Mke wangu hapendi kuongozana na mimi barabarani

raphael linkala

New Member
Jan 4, 2016
2
27
Wadau heri ya mwaka mpya,

Wife amekuwa hapendi kuongozana nami katika safari mbali mbali misiba, sherehe, outing na kadhalika, sio kwamba anakataa moja kwa moja bali atatafuta sababu ili twende tofauti, na akikubali kwenda anakuwa uncomfortable na uwepo wangu.

Mwezi uliopita wa 12 tulisafiri wote kwenda up country nyumbani kwao mkoani kwa mapumziko ya end year, tulianzia mkoani kwetu, mwisho tukamalizia kwao, sasa tukiwa kwao, mdogo wake wa kike ndie alikuwa akizunguka nami mjini kutalii na kunionesha sehemu mbali mbali, wife alikuwa akinipiga chenga ndipo shemeji akaamua kunipa kampani.

Tuliijadili sana hii tabia ya dada yake ambayo hata yeye akasema ameiona kwa muda mrefu sana, anashindwa kuelewa tatizo ni nini? Sababu sina ulemavu, mwonekano wangu ni wa kawaida, wakiitwa ma handsome siwezi kutoka, lakini pia wakiitwa wabaya pia siwezi kutoka, ni wa kawaida.

Siku ya kuondoka Arusha, tukawa na ugomvi mkubwa sana kwamba nakosaje aibu kiasi kile, kuzunguka na mdogo wake hadi watu kunielewa vibaya, kiasi kuwa akakataa kabisa kwa hasira shemeji asije na sisi Dar maana huwa tunaishi nae, hadi wazazi wao walipomuamuru akakubali.

Tabia hii imenichosha sana kufikia hatua najiona sina thamani, tukienda harusini au outing ya pamoja na marafiki pamoja na waume zao utashangaa kila nikitaka kuchangia mada ananiminya mkono nisizungumze labda nitaongea jambo la kumuaibisha wakati mimi kwanza sio muongeaji, waume wa marafiki zake wataongea wee mimi nipo kimya, mimi nikichangia tu ni ugomvi, ananikosoa mbele yao kila nalochangia tena kwa kunishushua, hivyo nakaa kimya muda wote hadi wengine waulize mbona huongei.

Nilishajiuliza huenda huwa naongea pumba, hata hivyo hapana, mimi huwa ni mtu mwenye kuchagua maneno sana kabla ya kuongea.

Sasa naomba mnisaidie mawazo, tatizo ni nini hasa? Ni suala la muda mrefu hivyo nimeshachoka, nataka kufanya mabadiliko, nahitaji mke mwenye kunithamini na ambae yupo proud of me nahisi huyu hanipendi Ingawa tuna watoto wawili.

Nawasilisha kwenu
 
Last edited by a moderator:
Inaonekana hayo mambo unafanyiwa sehemu public...hujatuelezea tabia yake mkiwa ndani ya zile kuta 4....huwa unanyimwa? Kama huko pia hadi utongoze, ujue huna chako mkuu!
 
Hahaha nimecheka kama mazuri!

Kwanza nianze na disclaimer. Binafsi i love flaunting my man around, kwa sababu siwezi kutoka na mwanaume ambae i am not proud of.

Hisia zangu ni kuwa huyu dada hakuwa hivi mwanzo. Atakuwa alimpenda kwa dhati huyu mtoa mada lakini ikafika mahali akawa hayuko proud tena na mumewe. Na suspicion yangu ya kwanza ni kuwa mwanaume anafanya ujinga (labda wa kuwa na affairs) hadharani kiasi kwamba dada anaona aibu kuitwa mke wa fulani.

Mahusiano ni mtihani. Ila mtihani mkubwa ni mwenza kutokuwa proud na wewe. Kama huwezi kurekebisha hiyo kasoro iliyomfanya aanze kukukimbia, jiandae kisaikolojia manake anakupigia mahesabu ya kukuacha aisee. Kama hujui sababu muulize mdogo wake ama rafiki yake wa kike. Wanaume huwa hawaoni sababu za wazi kabisa. Niamini, mwanamke hawezi kukukimbia kwa sababu ya muonekano ila kwa sababu ya how you make her feel.

Afu wewe The Boss, unanichimba eeh!
Hahaaa nimecheka kwa kweli
una uhakika hujamuoa BADILI TABIA ?

au King'asti ?

hadi kuongea anaogopa utamuaibisha?
level ya mkeo shule ikoje?kulinganisha na yako?
unavaaje?kama Kofi Olomide?
 
Kaka hiyo ndoa unaonekana wewe ndo umeilazimisha inabidi uanze kuwa ngangari inaonekana unampenda kuzidi anavyokupenda
anakuone wewe sio type yake na bila shaka mpka sasa yeye anatype yake anagegedwa mdogomdogo
saasa cha kufanya naomba umpotezee kabisa ukifika nyumbani fanya mambo yako. mkitaka kutoka toka wewe fanya kila kitu mwenyewe
 
Hahaha nimecheka kama mazuri!

Kwanza nianze na disclaimer. Binafsi i love flaunting my man around, kwa sababu siwezi kutoka na mwanaume ambae i am not proud of.

Hisia zangu ni kuwa huyu dada hakuwa hivi mwanzo. Atakuwa alimpenda kwa dhati huyu mtoa mada lakini ikafika mahali akawa hayuko proud tena na mumewe. Na suspicion yangu ya kwanza ni kuwa mwanaume anafanya ujinga (labda wa kuwa na affairs) hadharani kiasi kwamba dada anaona aibu kuitwa mke wa fulani.

Mahusiano ni mtihani. Ila mtihani mkubwa ni mwenza kutokuwa proud na wewe. Kama huwezi kurekebisha hiyo kasoro iliyomfanya aanze kukukimbia, jiandae kisaikolojia manake anakupigia mahesabu ya kukuacha aisee. Kama hujui sababu muulize mdogo wake ama rafiki yake wa kike. Wanaume huwa hawaoni sababu za wazi kabisa. Niamini, mwanamke hawezi kukukimbia kwa sababu ya muonekano ila kwa sababu ya how you make her feel.

Afu wewe The Boss, unanichimba eeh!
Mumeo utakua nae proud hadharani hata akivaa kama Koffi Olomide?
au utamtanguliza kiaina....hahaaa..

kweli labda anaandaliwa kuachwa
 
Bossman, faida moja ya mwanamke mwenye akili anajua hata jinsi ya kukubadili bila wewe kujua. Kama anavaa kama koffi olomide (hivi koffi anavaa vibaya ama nampenda hadi sijagundua uvaaji wake? Ila ni mwanamuziki, kuimba na suti na tai labda isingekuwa sawa); dawa ndogo tu ningejipa kazi ya kumnunulia nguo. Manipulating from around the corner.

Unajua ukishanunuliwa mashati kama 10 na sarawili 5 na viatu pair 3, kila asubuhi ukaambiwa vaa hili shati linakupendeza sana; ukiingia ofisini unahisi kila mtu anakuangalia kwa sababu mkeo kakusifia. Sasa kama umetoka wakati mke kageukia ukutani, utahitaji mama mzazi akujengee confidence upya.
Mumeo utakua nae proud hadharani hata akivaa kama Koffi Olomide?
au utamtanguliza kiaina....hahaaa..

kweli labda anaandaliwa kuachwa
 
Sio Muda wakulia lia na kuomba ushauri huku maamuzi unayo wewe ili hali wakati mnakutana mlikuwa wawili hivyo jukumu la kupanga na kupangua unalo wewe...lkn kwa namna nyingine nikiambiwa niseme neno lolote juu ya hili...huyu HAKUFAI...HAKUFAI NASEMA HAKUFAI...shuka panda gari nyingine..ila hakikisha gari utakalo lipanda safari hii liwe na Bima....Biblia inasema Heri kuishi porini na wanyama wakali kuliko kuishi na mwanamke MGONVI..
 
Kuna mdada mmoja aliniambia unajua mume wangu ni std 7, halafu amekulia makambi ya mgodini? Hadi kumfikisha hapa nimefanya kazi haswa and i am proud of him. Nilishangaa sana. Wanapendana na kuheshimiana waziwazi. Mwanaume anakiri yeye ni kichwa lakini engine ni mkewe. Amejifunza kumuamini mkewe kwa sababu anasali sana. Hiyo tu, sio kwa sababu ana digirii
Nimependa maswali yako ngoja nami nisubili majibu
 
Kuna mambo magumu sana kuyafanya kwenye jamii za kiafrika. Hivi unaweza kusema namuacha mke wangu kwa sababu hafuatani na mimi? Wakati anapika, anaangalia nyumba, anaangalia wanao, na akienda kijijini na wewe anakaa nyumbani akipika na kusimamia mambo mengine na anakataa kuenda kubarizi na wewe mitaani?

Mtoa mada anapaswa kuongea na mkewe na kufanyia kazi majibu. Sio kuleta ubabe wa kiume. Mapenzi hayashikiliwi na plasta.
Sio Muda wakulia lia na kuimba ushauri huku maamuzi unayo wewe ili hali wakati mnakutana mlikuwa wawili hivyo jukumu la kupanga na kupangua unalo wewe...lkn kwa namna nyingine nikiambiwa niseme neno lolote juu ya hili...HAKUFAI...HAKUFAI NASEMA HAKUFAI...shuka panda gari nyingine..ila hakikisha gari utakayo ipanda safari hii ina Bima....Biblia inasema Heri kuishi porini na wanyama wakali kuliko kuishi na mwanamke MGONVI..
 
Duh mkuu hapo kwanza angalia mtoko kwa upande wa kimavazi je unavaa kama hao waume wa wengine. pengine kasoro zaidi itakuwa ktk mavazi hebu jifikirie kwa upande wa mavazi na muonekano wako je wajiweka soap soap....mfano kama sura yako ina ndevu then nyoa usiwe na mandevu takachafua kidevu chote, kama ni nywele piga dawa ile zinang'aa kidogo, angalia upande wa manukato je watumia au lah, tumia gharama kidogo ktk suala la mavazi maana ktk mavazi na muonekano ndo huleta hali hii.

Kama hayo yote unayatimiza jaribu kuangalia wanaume ambao wife anawakubali wakiwa wanachangia maoni yao then jicheki kuna tofauti ipi kati yao na wao. ila kama hayo yote yapo sawa basi mchunguze mkeo atakuwa na tabia zile za umimi yaani hapendi watu anataka kuwa peke yake. sasa kama hayo yote umeyatimiza basi sijui u dini gani taratibu za kuacha mke zinatofautiana. ila huwezi kuishi na mke wa hivyo maana hata ukiugua sidhani kama atakuhudumia.
 
Back
Top Bottom