akirudigi huwa anafikia bafuni? Au ana tabia ya kuoga usiku? Msome na body language yake. Ila kuna kitu hakiko sawa, angesema tu kuwa alipitia sehemu zingine, foleni ya ubungo mpaka tabata saa saba usiku?? Mi mwenyeji wa Vetenary, naijua pia hii barabara na foleni zake vizuri sana, foleni kama hiyo ndo itakuwa ya kwanza. Yaani mpaka saa saba usiku? Pole, ila una haki ya kuwa na jazba. Huenda ni kweli kulikuwa na foleni au kuna jambo tu lilimsibu akaona atumie foleni.
 
Ha!......huyo mbona kawahi.......mimi nipo kwenye foleni hapa kutoka Sanawari kwenda Kijenge ndio kwanza hata daraja la mto Themi sijafika.......jamani naomba muelewe mambo ya foleni.......hivi mnataka tupae........?
 
barafuyamoto

Hiyo foleni ya kufika saa Saba labda ya Mbagalla au Kibamba kabla ya upanuzi wa Barabara ....kwa watu wa maeneo yote yaliyobaki mjini ukitoa Siku Za Mvua saa nne ya usiku Ikifika unaweza kwenda popote NDani ya dakika 45 hadi 60 ....kwa nje ya mji ...
Ndio maana ambao hawapendi husumbufu huenda happy hour kwenye spots Za mjini ie holiday inn ,south sun ,raphsodys ,gymkhana ,Msumba lounge Etc ...saa 3.30 Ikifika wanaondoka na wanafikia muda sawa na walioondoka mjini saa Moja
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana, wanawake wanachomekewa sana kwenye foleni. Kama kugongewa utagongewa mchana, siyo usiku hivyo.

Umeonaa eeeeh........haswa hizi daladala.........wajinga kweli hawa makonda.........sijui wananitaka nini.......
 
Ha!......huyo mbona kawahi.......mimi nipo kwenye foleni hapa kutoka Sanawari kwenda Kijenge ndio kwanza hata daraja la mto Themi sijafika.......jamani naomba muelewe mambo ya foleni.......hivi mnataka tupae........?

Duh! Umecomment saa 1: 36am, hiyo bara bara ni one way na inatakiwa kupishanisha magari au kusema Arusha mna magari mengi? Mbona usiku sana kuwa na foleni lote hilo. Pole hata hivyo.
 
Kazi mnayo, sisi huku kijijini hakuna hayo mambo kabisaaaaa
 
Possibility ya kuwa kakudanganya ni 89%...
Lakini ukweli ni upi? Kuwa alienda kugegedwa...not necessary...

Kuna wanaume wanoko mpaka unaweza jikuta unadanganya hadi unaonekana cheater...

Mfano naweza pokea simu ya mtu anayenifukuzia...mume wangu akiniuliza 'who was that'...nikamwambia wrong number...ili kuepusha shari...

Sasa akija kushtukia kuwa ni mtu anayepiga mara kwa mara unadhani ata conclude nini? nina cheat...

Yani ukajikuta una vitabia vya kitoto tokana na unoko wa mume (hata mke)...

anaweza kuwa alipitia mahali na shoga zake...anajua akikwambia ukweli utamfikiria vibaya ndio kaona ni heri asingizie foleni...

Mimi mwenyewe nshadanganya sana...na wala sina mchepuko...ila naepusha shari...


Foleni ya ubungo kwenda tabata masaa tano?
 
Duh! Umecomment saa 1: 36am, hiyo bara bara ni one way na inatakiwa kupishanisha magari au kusema Arusha mna magari mengi? Mbona usiku sana kuwa na foleni lote hilo. Pole hata hivyo.

Arusha ni mji wa mamilionea.........kila mtu ana gari......
Ndio naingia Philips...........
 
tuliza munkari kijana, wala usioneshe jazba. kama una moyo mpana wenye uwezo wa kubeba mazito kama sisi ma Al-Salafi basi unaweza kufanya mawili, moja lisilo na maumivu sana ni kuazima gari yake siku moja na kwenda kuiwekea system ya tracking, la pili ambalo ni la bei rahisi kiasi ni kuweka system ya kutrack simu yake: hili ndiyo hasaaa zito na litakuletea majibu si muda. Wengi huwa wanapinga kumfuatilia mke/mume, lakini mkiwa kwenye mahusiano na unahisi kudanganywa mimi huwa naona ni heri kuujua ukweli pasina shaka kuliko kuishi maisha ya udanganyifu!
 
...pole sana mkuu, yawezekana ni kweli kapigwa!
"msamehe tu' wake zetu siku hizi ni kama viti vya ma-basi (tena daladala)...!"
 
...pole sana mkuu, yawezekana ni kweli kapigwa!
"msamehe tu' wake zetu siku hizi ni kama viti vya ma-basi (tena daladala)...!"

Ni kweli, ila basi wawage wanasema true lies. Kuisingizia foleni saa saba usiku haipendezi.
 
Ha!......huyo mbona kawahi.......mimi nipo kwenye foleni hapa kutoka Sanawari kwenda Kijenge ndio kwanza hata daraja la mto Themi sijafika.......jamani naomba muelewe mambo ya foleni.......hivi mnataka tupae........?
Mmmmh Arusha.....?
Duuu .......siamini!
Duu kweli Arusha kuna mabadiliko siku hizi....foleni muda huu.......
Sasa kama mji kama Arusha unakuwa na foleni muda huu ndio Dar mtu ashangae mkewe kushikwa na foleni?
 
Back
Top Bottom