Mke wangu anataka kurudi kwao

Mke wangu anataka kurudi kwao

Acha uongo wako unachezea dini za watu sio vizuri ,kwanini usiandike kitu cha maana kuliko kukaa kwenye keyboard nakutunga ujinga kama huu
yesuu kumbe katunga ?

basi leo atakuwa hana wateja kwenye kanisalake la kiroho
 
Muombe bwana maana ni muweza wa yote.
Mchungaji kulialia sio vizuri maana ninyi ndio mnatuhubiria kuwa bwana yesu anaweza yote.
Mchungaji kulialia kunaleta mwangwi wa kwamba kile mnachotuhubiria sio kweli.
 
Unatakiwa ufunge na kuomba siku 90,mungu akusamehe ujinga wako.hivi ata aibu hauoni?!
 
Wewe naye unaitwa nabii nani maaana mpo wengi kweli...hivi hauoni aibu kuleta upuuzi kama huu hapa jukwaani.
 
unahitaji toba umpokee Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako .huu ndo ushauri wangu kwako
 
Hivi haya makanisa ya kijanjajanja yashaanza kulipa kodi kweli?
 
Mme mchungaji kondoo
Mke mchungaji kondoo
Then wakashindwa kujichunga wao.... Daa hii dunia bana ina vituko....
 
sij
Wadau shalom

Bwana asifiwe

Mwaka 2014 mke wangu aliingiwa na tamaa yeye na wenzie wakajitenga na kanisa wakaenda kufungua huduma yao mahala pengine, hawakua na eneo hivyo wakawa wanatumia darasa la Shule ya msingi hadi sasa wako humo, aliendelea kuishi na mm kwa miezi kama 2 hivi baadae akabeba kila chake akaondoka

Baada ya mwaka Bwana akawa amenifunulia nichukue mdogo wake ambae yeye hakuhama kanisa kumfuata dada yake, basi tangu mwaka Jana mwezi may tunaishi pamoja na huyu mdogo wake Kutokana na MUNGU kutufunulia hivyo katika maono, kukawa na kama mgogoro hivi maana ukoo wao wote waliamia kule kwa mke wangu wa awali pamoja na wakwe zangu wanaabudu huko sasa hivi,

Hivi karibuni mke wangu mpya anadai amechoka na ugomvi na amechukiwa na wazazi wake kwa sababu amebaki kwangu sasa ameona hawezi kuendelea hivi, hivyo yeye ameona arudi ahamie kwa dada yake Ingawa ana mimba yangu kubwa tu, anasema ameona akapatane na dada yake akaenda kuomba msamaha , hawawezi kuishi kwa uhasama, hivyo akawa ameondoka mwanzo wa hii wiki,
Nikawa nimeomba kikao nao wote kujua hatma ya watoto wangu wawili na huyo ambae hajazaliwa, wamenijibu hovyo sana kwamba Sina changu, ila huyu mjamzito inaonekana yy anasukumwa tu bado ananipenda

Hata Kuna wakati nilisingiziwa kutembea na mke wa muumini wangu kumbe ni yule aliekua mke wangu aliehama kanisa ndie pamoja na wenzie wachache ndio walitengeneza Mpango ule ili niondolewe kama mchungaji mkuu iliposhindikana ndipo wakaenda kuanzisha huduma yao, lakini MUNGU akanipigania bado huduma yangu ndio kubwa wao bado wanasali kwenye darasa, sasa wameamua wamrubuni huyu binti (mke wangu wa sasa) na wamemtoa wanae huko wanadai watamtenga hivyo akaogopa, ila kwa kweli mm nampenda sana, tangu ameondoka jumatatu naumwa homa kali sana, sijatoka hata ndani, sikua najua nampenda huyu binti kiasi hiki alivyoondoka juzi

Sasa watu wa MUNGU sijui mnanishauri nifanyeje, niweze kupata haki yangu bila kudhuru image ya kanisa letu, na huyu binti nifanyeje aweze kurudi maana hata kula imekua shida kwangu,
Sasa hivi wamenibadilishia kibao wanadai nimemsaliti ndoa kwa kuchukua mdogo wa mke wangu wakati yeye ndie alikimbia nyumba
sijia kama unajua unachokiandika
 
Back
Top Bottom