Mke wangu ananipiga makofi kila ninapochelewa kurudi nyumbani, nifanyaje jamani nimechoka!

Mimi ni mwanaume niliejaaliwa kuwa na watoto wawili wakike na wa kiume na mke wangu nimemuoa miaka kumi iliyopita huko mkoani iringa, shughuli zangu ni fundi seremala katika hizi kampuni za ujenzi za kichina zilizotapakaa hapa jijini dar ambazo tunajenga nyumba mbalimbali za miradi ya jamii.

Sasa mara nyingi pesa huwa tunalipwa kwa kila wiki, sasa hapa kati huwa napigika sana yaani nakuwa sina pesa hivyo ni lazima nijiongeze kwa kufanya kazi za ziada pindi ninapotoka kazini ile saa kumi, sasa najikuta nakuwa huko mitaani mpaka saa mbili au saa tatu usiku ndipo namaliza kazi zangu za ziada na kupata pesa then naelekea home.

Lakini ninapofika nyumbani nakumgongea mke wangu anifungulie mlango nikiingia ndani tu maneno yanaanza, nikimjibu kuwa nilipitia sehemu kufanya kazi maana nimerudi kazini nikiwa sina pesa naambulia vibao usoni napigwa mpaka nalia ndugu zangu huku nikiambiwa na mke wangu...usinijibu mimi nakwambia...roho inaniuma sana ndugu zangu naomba mnishauri nifanye nini ili kuepukana na vipigo hivi mimi jamani?.
Mwambie asiwe anafanya hivyo, mtafutie bakora nzuri ya mpera umpelekee awe anatumia kukuchapia.Mwanaume kupigwa vibao na mkewe kumepitwa na wakati ndugu yangu,bakora ndo sahihi zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh, pole mkuu, sasa umeshajaribu kumrudishia kipigo? Maana hapo hakuna raha ni karaha tu. Kaa naye chini muongee, kama hawezi kuacha kukufanya wewe ndio "punching bag" lake, basi itabidi uamue mwenyewe, kuendelea kudundwa, kuzichapa naye au kila mmoja wenu achukue hamsini zake. Kumbuleni pia wakati anakudunda/kulimba, watoto wanasikia na kuona yote yanayojiri, hii si nzuri kwa afya zao za akili.
 
hapo sasa nani kamuoa mwenzie? mbona unatia mashaka....... sina uhakika kama story yako ni ya kweli au ya kutengeneza maana ....mhhhh, wewe ndo unaeishi nae na wewe ndo mwathirika wa kupigwa mpaka unalia so unahitaji kufanya maamuzi, mwanamke anapokuwa mkorofi kiasi hicho nadhani sio mke mwema aliyekupangia Mungu, lazima atakuwepo wa kwako sehemu so ni kuachana nae tu maana unatafuta kwa faida yenu wote halafu ukirudi unapigwa mpaka unalia na mkeo?????
 
Wewe hujaoa, ila umeolewa. Ni mpaka ubadilishe hilo kwanza ndo mambo yakae sawa.
Pili, kuna kosa ulifanya wakati unataka kuoa.. sitaki kulifafanua sana kwa sasa maana hata nikikuambia haitasaidia.
Maana umeshachelewa. Ndo unaambiwa kosea kujenga nyumba ila usikosee kuoa.
Hilo ni janga lako, jua liwake, mvua inyeshe, ije baridi ije joto, pambana
 
Yaan hapa nina hasira hivi wewe mwanaume gani wa kupigwa na mwanamke?yaan natamani ningekuwa mm ili nimuonenyeshe show
 
Mtu alishamalizwa mapema tu hapo.
Kinachofuata ni kufuata tu mwanamke anavosema kichwa chini tu kama kondoo
Kipigo lazima achezee tu. Ila ipo siku akili ukikurudia utamfanyia maajabu huyo mwanamke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mwanaume niliejaaliwa kuwa na watoto wawili wakike na wa kiume na mke wangu nimemuoa miaka kumi iliyopita huko mkoani iringa, shughuli zangu ni fundi seremala katika hizi kampuni za ujenzi za kichina zilizotapakaa hapa jijini dar ambazo tunajenga nyumba mbalimbali za miradi ya jamii.

Sasa mara nyingi pesa huwa tunalipwa kwa kila wiki, sasa hapa kati huwa napigika sana yaani nakuwa sina pesa hivyo ni lazima nijiongeze kwa kufanya kazi za ziada pindi ninapotoka kazini ile saa kumi, sasa najikuta nakuwa huko mitaani mpaka saa mbili au saa tatu usiku ndipo namaliza kazi zangu za ziada na kupata pesa then naelekea home.

Lakini ninapofika nyumbani nakumgongea mke wangu anifungulie mlango nikiingia ndani tu maneno yanaanza, nikimjibu kuwa nilipitia sehemu kufanya kazi maana nimerudi kazini nikiwa sina pesa naambulia vibao usoni napigwa mpaka nalia ndugu zangu huku nikiambiwa na mke wangu...usinijibu mimi nakwambia...roho inaniuma sana ndugu zangu naomba mnishauri nifanye nini ili kuepukana na vipigo hivi mimi jamani?.
Wewe mzima kweli?
 
Hivi bado unatembezewa m, mkong'onto? Mpe katoto kengine ili awe busy sana
 
Back
Top Bottom