Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 38,020
Mila gani wewe za kishenzi hizo.... Kuendekeza umalaya tu huko. Kama vipi toa talaka halafu umuoe mle wa marehemuAngalia utapata laana mwanamke, mambo ya mila sio ya kuchezea utaokota makopo ohooooo!!!!
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.
Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.
Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...
hana la kujitetea huyo mpenda wake za marehemu a.k.a wajaneHivi mke wa nduguyo ni damu ya nduguyo kweli? Au wewe umekosa la kujitetea
Naomba tuheshimiane mkuu, mimi nafuata mila za kabila letu hata wewe una mila za kwenu sema tu umezitelekeza kwa kudanganywa na mila za Magharibihana la kujitetea huyo mpenda wake za marehemu a.k.a wajane
Acha kashfa, kufa kwa ajali ndio ukimwi?.....Unajua kaka yako kafa na nini? Utakufa kwa ukimwi shauri yako.
Hebu muache huyo mkeo usije muua bure!!
Wewe nadhani unanionea wivu tu kuwa nitafaidi wake wawili lakini hata wewe unatamani ikutokeeMila gani wewe za kishenzi hizo.... Kuendekeza umalaya tu huko. Kama vipi toa talaka halafu umuoe mle wa marehemu
Wewe hujui mambo ya mila ndio maana unadharau, ngoja yakukute utakuja hapa kusimulia, labda ufanye siriMikosi gani kwa mfano?
Je ukitunza watoto afu usitoe unyumba kwa mjane?
Disown you? Do they own you? - Nkem Owoh
Hivi unaweza kuniambia ni lini mila za kale zilifutwa? na kwa mamlaka ya nani?kwani aliyekufa kwa ajali hawezi kuwa alikuwa nao kabla we una hakika gani na afya yake? Mila nyingine inabidi zifutwe tu hali ya sasa au we mwenzetu unaishi nchi gani, mana nashangaa eti mpaka leo hii bado hizo mila na desturi........tafakari na chukua hatua!!!!!! Achana na mambo ya kizamani
Mtani hili nalo ni jamboKwa
kuwa kuachwa na mkeo sio uvunjifu wa mila, binafsi naona ni bora akuache
ili wewe mshika mila uendeleze mila
Hahahahaha kweli hapo naona inafagiliwa ngono tu si bure. Yaani hata enjili huko aliko huyu bwana haijafika au hata ustarabu wa kawaida nao hakuna loh mbona kazi ipo. Kuna mila njema na mila mbovu , mila mbovu yafaa zikaachwa na njema zikaendelezwa. Hivi huwezi mtu kutoa msaada mpaka na wewe upate kitu loooooooooooh shame on himMpe talaka yake aende zake kwa amani na MUNGU amjalie huko aendako afanikiwe wala asikukumbuke tena ubaki na mjane wako, unataka kumuua mwenzio na virus. Bado watu badala ya kutafuta hela mnakaa vikao vya uzinzi.
Umejuaje kama huyo mke wa kaka yako anakupenda? Unahisi watoto wake watajisikiaje wakikuona unalala kitanda cha baba yao? Ingekuwa ni mama yako anatembea na baba yako mdogo ungejisikiaje?
Inaelekea ulikuwa unamtamani toka kaka yako akiwa hai!
Kuna kabila moja huku kwenye visiwa vya ziwa victoria, wana tabia ya "KUWATAKASA WAJANE".eti kila mwanamke anayefiwa na mumewe, ili aweze kuolewa na mwanamme mwingine lazima "ATAKASWE", kwa maana kwamba kuna mwanaume(MTAKASAJI) ameteuliwa kwa kazi hii ya kuwatakasa(KUWAGEGEDA) wajane kabla hawajaolewa tena ili wasipate mikosi kwenye ndoa zao.
Sijajua kama huyu mtakasaji ameoa, na kama ameoa, mkewe anajisikiaje wanapoletwa wajane pale kwake kwa ajili ya kutakaswa?
marehemu kaka yako alipima???????swali lingine...hivi huko kwenu tarehe mnazotumia zimeshafika ANGALAU 1900?swali la mwisho tafadhali......unaishi misitu ya kongo au tanzania hii hii?