Mke wangu anatuma post za kunisimanga Facebook

Mke wangu anatuma post za kunisimanga Facebook

Hii mitandao ya kijamii inavuruga sana ndoa/mahusiano,wengi wanaitumia visivyo.
 
Kaota mapembe, basi achwe aende kwa wenye mapembe wenzie..tulia utampata kipara mwenzio...
I know It's hard but also its better.
 
kaka pole sana, ila naamini kuna kitu zaidi ya hiyo....humu duniani pesa na wanawake ndo kinachotuhangaisha wanaume, mmeshazaa? how many kids? fikiria zaidi wanao, huyo mdisable...uwe na roho ngumu kuchukua maamuzi magumu, maisha lazima yasonge.
 
Mkuu Elli nawe acha upole huo bwana! Yaani mtu anachukia mie kupeleka kwa mama huko Shambalai shs laki tatu halafu nimtumie ujumbe wa kumsifia? Aah wapi labda uniambie nimtumie ujumbe kuwa nimeongeza kiwango kuwa laki tano.

Basi nakubaliana na wewe Mpwa wangu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakushangaa sana, "Mwanamke ambaye hataki nimtumie mama yangu pesa" huyo ni wa kuachana naye haraka sana, akiona husikii, jiandae kuwekwa kiganjani.
 
ahahahahaaa....nimecheka na hiyo mipasho.....anyway. hivi na wewe ukimjibu kupitia ule wimbo wa christian bella wa nani kama mama unadhani hawezi kukuelewa?...haya lets saya haelewi kiswahili...mjibu basi kwa ule wimbo wa tupac wa dear mama....na kama haelewi hip hop ngumu mjibu tuu hata kwa wimbo wa boyz II men wa mama ataelewa tuu.
asipoelewa mrudishe kwa wazazi wake.

aisee umenikumbusha mbali kidogo...mie naye aliwahigi kuleta query kwanini namsaidia mkwewe sana kuliko wakwe zangu ....nilimjibu jibu moja tuu. muambie mungu amuite mshua wako mbele za haki ili nitoe mgao sawa maana huyu mama angu mjane wewe bado wapo wote....aliufyataaaaaaa mpaka leo akiniona anajiulizaga anianzie wapi unyayoni au utosini.

in short it takes two stupid minds to make up a serious story....akiwa chizi wewe kuwa chizi zaidi yake atakuelewa tuu. la sivyo jiandae kupandiliwa kichwani mpaka siku akuambie kwanini umenunua boxer yako hujamnunulia baba angu kijijini.

arghhhhhhhhhh...2015 i do care.
 
Umejaribu kumuhakikishia kwamba kweli hizo laki 3 zinaenda kwa mama Kijijini??? Maana huenda akawa anahisi unatuma kwa Kimada na sio Mama.
 
Very






sad,amekuwa akiweka ujumbe wa ajabu ajabu kwenye wall yake ya Facebook,
na sasa hii ndio profile picture yake.
Hii amenza kufanya kama miezi miwili na nusu nyuma, na mbaya zaidi ni
kwamba yeye ni mlokole na amehama Kanisa letu lilotulea na kuhamia
kwenye makanisa ya miujiza.

Yeye yuko very demanding, ukimwambia mshahara hautoshi, kwake ni maneno,
nimejaribu kufungua biashara na yeye ndiyo msimamizi mkuu.Bado faida
haionekani licha ya kuwa sichukui chochote toka kwenye biashara hizo.

Analalamila kisa eti kila mwezi namtumia mama kijijini laki 3, what is
laki tatu by the way ni sawa na elfu kumi kwa siku.
ukimuelewesha haelewi, anataka mama yake nimtumie laki tano,mpaka sasa
nahisi amegeuka kero na mzigo.

Sina mengi, ila namshukuru Mungu kwa yote.

10927928_359236227594237_347315041_n.jpg








maskini si kwanza amshukuru mungu kwa huyo mama kumzalia mme?

ivi anajua maana ya mama?
je anajua huyo mama alikusomesha kwa sh ngap?

yaan mama yake apewe laki 5 mama yako na iyo tatu unayompa analalamika?

je yeye angekuwa ndo mme angefanya ivo kwa mama yake?

hii ni kuigiza ukichaa. mtu unakula unakunywa shida yako nn?

anyway, wanasema "you don know wat u have until u loose it"

ebu kaongee nae uone anasemaje wenda kuna jingine ndani ya kapeti.
 
Tatizo la haya makanisa yetu kuna watu wanasahau hadi wajibu wao katika nyumba zao kama mama au baba mtu anachukua hadi school fees ya mtoto anapeleka kanisanu eti unatakiwa kutoa kitu kinachokugusa moyoni inawezekana huyo mkeo anapeleka pesa huko
Ni vyema kukaa nae chini na kuongea mwambie hii ni mara ya mwisho unahitaji abadalike na aone kipi ni bora kwake ndoa au kanisa
Maana democracy ikizidi mahali popote sio nzuri diktetaship itumike muda mwingine :angry:
 
She is deeply depressed, chukua hatua mapema kamanda.
Kaa naye chini mueleze umuhimu na wajibu ulio nao kwa wazazi wako.
 
kaanza kutanga na makanisa ya manabiiii .... mpuuzi huyo sasa mpige marufuku kwenda kwenye hayo makanisa au aache ndoa .. faida anapelekewa mchungaji .... kingine kama umnyanyasi anza sasa kumnyanyasa

huyu mwanamke yukoje? acheni kumshobokea coment zake za maudhi sana
 
mmmmmh.....ndoa yataka uvumilivu na maombi
she dont know ur value pole sana

peaneni space pata holiday safar itasaidia

jitahid sana kumuombea hilo pepo la roho ya kaksi uchoyo na pia haya makanisa ya miujiza hajitambui huyu
 
Cha kufanya jidai kama hujaziona hizo mbwembwe taarabu zake na uishi kama hamna tatizo na kama kuna malove mawili matatu ulikua unamrusha nayo unayaondoa bila kuuliza au kuruhusu muda wa kuulizwa baada ya muda akishaipata fresh atarudi kujiuliza kunani hapo ndio unamkumbusha miiko ya ndoa.
 
huyu mwanamke yukoje? acheni kumshobokea coment zake za maudhi sana

mrembo /handsome acha kuwa mkorofi nakuangalia mda tu naona unatoka povu nini shida mtoto mzuri eeeeh... haya maisha tu lazima yaende ..:A S kiss:
 
mmmmmh.....ndoa yataka uvumilivu na maombi
she dont know ur value pole sana

peaneni space pata holiday safar itasaidia

jitahid sana kumuombea hilo pepo la roho ya kaksi uchoyo na pia haya makanisa ya miujiza hajitambui huyu

mtumishi kamshika ... biashara anafunga anaenda kuomba
 
Tatizo la haya makanisa yetu kuna watu wanasahau hadi wajibu wao katika nyumba zao kama mama au baba mtu anachukua hadi school fees ya mtoto anapeleka kanisanu eti unatakiwa kutoa kitu kinachokugusa moyoni inawezekana huyo mkeo anapeleka pesa huko
Ni vyema kukaa nae chini na kuongea mwambie hii ni mara ya mwisho unahitaji abadalike na aone kipi ni bora kwake ndoa au kanisa
Maana democracy ikizidi mahali popote sio nzuri diktetaship itumike muda mwingine :angry:

tena udikiteta wa mjerumani aache ujinga huyu mwanamke
 
Umejaribu kumuhakikishia kwamba kweli hizo laki 3 zinaenda kwa mama Kijijini??? Maana huenda akawa anahisi unatuma kwa Kimada na sio Mama.

kuna haja gani ya kuhakikisha?? kapewa biashara anapeleka kanisani mtaji ... badala atafute faida atume laki 5 kwa mama yake anaenda kuimba injili fake kwa nabiiii,... atafute hela na yeye haonge hapa ndipo mnapoenda mbali na ndoa kutushinda vyako vikienda sawa hakuna haja ya kujua vya wengine vinaendaje
 
Back
Top Bottom