Mke wangu anataka kurudi kwao

Mke wangu anataka kurudi kwao

bwana Asifiwe sana (sio Bwana)
Ushauri wangu, Kama wana Mdogo wao wa kike mwingine vuta piga mimba. Halafu unipe address yako nije kusali kanisani kwako manake huko Mstari wa 'naye anayemuoa alieachika anazini nae' hauhusiki kabisa.
Wadau shalom

Bwana asifiwe

Mwaka 2014 mke wangu aliingiwa na tamaa yeye na wenzie wakajitenga na kanisa wakaenda kufungua huduma yao mahala pengine, hawakua na eneo hivyo wakawa wanatumia darasa la Shule ya msingi hadi sasa wako humo, aliendelea kuishi na mm kwa miezi kama 2 hivi baadae akabeba kila chake akaondoka

Baada ya mwaka Bwana akawa amenifunulia nichukue mdogo wake ambae yeye hakuhama kanisa kumfuata dada yake, basi tangu mwaka Jana mwezi may tunaishi pamoja na huyu mdogo wake Kutokana na MUNGU kutufunulia hivyo katika maono, kukawa na kama mgogoro hivi maana ukoo wao wote waliamia kule kwa mke wangu wa awali pamoja na wakwe zangu wanaabudu huko sasa hivi,

Hivi karibuni mke wangu mpya anadai amechoka na ugomvi na amechukiwa na wazazi wake kwa sababu amebaki kwangu sasa ameona hawezi kuendelea hivi, hivyo yeye ameona arudi ahamie kwa dada yake Ingawa ana mimba yangu kubwa tu, anasema ameona akapatane na dada yake akaenda kuomba msamaha , hawawezi kuishi kwa uhasama, hivyo akawa ameondoka mwanzo wa hii wiki,
Nikawa nimeomba kikao nao wote kujua hatma ya watoto wangu wawili na huyo ambae hajazaliwa, wamenijibu hovyo sana kwamba Sina changu, ila huyu mjamzito inaonekana yy anasukumwa tu bado ananipenda

Hata Kuna wakati nilisingiziwa kutembea na mke wa muumini wangu kumbe ni yule aliekua mke wangu aliehama kanisa ndie pamoja na wenzie wachache ndio walitengeneza Mpango ule ili niondolewe kama mchungaji mkuu iliposhindikana ndipo wakaenda kuanzisha huduma yao, lakini MUNGU akanipigania bado huduma yangu ndio kubwa wao bado wanasali kwenye darasa, sasa wameamua wamrubuni huyu binti (mke wangu wa sasa) na wamemtoa wanae huko wanadai watamtenga hivyo akaogopa, ila kwa kweli mm nampenda sana, tangu ameondoka jumatatu naumwa homa kali sana, sijatoka hata ndani, sikua najua nampenda huyu binti kiasi hiki alivyoondoka juzi

Sasa watu wa MUNGU sijui mnanishauri nifanyeje, niweze kupata haki yangu bila kudhuru image ya kanisa letu, na huyu binti nifanyeje aweze kurudi maana hata kula imekua shida kwangu,
Sasa hivi wamenibadilishia kibao wanadai nimemsaliti ndoa kwa kuchukua mdogo wa mke wangu wakati yeye ndie alikimbia nyumba
 
unaitwa pastor masumbuko duuu una mtihani yani mungu amekupa ufunuo kweli naamini kuna mungu wa wanadamu wote na mungu wa masumbuko hata kama mkeo wa kwanza kaondoka mwenyewe sio kumzini mdogo wake na mimba juu na wote wana watoto na wewe na ndoa za kikrsto hazina talaka duu kweli unawaongoza nyumbuz
 
Umenena vyema mkuu.Kwa sababu inaonekana Mchungaji huwa anapata maono kabla ya kufanya maamuzi kwa sababu hata mke wake alivyokimbia hakuja kutuomba ushauri bali alipata tu maono kutoka huko kwa Lusifa kuwa amchukue huyo mdogo wa mke wake. Kwa hili bora atulie tu ili maono yaje tena huenda yakamshauri kitu kizuri zaidi.
HHAHAHAHAHAHAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Bwana Yesu asifiwe! Mtu wa mungu nakushauri urudi tena kwenye maombi ya nguvu huenda mungu akakufunulia tena mdogo wao mwingine!.......Na huenda mungu akakufunulia wadogo zake wote hadi uzae nao wote
HAAHAHAAHAHAHAA CHEKA SANAAAA
 
Wachungaji wa kweli hawapo kama wewe acha kumkebehi mungu Masumbuko na usipojiangalia utasumbuka kwelikweli.
 
Wewe ni mzinzi tu kama walinzi wengine; unamtukanisha Kristo. Futa neno Pastor kwenye jina lako. Hakuna mwanadamu yeyote achilia mbali mzinzi mwenye huduma labda kama hiyo huduma ni ya lucifer. Nitawashangaa sana wizards ya mambo ya ndani wasipokutafuta ili wakufungie honcho unachoita huduma. Hats hiyo Mungu akurehemu
 
Acha uongo wako unachezea dini za watu sio vizuri ,kwanini usiandike kitu cha maana kuliko kukaa kwenye keyboard nakutunga ujinga kama huu
Mungu anamuona kile afanyacho kua sio sahihi maana hapa anafanyia dhihaka dini za watu..... Mungu na atete nae
 
Kwanza pia ukae ukijua sio mungu aliekufunulia kua mdogo wa mke wako anafaa ila ni tamaa zako ndo zilikuonyesha kua anakufaa.... Na kama ni kwely wewe in mchungaji basi ujue nyinyi ndo wale wachungaji wa uongo na wala kwely haimo ndani yenu
 
unaitwa pastor masumbuko duuu una mtihani yani mungu amekupa ufunuo kweli naamini kuna mungu wa wanadamu wote na mungu wa masumbuko hata kama mkeo wa kwanza kaondoka mwenyewe sio kumzini mdogo wake na mimba juu na wote wana watoto na wewe na ndoa za kikrsto hazina talaka duu kweli unawaongoza nyumbuz

Usimsikilize huyo bangi mtu! Mungu wake kichwa chake kilichopo kwenye suruali yake! Shameless man
 
tangu ameondoka jumatatu naumwa homa kali sana, sijatoka hata ndani, sikua najua nampenda huyu binti kiasi hiki alivyoondoka juzi

Laiti huyo Israili angekutia rungu uishie uachane na kulidhalilisha kanisa na visa vyako vya kijinga
 
Wadau shalom

Bwana asifiwe

Mwaka 2014 mke wangu aliingiwa na tamaa yeye na wenzie wakajitenga na kanisa wakaenda kufungua huduma yao mahala pengine, hawakua na eneo hivyo wakawa wanatumia darasa la Shule ya msingi hadi sasa wako humo, aliendelea kuishi na mm kwa miezi kama 2 hivi baadae akabeba kila chake akaondoka

Baada ya mwaka Bwana akawa amenifunulia nichukue mdogo wake ambae yeye hakuhama kanisa kumfuata dada yake, basi tangu mwaka Jana mwezi may tunaishi pamoja na huyu mdogo wake Kutokana na MUNGU kutufunulia hivyo katika maono, kukawa na kama mgogoro hivi maana ukoo wao wote waliamia kule kwa mke wangu wa awali pamoja na wakwe zangu wanaabudu huko sasa hivi,

Hivi karibuni mke wangu mpya anadai amechoka na ugomvi na amechukiwa na wazazi wake kwa sababu amebaki kwangu sasa ameona hawezi kuendelea hivi, hivyo yeye ameona arudi ahamie kwa dada yake Ingawa ana mimba yangu kubwa tu, anasema ameona akapatane na dada yake akaenda kuomba msamaha , hawawezi kuishi kwa uhasama, hivyo akawa ameondoka mwanzo wa hii wiki,
Nikawa nimeomba kikao nao wote kujua hatma ya watoto wangu wawili na huyo ambae hajazaliwa, wamenijibu hovyo sana kwamba Sina changu, ila huyu mjamzito inaonekana yy anasukumwa tu bado ananipenda

Hata Kuna wakati nilisingiziwa kutembea na mke wa muumini wangu kumbe ni yule aliekua mke wangu aliehama kanisa ndie pamoja na wenzie wachache ndio walitengeneza Mpango ule ili niondolewe kama mchungaji mkuu iliposhindikana ndipo wakaenda kuanzisha huduma yao, lakini MUNGU akanipigania bado huduma yangu ndio kubwa wao bado wanasali kwenye darasa, sasa wameamua wamrubuni huyu binti (mke wangu wa sasa) na wamemtoa wanae huko wanadai watamtenga hivyo akaogopa, ila kwa kweli mm nampenda sana, tangu ameondoka jumatatu naumwa homa kali sana, sijatoka hata ndani, sikua najua nampenda huyu binti kiasi hiki alivyoondoka juzi

Sasa watu wa MUNGU sijui mnanishauri nifanyeje, niweze kupata haki yangu bila kudhuru image ya kanisa letu, na huyu binti nifanyeje aweze kurudi maana hata kula imekua shida kwangu,
Sasa hivi wamenibadilishia kibao wanadai nimemsaliti ndoa kwa kuchukua mdogo wa mke wangu wakati yeye ndie alikimbia nyumba
Kamchukue dadaako uishi nae huyo hataondoka kwa kuwa hata akikimbia atakimbilia kwenu, kunguru we
 
Kitabu cha mithali 6;32 imeandikwa;- mtu aziniye na mwanamke hana akiri kabisa afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi yake. hivyo kwa mjibu wa neno hili naweza kuamini kuwa hazikutoshi vizuri.
 
kwanini wewe hujioni km ni mkosaji? unajipamba sifa nzuri kuliko wao? by the way we ni nabii wa uongo mwenye unafki kwa YESU. jishushe ukatubu jalala lako la dhambi liondolewe pamoja na kujikweza.
 
Back
Top Bottom