Mke wangu ananipiga makofi kila ninapochelewa kurudi nyumbani, nifanyaje jamani nimechoka!.

Dec 7, 2017
42
95
Mimi ni mwanaume niliejaaliwa kuwa na watoto wawili wakike na wa kiume na mke wangu nimemuoa miaka kumi iliyopita huko mkoani iringa, shughuli zangu ni fundi seremala katika hizi kampuni za ujenzi za kichina zilizotapakaa hapa jijini dar ambazo tunajenga nyumba mbalimbali za miradi ya jamii.

Sasa mara nyingi pesa huwa tunalipwa kwa kila wiki, sasa hapa kati huwa napigika sana yaani nakuwa sina pesa hivyo ni lazima nijiongeze kwa kufanya kazi za ziada pindi ninapotoka kazini ile saa kumi, sasa najikuta nakuwa huko mitaani mpaka saa mbili au saa tatu usiku ndipo namaliza kazi zangu za ziada na kupata pesa then naelekea home.

Lakini ninapofika nyumbani nakumgongea mke wangu anifungulie mlango nikiingia ndani tu maneno yanaanza, nikimjibu kuwa nilipitia sehemu kufanya kazi maana nimerudi kazini nikiwa sina pesa naambulia vibao usoni napigwa mpaka nalia ndugu zangu huku nikiambiwa na mke wangu...usinijibu mimi nakwambia...roho inaniuma sana ndugu zangu naomba mnishauri nifanye nini ili kuepukana na vipigo hivi mimi jamani?.
 
Mima white cute

JF-Expert Member
Nov 24, 2017
740
1,000

Ww unajitetea tu si useme ukitoka unapitia bar na kwa machangudoa tu....huyo mkeo aongeze jitihada akutandike has a hadi unyooke
 
Hunyu

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
4,785
2,000
Kumshauri mwanaume kama wewe ni ngumu sana kwasababu inaonekana huna nguvu katika familia yako hasa kiuchumi. Lakini pia huko mwanzo inaonekana kuna vitu ulikisea ukampa nafasi kubwa ya maamuzi mkeo.

Kaa chini ufikirie kama ungemweleza Baba yako uliyoyaandika hapa angejisiaje. Unamapungufu mengi sana Brother kama mwanaume, unless ni story ya kutunga.
 
sukuma boy

New Member
Nov 9, 2017
3
45
Mkabidhi hela ya wiki then mwambie asikuombe hela tena ndani ya hiyo wiki Ila ubaki na nauli ili wiki nzima usifanye kazi za ziada na uwahi kurudi tu home. Isipo tosha mwambie ndo maana mm naitwa baba nakojoa nimesima wewe unachuchumaa.
 
bioto

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
1,198
2,000
umenisikitisha aisee
badilika bana dem ataanzaje kukupiga wewe mwanaume kamili?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom