Mke wangu ananipa mashaka

zipumbovu

Member
Joined
Nov 27, 2023
Posts
24
Reaction score
392
Ninahisi mke wangu ni aina ya wanawake ambao upo nae kwenye ndoa lakini na yeye anajenga nyumba yake kwa Siri

Niliwahi kumwambia kwamba tufungue biashara na yeye ndie aisimamie biashara yetu lakini alikataa na kusema kwamba anataka nimfungulie biashara yake mwenyewe na sio ya familia yaani nimuwezeshe ili awe na biashara yake yeye ( sio ya familia )

Nikazuga zuga na sikufungua biashara Wala kumfungulia yeye, sasa kwa sasa anaonekana yuko serious sana ananihimiza nimpatie pesa afungue biashara yake binafsi.

Kwenye stori zetu na kusukuka siku amekuwa akitamka kauli kama nikiwa na pesa ntafanya mambo mamkubwa mala nitaitafuta pesa yangu kweli kweli

Siku moja nikasema unataka kutafuta pesa ili tusongeshe vizuri familia au unajitafutia wewe mwenyewe , akasema zitakuwa pesa zangu Mimi ila vitu vidogo vidogo nitakuwa nakusaidia

Sasa wakuu huyu mwanamke hana hata 100 mbovu na hataki biashara ya familia anataka biashara yake binafsi na anataka mtaji utoke kwangu Mimi , nafikilia kuingia mitini tuu
 
Hao ndio wanawake, The Good point ni kua Umeshajua nia yake ya Ubinafsi.

Sasa We endelea na Wazo lako la kufungua biashara Yako, Kama atataka kuajiliwa hapo sawa, kama hataki weka wasimamizi wengine.

Kuhusu biashara yakwake, Angalia kwanza kipato chako, kama kinaruhusu mchangie kama na wewe una unga unga Weka kwanza mambo yako sawa.
 
Kuhusu biashara yakwake, Angalia kwanza kipato chako, kama kinaruhusu mchangie kama na wewe una unga unga Weka kwanza mambo yako sawa.
Hii option haitakiwi kutekelezwa, huo mtaji uwe wa kufungua biashara ya familia, mke wako anakuwaje na biashara yake kwaajili yake ila kwa mtaji wako? Unajua matokeo ya kufanya hivy
 
Hii option haitakiwi kutekelezwa, huo mtaji uwe wa kufungua biashara ya familia, mke wako anakuwaje na biashara yake kwaajili yake ila kwa mtaji wako? Unajua matokeo ya kufanya hivy

Mkuu kama hela zipo hakuna shida, Wakati mwingine ni kumpa kile anacho kutaka.

Mbaya ni pale ambapo Mwanaume hana hela ni Unga unga, Anakopa au kudunduliza ili amfungulue mke biashara iwe yake tu
 
Mkuu umeoa mwanamke wa mtu.

Ukioa au ukiwa na mwanamke wako wewe utashangaa jinsi anakihurumia kila jambo unalofanya anatanguliza huruma na discipline.

Nimepitia Nyuzi zake kazaa.
Nimesikitika sana, He is A good Guy.

Japo Ndo hivo Mwanamke anataka kufunzwa na Ulimwengu.

Na ni kweli Hii ndoa haina maisha marefu
 
Hakuna mke hapo. Kama hamna watoto, kimbia mbio usije pigwa na kitu kizito.

Shemeji yetu naona yuko tayari kukuua, uza, saliti ili tu apate pesa zake mwenyewe. Siku ukiwa na hiyo biashara yako mwenyewe, atakuua ili iwe mali yake. Kichwani mwake na katika mipango yake hakuna neno familia wala chetu isipokuwa mimi na changu tu.
 
#KATAA NDOA
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…