Mke wangu ananifanyia vituko ili tuachane

Katika maisha ya ndoa ,misuko suko mingi iko katika umri wa ujana miaka 30-45.omba Mungu upite salama ktk miaka hiyo kwani vishawishi ni vingi.baada ya muda huo mapenzi yataanza kurudi upyaa na ndio mpaka uzeeni.zaidi ya sms ushawahi kumkuta labda anapigwa denda hivi ,au na mwanaume mahali? Ukianza kumfuata fuata mkeo na kuchunguza nyendo zake utaishia hapo ulipo ww na trust me si ww tu ni ktk ndoa nyingi.Hata baada ya ndoau tajikuta tu unapenda au kupendwa pia na naamini hata ww kuna wanawake wanakutaka mahali .Hapo sass
 
Kuna wakati nafikiria,nitafute nyumba ndogo.Lakini kwa jinsi navyo jijua , nikinogewa na mapenzi huko,sito weza jificha na ndo talisanua rasmi lijulikane,nimuache na nyumba na watoto.Nikaanzishe maisha mapya...
 
Watoto ni wangu hilo sina tatizo nalo.Damu nzito kaka,ingekuwa si wangu,yangesha julikana kitambo sana...
Basi fanya ngumu kumeza kaa naye kama dada na kaka kua bussy na mambo yako atapata wivu ajirudi mwenyewe
 
Duh kaka una moyo hongera sana kwa kuwa na Moyo huo,mim kitendo cha kumkuta na mesej za wanaume siku ya kwnza ningemfukuzilia mbali huwa sitak kbsa mtu acheze na hisia zangu maana ndoa sio mateso hasa kwa mtu uliekutana nae ukubwani tu,anyway hapo nahisi Mwanamke ndo kichwa cha nyumba.
 
Unajua hakuna mwanaume anaye weza kuvumilia haya,kinacho nichanganya ni kwamba.
Mara zote nilizo fuatilia sms,inaonyesha kama ana wazingua wanaume.Akiambiwa i love you,yeye ana jibu i love you two.
Sasa sijui nini kipo moyoni mwake,she mean it au anawajaribu Wanaume...
 
Sijawahi mkuta akifanya hayo.
Na kwa utaalamu nao fuatila simu zake,ningesha jua a to z ya chocho zake.
Maana njia nayo tumia ku trace ni ya kitaalamu sana,na deal na simu yake kupitia simu yangu.
Na naona sms na call list hata kama yuko wapi,pia hata picha nikitaka simu inampiga na natumiwa hapohapo.
Yeye anajua nime deal na makampuni ya simu.
IT tu.
Hii ina madhara maana nitashuhudia mengi sana labda atafute namba mpya na simu mpya na hiyo simu asinipe nikaigusa ...
 
Hata km unakipato kidogo,usijikatae lazima usimamie haki kuwa wewe ni kichwa cha familia hata biblia inasema hivyo..simama imara usiwe mdhaifu ndo atazid kukutesa,km kachok n ww fukuzia mbali,ww baki na watoto wako,tafuta dada wa kazi,then endelea kutafuta pesa kwa nguvu na ukiweka tumain kwa mungu utaona maish yatavyokuwa na amani
 
Mwanamke ukimg'ag'ania ndio kama umemzidishia kiburi achane nae mpe Uhuru yeye akiamua kuondoka aondoke kikubwa acha kushiriki nae kinyumba atakuua kwa maradhi
Haya.. akimwacha halafu wa tatu na wa nne naye akiyafanya hayo hayo aachane naye..?? Kuachana siyo suluhisho... utaacha wangapi?
 
Hapo kwenye kufukuzia mbali ndo pagumu.
Nyumba ambayo wewe ulimwaga trip 10 za mawe uka safiri kutafuta pesa,kurudi ukakuta kajichanga kaongeza trip tano na yuko busy ku process mkopo bank aendeleze,unaanzaje kumfukuza mtu na anaanzaje kuondoka?
Wanawake siku hizi sijui wamekumbwa na nn.
Nina rafiki yangu alichanganywa mpaka akaamua kubadili mpaka dini na kuoa upya...
 
Yesu alibebeshwa msalaba......kiimani alibeba thambi zetu.......upo hapo... kama mke na watoto ni dhambi sawa......tutawabeba......mbali na hapo ndoa ni matatizo ya kujitakia....
nimekuelewa....ila nimecheka pia
 
nadhani hujanielewa namaanisha asimuache for the sake of watoto na asijishughulishe nae kwa lolote afanye yanayomuhusu
kuna haja gani ya kuishi na mke ambaye sishughuliki naye kwa lolote?....watoto watakua tu hata bila mama.....furaha na amani kwanza
 
Sasa km unajua hilo kwann unakuja kutusumbua na ushauri,mwanaum kaumbiwa mateso kubali bas uteswe,hahahah eti unawaza tofali,mchanga,km hamna amani ya ndoa bas usitegemee furaha,watu wanaacha majumba na vitu vya thaman wanakimbia wanaon nyumba chungu ww unawaza cement ya dangote
 
Hujanielewa kk,kuna mtu ali post kuwa nimfukuzie mbali,nikawa namjibu kuwa ni nguvu kumfukuzia mbali kwa sababu hapa tulipo jenga pana mchango wake,labda mimi ndo niondoke...
Na ninaanza kufikiria hili la kuondoka ndio utakuwa muafaka...
Maana soon tampasua mtu atakapo zidisha dharau...
 
una mume unawezaje kuentertain kutongozwa jamani!!loohh!
pole hilo limbwata la Huyo Dada nahisi la msumbiji!
 
Muachie nyumba hiyoo si ya watoto kwani atauza?!!
kaa mbali kama miezi miwil hv km anakupenda kweli na una umuhimu wako atakutafuta tu na atajirudi!
Unawaza nyumba,wakati haina amani si moto huo!
We mwanaume pambana tu,utafika tu!
 
Muachie nyumba hiyoo si ya watoto kwani atauza?!!
kaa mbali kama miezi miwil hv km anakupenda kweli na una umuhimu wako atakutafuta tu na atajirudi!
Unawaza nyumba,wakati haina amani si moto huo!
We mwanaume pambana tu,utafika tu!
Mawazo mazuri
 
Watu kama hao hawapendi vikao vya usuluhishi me akiuchuna naye anauchuna vilevile matokeo yake anayeumia Me.
 
Watu kama hao hawapendi vikao vya usuluhishi me akiuchuna naye anauchuna vilevile matokeo yake anayeumia Me.
Bro!una moyo mwepesi sana, mimi mume wangu akijitia kuuchuna tu ujue kaumia maana ataisoma namba, hakuna sababu ya kuuchuna bila kukoseana na ndo maana mi huwa sipend kuuchuna na ukiuchuna nakupokea kijiti mpaka ukome
 
Bro!una moyo mwepesi sana, mimi mume wangu akijitia kuuchuna tu ujue kaumia maana ataisoma namba, hakuna sababu ya kuuchuna bila kukoseana na ndo maana mi huwa sipend kuuchuna na ukiuchuna nakupokea kijiti mpaka ukome
Kumbe tuko wote kimtazamo najua ke ni bingwa wa kuuchuna ndio maana nikasema atakaye umia ni Me
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…