Mke wangu hajali familia

Mbona sasa namna unaongea ni kama mtu ambaye hajatoka kwa wazazi wake?!

Coz kuna lugha ungetumia hapo ungewakilisha vema sana wanawake waliopo katika ndoa na wanaijua vema.

Mkuu nimeongea vyema kabisa kama wewe unaona sio vyema ni juu yako sasa, mimi siwajibiki kwenye hilo.

Toka juu nimemshangaa mtoa mada na kutoa ushauri wangu ninaona unafaa, kama wewe unaona comment zangu hazipo kwenye Lugha nzuri hiyo ni wewe.
 
Kwahiyo wewe unaona ni sawa mke Akusaidie majukumu yako halafu wewe usimsaidie ya kwake
Majukumu gani ya kiume ambayo wanaume wanataka mwanamke asaidie na ni wapi na lini wanaume wameweka kampeni ya kuomba kusaidiwa?!

Kwann mabinti wa siku hizi mnapenda ligi kwa mambo ambayo hayana discussion ya kufanya?!

Sasa wewe kama mwanamke unakuwa na faida gani kama haufanyi yale mwanaume anataka ufanye?!
 
Mkuu nimeongea vyema kabisa kama wewe unaona sio vyema ni juu yako sasa, mimi siwajibiki kwenye hilo.

Toka juu nimemshangaa mtoa mada na kutoa ushauri wangu ninaona unafaa, kama wewe unaona comment zangu hazipo kwenye Lugha nzuri hiyo ni wewe.
Hamna bwana. Hapo ni unatafuta kulazimisha kujenga hoja kwa nguvu ya ubishani ila unajua hoja yako ndani yake ni hoja yenye maudhui ya kutest mitambo....

Ngoja nikwambie , mleta mada kama umemuelewa, amelenga kulalamika nini kumhusu mkewe?!
 
Hamna bwana. Hapo ni unatafuta kulazimisha kujenga hoja kwa nguvu ya ubishani ila unajua hoja yako ndani yake ni hoja yenye maudhui ya kutest mitambo....

Ngoja nikwambie , mleta mada kama umemuelewa, amelenga kulalamika nini kumhusu mkewe?!

Bado nasimamia msimamo wangu kama mama wa nyumbani anapaswa kufanya majukumu yote tena mtu mwenye watoto wawili ni rahisi sana kuwajibika.

ila kwa mke anayefanya kazi ni wajibu wake kuhakikisha majukumu ya nyumbani yanafanyika ipasavyo kwa kumueka mdada na kumsimamia, weekend ni zamu ya mke kuwajibika yeye binafsi.

Mkewe hatimizi majukumu kama Mke na Mama.

Mkuu mimi ubishi siuwezi tuishie hapa kila mtu abaki na mtizamo wake.
 
Ila wapo wastaarabu wanajua mke wangu kachoka nae anatakiwa apumzike, Mungu atutunzie kwa kweli Wanaume wa hivi.
Kuchoka ni swala moja hata sisi wanaume kuna muda tunachoka. Ila issue ni kukwepa majukumu yako kwa kisingizio cha kuchoka, unachoka na nini sasa kinachokukeep busy , so wewe katika maisha yako nini muhimu zaidi familia yako au mwili wako kujilaza na kuchoka?!

Kama una mambo ya kufanya na unaona ni muhimu kuliko familia why sasa unakuwa na familia?!

Hivi umesshawahi kuona wale wanaume wanaotelekeza familia na kukimbia kusikojulikana....?!

Sasa hiyo ndio version ya kiume ya hiki unachokiita kuchoka. Unapoona una mwanaume anarudi nyumbani kila siku na kuendelea kuihudumia familia yenu namna bora na pekee ya kumuonyesha umetambua uwepo wake ni kwa wewe kuwa serious na majukumu yako ndani ya nyumba.

Sababu kama yeye hachoki kuwa baba wa familia na mume wako then ni dhahiri kuwa wewe pia hautakiwi hata siku moja kusema unachoka kuwa mke kwake na mama wa familia sababu hayo ndio majukumu yako ya ndoa.

Hakuna sehemu utaambiwa mwalimu bora, muhasibu Bora, dokta bora ni sifa ya mke na mama wa familia. Usichanganye majukumu ya ajira na majukumu ya familia na ndoa.

Wewe kama ulitaka kufanya kazi au biashara that was your choice sasa why ianze kuingilia ndoa na familia yako?!
 
Sasa ubinafsi ni kukutaka ufanye majukumu yako ya kike ndio nakuwa mbinafsi.... Khaaaaaaaaaaaaa ...
Mkuu haujanielewa! Hapa naongelea wale wanawake ambao mnatoka wote asubuhi kwenda kutafuta mkate wa kila siku na mnarudi jioni halafu mwenzio aingie kufanya kazi za ndani peke yake ili hali wewe umekaa sebuleni miguu juu humsaidii!

Hapa siongelei mama wa nyumbani huyo hizo kazi ni lazima afanye maana kwa vyovyote vile lazima mwanamke wa hivyo anamtegemea mume wake kwa kila kitu yaani huyo hadi hela ya chumvi na sabuni anamuomba mumewe yeye hatafuti!

Wengi mnajifanyaga oo mwanamke ni mwanamke tu hata awe na kazi kiasi gani au kachoka vipi majukumu yake lazima ayatimize tu! Ila sote tunaujua ukweli huwezi kumfananisha mwanamke anayekusaidia kutafuta na mama wa nyumbani!

Yaani hawa ni wanawake wawili tofauti kabisa wala haupaswi kuwaweka kundi moja! Kwahiyo ubinafsi wenu unakuja pale mnapotaka wanawake wawasaidie majukumu yenu ila ninyi majukumu yao hamtaki kuwasaidia wakati wote mnachoka!
 
Majukumu gani ya kiume ambayo wanaume wanataka mwanamke asaidie na ni wapi na lini wanaume wameweka kampeni ya kuomba kusaidiwa?..
Hehe kwamba mnajifanya hampendi wanawake zenu wanavyotoka kwenda kutafuta pesa either kwa kufanya kazi au biashara? Si ndiyo ninyi wanaume wa siku hizi mnaosema hampendi wanawake magolikipa dunia imeshabadilika wanawake nao inabidi watoke kujitafutia vya kwao na watoto wakati hilo kwa tamaduni zetu ni jukumu la mwanaume tu?

Sasa hiyo dunia kwanini muibadilishe kwenye majukumu ya mwanaume tu ila ya mwanamke aahh yako pale pale afanye mwenyewe! Yaani watu mnatoka wote asubuhi mnaenda kazini wote mnarudi jioni mmechoka tena pengine mkeo ndiyo anafanya kazi za kuchosha zaidi kuliko wewe ila yeye tena ndiyo aingie jikoni kufanya kila kitu halafu humsaidii!
 
Kuchoka ni swala moja hata sisi wanaume kuna muda tunachoka. Ila issue ni kukwepa majukumu yako kwa kisingizio cha kuchoka, unachoka na nini sasa kinachokukeep busy...
Oohh kwahiyo mkeo akiacha kazi akawa mama wa nyumbani full time utamhudumia kwa kila kitu bila kumtesa na utampa kama kile ambacho alikuwa anakipata huko kwenye kazi au biashara yake?

Hakuna kusema eti utamhudumia kwa kadri ya uwezo wako mhudumie kwa kadri ya mahitaji yake utaweza?
 
Watoto chini ya miaka 5? Ni mapacha hao au umemzalisha kwa fujo bila mpangilio tu?
 
Oohh kwahiyo mkeo akiacha kazi akawa mama wa nyumbani full time utamhudumia kwa kila kitu bila kumtesa na utampa kama kile ambacho alikuwa anakipata huko kwenye kazi au biashara yake?

Hakuna kusema eti utamhudumia kwa kadri ya uwezo wako mhudumie kwa kadri ya mahitaji yake utaweza?
Mtoto wako mwenyewe unaweza kumhudumia kwa kadri ya mahitaji yake? Bila kujali kama mahitaji yatamspoil nk? Hapo ni maswali mawili, la kwanza jibu likiwa ni NDIO basi ndio ujibu na la pili
 
Huyo dawa yake ni kumpeleka kwao na kumkarisha mbele ya wazazi wake na kuwaeleza hayo yote kwa pamoja ili awatie aibu. Baada ya hapo waombe umuache hapo walau kwa mwezi mmoja ili apigwe msasa walai nakwambia akirudi si yeye atabadilika. Lakini kingine mkeo unatakiwa sometime umweke makofi mawili matatu ili kumkumbusha kuwa wewe upo na alijue hilo akuheshimu pale unapomwelekeza jambo.
 
Habari wana JF!

Ebu wadau naombeni ushauri wenu. Nina mke na watoto wawili. Mke wangu ana changamoto moja hataki kupika na pia hajali watoto. Yaani tunaweza kukaa siku mbili tatu tunakula mikate na chai tu. Na yeye ni mama wa nyumbani sio kwamba ana shughuli kivile za kumkwamisha yeye kupika HAPANA.

Nikimwambia kwanini hapiki anadai sijaenda sokoni kununua vitu (asa nawaza si yeye ni jukumu lake kwenda sokoni) maana pesa za biashara tunazofanya ni yeye anashika kwahiyo sio kwamba haendi kwasababu hana pesa.

Kuhusu watoto ndio kabisa hawalishi wala hawaogeshi, na watoto ni wadogo chini ya miaka 5. Yaani watoto wasipojipambania wenyewe kula ndio basi hawali.

Kuna saa nakasirika kinoma lakini nakosa namna. NIFANYEJE
Mkeo anafanya kazi gani? Amesoma? Je, anatoka familia yenye uchumi gani?

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Tafta msaidizi wa ndani(housegirl au babysitter) alaf yeye umfukuze arudi kwao.
 
Mtoto wako mwenyewe unaweza kumhudumia kwa kadri ya mahitaji yake? Bila kujali kama mahitaji yatamspoil nk? Hapo ni maswali mawili, la kwanza jibu likiwa ni NDIO basi ndio ujibu na la pili
Mkuu mtoto hana uwezo wa kujitafutia pesa zake mwenyewe! Mwanamke anao uwezo wa kujitafutia sasa unapomkataza asitafute ili eti atimize majukumu yake kikamilifu basi na wewe uhakikishe unao uwezo wa kutimiza majukumu yako kikamilifu!
 
Huyo anayeshindwa kujali hata Watoto hafai kabisa, Watoto chini ya miaka mitano wanajipambania vipi kupata Chakula?
 
Back
Top Bottom