Hicho ni kilio kutoka kwa Jamaa yangu mmoja, anadai imefika mahali wapo ndani ikisikika ngurumo ya gari mke anashtuka na kutamka 'Amos huyo' Jamaa anadai jirani huyo 'Amos' ndio yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha nyumba yake hiyo wanayopakana naye Jamaa ameendelea kusema, huyo (Amos) yeye wala haonekani kumshobokea mkewe, na pia ni mtu anayeonekana mstaarabu sana na mwenye heshima, mwenye uwezo wake na mara nyingi huambatana na mkewe na watoto wao wawili wadogo.
Jamaa anaomba ushauri afanye nini kwani ameshachoka na mwenendo wa mkewe, na hajui la kufanya.