Mke wangu hana nidhamu?

Mke wangu hana nidhamu?

Mimi nina mke na tuna mtoto mmoja. Lakini tangu nimemuoa huyu mwanamke maka mitatu iliyopita hajawahi hata siku moja kunikaribisha kwenda kuoga maji bafuni kwa adabu ambazo mimi nimekuwa nikiziona katika maeneo mengine. Kwa mfano anaweza kuandaa maji bafuni na kuniambia...nyanyuka ukaoge maji yako bafuni...hivi ina maana anshindwa kusema maneno kama karibu mme wangu ukaoge maji yako tayari bafuni? Hata kwa chakua hali ni hiyohiyo.
Kutokana na hili pamoja na mengine nimekuwa nikimchukulia kuwa hana adabu kwa mme wake au nakosea wadau?
Naombeni msaad wenu nifanye ninikumfanya anitendee ninavyopenda kutendewa maana nikimwambia kuwa sifurahii jinsi anavyonifanyia anaonekana kunishangaa tu na kuishia kunilaumu eti labda nina visa vingine tofauti na hilo!
ifanye nini ndugu zangu? naomba mnishauri tafadhali!

Jesus Christ - Snipper sasa maji yanayotoka kwenye shower unakaribishwa vipi? anatakiwa akufungulie au?
 
Last edited by a moderator:
Huyu "Amu" naye ni Mmoja wao kutokana na Majibu yake. Kwa Hilo suala la Nyumba ndogo ni vigumu kuliteketeza kutokana na Vijitabia kama hivi.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Wanaume wetu bwana, bora atafute nyumba ndogo kuliko kutengeneza bafu zuri la kupunguza shughuli zisizo na tija asubuhi, khaaaah!!

asubuhi ndo kila kitu jamani, starehe hadi kieleweke.

Mkuu, hii tabia ilikuwepo tangu mwanzo na ukaiona ya kawaida au amebadilika? Nadhani issues zimeshaanza katika ndoa yako ndio maana hata yale ulitoamua kuyamezea yameanza kukukera.
 
Snipper inawezekana hivyo ndivyo mkeo alivyo hajazoea kubembeleza au niseme kunyenyekea.. nafikiri la muhimu usitumie nguvu kupata hicho unachotamani, tumia busara zaidi lolz..

Tabia haina dawa kaka angu.. Hivyo mwelekeze taratibu atakusomaaaa tu..

Aidha, usiigize yanayojiri ktk mahusiano/ndoa za wengine as hizi ishu hazina formula.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Tafuta nyumba ndogo chai utanywea bafuni utaogeshwa utasuguliwa utapakwa mafuta itachanwa nywele kila huduma unayokosa kwa mkeo hapo utaipata Mara Tatu yake

mimi nipo kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 na mpaka leo nikiweka chakula namkaribisha mume wangu "karibu mpenzi chakula" bafuni kwangu kuna maji siku zote tunaoga pamoja na several times ninamuogesha, namsugua miguu, namkata kucha, namchana nywele, nampasia nguo zake,,hata perfume ni mimi nampulizia...sio mara moja nampelekea chakula ofisini"lunch box" kwa surprise....naingia jikoni several times namuandalia vitu spesho hasa week ends ninapokuwa siendi ofisini... lkn bado alinicheat ...nyie wanaume bana hata mbebwe mgongoni na mbeleko hamriziki......
 
KAMUSI, Wewe ndiye unajua kazi big up, huenda ulikosea kidogo kupika na vingine! Ila vinarekebishika tafutia UVUMBUZI
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    8.4 KB · Views: 144
wandugu inabidi tufahamu ya kwamba kuoa sio jambo la lazima, kwani maoja ya mafundisho wanayopewa wanawake kwenye matamasha ya haki sawa ni kuto kumtii mwanaume yaana hata utii ule wa kawaida ni kuvunja haki ya mwanamke
 
Lokisa big up to u men for ur coments now baelezee banaume bengine baelewe.lazima utakuwa baba mzuri kwa watoto na mume bora pia kwa mkeo wa ukwee,wanaume jamani sometyme kuwen na roho za kibinadamu haimaanishi ufanye kila kitu bt to some extence u can assist naye aone kuna mtu wa karibu anamjali lol

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mimi nina mke na tuna mtoto mmoja. Lakini tangu nimemuoa huyu mwanamke maka mitatu iliyopita hajawahi hata siku moja kunikaribisha kwenda kuoga maji bafuni kwa adabu ambazo mimi nimekuwa nikiziona katika maeneo mengine. Kwa mfano anaweza kuandaa maji bafuni na kuniambia...nyanyuka ukaoge maji yako bafuni...hivi ina maana anshindwa kusema maneno kama karibu mme wangu ukaoge maji yako tayari bafuni? Hata kwa chakua hali ni hiyohiyo.
Kutokana na hili pamoja na mengine nimekuwa nikimchukulia kuwa hana adabu kwa mme wake au nakosea wadau?
Naombeni msaad wenu nifanye ninikumfanya anitendee ninavyopenda kutendewa maana nikimwambia kuwa sifurahii jinsi anavyonifanyia anaonekana kunishangaa tu na kuishia kunilaumu eti labda nina visa vingine tofauti na hilo!
ifanye nini ndugu zangu? naomba mnishauri tafadhali!

umenikumbusha mbali sana mkuu,ushaoga maji yaliyoungwa kwa mdalasini?!pole kwa maswahibu na subiri waje wataalamu kukushauri
 
Mimi nina mke na tuna mtoto mmoja. Lakini tangu nimemuoa huyu mwanamke maka mitatu iliyopita hajawahi hata siku moja kunikaribisha kwenda kuoga maji bafuni kwa adabu ambazo mimi nimekuwa nikiziona katika maeneo mengine. Kwa mfano anaweza kuandaa maji bafuni na kuniambia...nyanyuka ukaoge maji yako bafuni...hivi ina maana anshindwa kusema maneno kama karibu mme wangu ukaoge maji yako tayari bafuni? Hata kwa chakua hali ni hiyohiyo.
Kutokana na hili pamoja na mengine nimekuwa nikimchukulia kuwa hana adabu kwa mme wake au nakosea wadau?
Naombeni msaad wenu nifanye ninikumfanya anitendee ninavyopenda kutendewa maana nikimwambia kuwa sifurahii jinsi anavyonifanyia anaonekana kunishangaa tu na kuishia kunilaumu eti labda nina visa vingine tofauti na hilo!
ifanye nini ndugu zangu? naomba mnishauri tafadhali!

Ukipenda kubembelezwa ujue kubembeleza.
 
nyie ndo mkitafutiwa nyumba ndogo mnakimbilia kwa wagaga kienyeji kunusuru ndoa zenu wakati unaiua ndoa ni wewe mwenyewe kwa mikono yako na kukosa maarifa.MWANAUME KWANGU NI MTOTO WANGU MKUBWA!!!

umenena ukweli mtupu hasa kwenye nyeusi tii hapo! nimefurahia sana,heri mmeo aketiye na kula nyumbani kwako.
 
Sio culture Kongosho, extreme poverty ndugu yangu! Wanaume maskini kazi kweli kweli.
[/B][/SIZE][/COLOR]

hilo nalo neno.....kwanza miaka hii si ya kuweka maji kwenye mndoo bafuni........... Au unaishi ngudu?

Kwa upande wa pili unamtreat vyema mkeo? Au weee unataka upewe mahaba ilhali hutoi mahaba...........
Mkeo kazi anayo
 
Last edited by a moderator:
nimeoa mtu wa manyara....mbulu, mbona dada zake wanaonekana wana heshima? hata kama hayupo wao wakinitengea maji bafuni utasikia wanasema..''shem kaibu maji bafuni'' lakini yeye mwenye mali utasikia anafyatuka ''nyanyuka ukaoge wengine wanataka kuoga utawachelewesha'' basi mi namwangalia simumalizi!

hahaaah....sasa wangoja nini tia nanga kwa akukaribishae .... Dawa ya moto ni moto....

Anyway mtoe out kidogo na akiwa katika mood nzuri mueleze upendayo, kwa upole mambo yatakwenda, ....
 
mimi nipo kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 na mpaka leo nikiweka chakula namkaribisha mume wangu "karibu mpenzi chakula" bafuni kwangu kuna maji siku zote tunaoga pamoja na several times ninamuogesha, namsugua miguu, namkata kucha, namchana nywele, nampasia nguo zake,,hata perfume ni mimi nampulizia...sio mara moja nampelekea chakula ofisini"lunch box" kwa surprise....naingia jikoni several times namuandalia vitu spesho hasa week ends ninapokuwa siendi ofisini... lkn bado alinicheat ...nyie wanaume bana hata mbebwe mgongoni na mbeleko hamriziki......

Tabia za watu wa Pwani, Lakini kutwa kucha Talaka, talaka , talaka. Sipotezi nguvu zangu, bila kuwekeza ndani ya nyumba, hakuna huduma, full stop.
 
Kwa maelezo uliyoyatoa, inaonekana ni wewe ambaye huna nidhamu.
Mkeo amekutayarishia maji moto na amekuwekea tayari bafuni bado unataka akukaribishe,akuombe ukakoge?

Unaomba msaada....Ufanye nini?
Mwoneshe mfano. Kama mara tatu hivi.
Mtayarishie mkeo maji ya kuoga halafu mkaribishe " karibu mke wangu ukaoge maji yako tayari bafuni".
Kwa siku tatu mfululizo, ataelewa somo. Piga moyo konde na tekeleza ushauri. Huwezi amini, atabadilika na utapata hiyo nidhamu uitakayo.

we Nonda unataka mwenzio uanaume wake upungue? Hujui wanaume wanalelewz kama watoto????????
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom