Mke wangu hajawahi kuniambia ananipenda

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,969
1,392
Ebu nishaurini,nina mke ambaye tumeona kama miezi sita hivi imepita..katika hari ya uchumba wetu tulikuwa na mapenzi ya kawaida,si ya moto wala baridi katika kipindi cha miaka minne..

Tulikubaliana tuoane ..lakini katika kipindi chote cha ndoa sijawahi kusikia mke wangu akinitamkia kuwa ananipenda japo tunafanyia mambo mbalimbali kama wanandoa,kila nikimuuliza kwa nini huwa usijawahi ukisema kuwa unanipenda hata siku moja toka tuoane basi huwa ananuna mpaka basi..

Jana nimemwambia siku nikipata mtu anayeniambia ananipenda na kunijari kuliko wewe..utakuja kujuta na huku ukiwa umekwisha chelewa..basi kanununa usiku kucha mpaka naondoka nyumbani..

Nishaulini nichukue hatua gani kwa huyu bibie..
 
Ebu nishaurini,nina mke ambaye tumeona kama miezi sita hivi imepita..katika hari ya uchumba wetu tulikuwa na mapenzi ya kawaida,si ya moto wala baridi katika kipindi cha miaka minne.. Tulikubaliana tuoane ..lakini katika kipindi chote cha ndoa sijawahi kusikia mke wangu akinitamkia kuwa ananipenda japo tunafanyia mambo mbalimbali kama wanandoa,kila nikimuuliza kwa nini huwa usijawahi ukisema kuwa unanipenda hata siku moja toka tuoane basi huwa ananuna mpaka basi.. Jana nimemwambia siku nikipata mtu anayeniambia ananipenda na kunijari kuliko wewe..utakuja kujuta na huku ukiwa umekwisha chelewa..basi kanununa usiku kucha mpaka naondoka nyumbani.. Nishaulini nichukue hatua gani kwa huyu bibie..
unamaneno machafu kwa mkeo, jirekebishe
 
Heri asikwambie anakupenda akakupenda kwa vitendo kuliko kukwambia anakupenda wakati hakupendi. Hivi angekuwa hakupendi ungemuoa au ni yale yale ya kuigizi uzungu? Wazungu huambiana nakupenda kila siku lakini huwa wengi hawakawii kuachana pamoja na kupendana huko kwa maneno.
 
Duuh! Ni maneno makali mno kwa mke..kha! inabd uelewe kuwa kuna wakat matendo huongea zaid kuliko maneno..kama anakukidhia mahitaj yako yote kama mume,neno nakupenda ni dogo saaanaaa...japo inaleta nakshi ktk mahusiano. Unatakiwa uwe Romantik bana.. Hayo maneno makali uliyotumia yatakuwa yamemfanya ahisi kama humuamin..ndo maana ananuna..
 
Kwa lugha nyingine umemwambia mkeo kuwa unatafuta mwanamke mwingine, sasa subiri mkeo apate mwanaume mwingine ndo utaelewa maana ya maneno yako.....

Jana nimemwambia siku nikipata mtu anayeniambia ananipenda na kunijari kuliko wewe..utakuja kujuta na huku ukiwa umekwisha chelewa..basi kanununa usiku kucha mpaka naondoka nyumbani..

Nishaulini nichukue hatua gani kwa huyu bibie..
 
Ebu nishaurini,nina mke ambaye tumeona kama miezi sita hivi imepita..katika hari ya uchumba wetu tulikuwa na mapenzi ya kawaida,si ya moto wala baridi katika kipindi cha miaka minne..

Tulikubaliana tuoane ..lakini katika kipindi chote cha ndoa sijawahi kusikia mke wangu akinitamkia kuwa ananipenda japo tunafanyia mambo mbalimbali kama wanandoa,kila nikimuuliza kwa nini huwa usijawahi ukisema kuwa unanipenda hata siku moja toka tuoane basi huwa ananuna mpaka basi..

Jana nimemwambia siku nikipata mtu anayeniambia ananipenda na kunijari kuliko wewe..utakuja kujuta na huku ukiwa umekwisha chelewa..basi kanununa usiku kucha mpaka naondoka nyumbani..

Nishaulini nichukue hatua gani kwa huyu bibie..

Mnunulie wax, nenda naye kwa fundi kwa surprise akampime na amshonee mtindo autakao kisha nenda naye kula kiti moto (astakafululaaa!) halafu msopsop kwa sana tu siku hiyo ukimpamba kwa maneno ambayo hujawahi kumpa namna anavyopendeza na uzuri alio nao na useme hayo wakati wa faragha (hata kama ni migulubaja wewe sema positive tu). Mwambie umewaona mabinti wengi lakini ukagundua hakuna kama yeye......atasema hata zaidi ya kukuambia anakupenda.
 
katika ndoa upendo ndiyo nguzo kuu je wewe unaupendo wa dhati kwake .unamawasiliano ya karibu kwake yeye ndiye katibu wako kila jambo unamshirikisha mwanaume ndiye kichwa cha nyumba lazima utafute ufmbuzi wa jambo lako utakuja msusa hata mtoto wako
 
Tricky one.
Ila umetumia maneno mabaya sana, na tayari umeshaweka Doa ambalo kulifuta ni vigumu sana moyoni mwake. Hatakaa akuamini kwamwe! Yaani umeweka pilipili kwenye kidonda!

How old are you?

Nafikiri JF kwa kiasi Fulani imekuathiri negatively, chuja sio kila kitu tusenacho ndicho tukofanyacho!
 
Wakati mkiwa wachumba alikua anasema? Kama siyo inawezekana lbd hajazoea yaani hizo kwake si swaga lbd anafanya kwa vitendo na pia kwa hayo maneno uliyomwambia inaleta picha ka haumthani flan hivi au unamnyasasa so lbd ndo maana hasemi, au haijiami(yuko inferior kwako na anajihisi) kwa hiyo anakuogopa!!
 
Jaribu kujiuliza,kwanini unataka kuamini maneno zaidi?Mi nadhani ungeangalia yale anayofanya kwanza!
 
jamii01 that is understatement to your wife.Binafsi umetumia lugha chafu na ya kuonyesha kuwa uko radhi kutoka nje so ni mpango uliokuw umeupanga na hapa unatafuta jinsi ya kutokea tu. ndoa yenyewe miez site ushaanza kuuchokoa mchokoo kweli weye hata first born utalea jamani? badilika wewe wala mkeo hana shida yeyote.
 
Last edited by a moderator:

dada yangu wa moyoni, mbona hujalalamika kuwa sijakwambia nakuloveeeee toka tumekuwa dada's in hearts?? lolest! nakupendajeeee sasa my dada! kha!
 
Umezowea kudanganywa na i love u nyingi za kukuhadaa? Anakupenda huyo.
 
Tricky one.
Ila umetumia maneno mabaya sana, na tayari umeshaweka Doa ambalo kulifuta ni vigumu sana moyoni mwake. Hatakaa akuamini kwamwe! Yaani umeweka pilipili kwenye kidonda!

How old are you?

Nafikiri JF kwa kiasi Fulani imekuathiri negatively, chuja sio kila kitu tusenacho ndicho tukofanyacho!
Hii nimeipenda..kuna watu wanaamini na kuchukua vitu/mambo mengi yanayozungumzwa humu...kibaya zaidi unashauriwa vitu ambavyo hata anaekushauri hajawahi kufanya hivyo. Mawazo ya JF changanya na ya kwako.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom