Mke wangu hajawahi kuniambia ananipenda

Una umri gani? Maana nafikiri wanaopenda maneno ya aina hiyo hata kama ni ya kejeli ni wale teenagers. Kama umeoa ukiwa na umri wa kutosha, sidhani kama utahitaji kusikia maneno hayo, badala yake utaangalia matendo yake kwako na treatments anazokupa kama mke? Yaani wewe unafikia mahali pa kuweka ndoa rehani kisa unataka kusikia neno nakupenda?

lukolo dear, huyu jamaa natamani ningeweza kumuwekea kale kawimbo ' we nidanganye danganye danganye tuuu ...... "
 
muhanga unapenda sana ndogo ndogo?

duh T ulijuaje? duh give me five man!! yaani mie ndogo tu kubwa mwiko.... hayo makubwa kubwa yoote tulicheza wote mbinu zetu zile zile... kwa hiyo nimegundua kwenye ndogondogo kuna mabadiliko najifunza mambo mapyaaa!
 
kaka mi naona labda mapenzi yako yako shallow sana...jaribu kumpa 'vitu adimu' uone kama hatapagawa na kukutamkia 'nakupenda mume wangu..' hadi ukashangaa.....so kaka jaribu kuwa romantic sana mpe mambo mazito atapagawa na utafurahi sana! jaribu tafadhali...
Ebu nishaurini,nina mke ambaye tumeona kama miezi sita hivi imepita..katika hari ya uchumba wetu tulikuwa na mapenzi ya kawaida,si ya moto wala baridi katika kipindi cha miaka minne..

Tulikubaliana tuoane ..lakini katika kipindi chote cha ndoa sijawahi kusikia mke wangu akinitamkia kuwa ananipenda japo tunafanyia mambo mbalimbali kama wanandoa,kila nikimuuliza kwa nini huwa usijawahi ukisema kuwa unanipenda hata siku moja toka tuoane basi huwa ananuna mpaka basi..

Jana nimemwambia siku nikipata mtu anayeniambia ananipenda na kunijari kuliko wewe..utakuja kujuta na huku ukiwa umekwisha chelewa..basi kanununa usiku kucha mpaka naondoka nyumbani..

Nishaulini nichukue hatua gani kwa huyu bibie..
 
Yaani Mtu anafikiri kuwa kila kitu kinachonenwa katika JF kuwa ni sawa au uko sahihi kumbe watu wenyewe ni waongo/ wanafiki maana wengi wanatumia majina yasiyo yao kweli unaweza kuwaamini kweli!! Hapa ni kuwa kama zmbayuwayu tu unachanganya na zako ndo utafanikiwa. Kwenye Neno la Mungu linasema Enyi wanaume wapendeni wake zenu na kuishi nao kwa akili..... sasa ndugu yangu wewe akili zako ziko wapi...... Onyesha ukomavu kwa kumpenda mkeo kwa maneno na vitendo.
 
Back
Top Bottom