Mke wangu anamshobokea jirani yetu

Mke wangu anamshobokea jirani yetu

Mwambie afanye kazi kwa juhudi na maalifa ajitume sana huku akimuomba mola wake amuafikishe kupata pesa ya kununua gari zuri zaidi ya hilo la Amosi naamini hapo shobo ya kumshobokea huyo itaisha na badala yake itahamia kwake
Kwa maelezo ya Jamaa wala hadhani kama tatizo ni mali maana nao si kwamba wamechoka kivile.

Tatizo anadhani ni muonekano wa Jamaa, Amos ni mtanashati na mapozi yake ya kibrazameni, cheni shingoni n.k..ili hali Jamaa hizo sio pigo zake kabisa.

Mpaka Jamaa anajuta kuwa jirani na Amos.
 
Hicho ni kilio kutoka kwa Jamaa yangu mmoja, anadai imefika mahali wapo ndani ikisikika ngurumo ya gari Mke anashtuka na kutamka 'Amos huyo'....Jamaa anadai jirani huyo 'Amos' ndio yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha nyumba yake hiyo wanayopakana nayo...Jamaa ameendelea kusema, huyo (Amos) yeye wala haonekani kumshobokea Mkewe, na pia ni Mtu anayeonekana mstaarabu sana na mwenye heshima, mwenye uwezo wake na mara nyingi huambatana na Mkewe na Watoto wao wawili wadogo.
Jamaa anaomba ushauri afanye nini kwani ameshachoka na mwenendo wa Mkewe, na hajui la kufanya.
Mshauri ampige mkewe
 
Kwa hiyo jamaa amekutuma uje useme humu ?, kwa nini asiseme mwenyewe ili tuone hisia zake ?
Sio kila Mtu yupo kwenye social media, ingawa siwezi msemea sana huenda yupo ila sio active sana mitandaoni.
 
Hiyo ndilo linalomkera Jamaa.

Wife anashindwa kuficha hisia zake ili hali wanafahamiana hata na Mkewe lakini Wife hana habari sana na Mwanamke mwenzake.
ukiona mpaka mtu anashindwa kuficha hisia zake, basi jua situation iko critical, huyo mke mahaba yamemzidi
 
Nafiri ahame hapo, mpaka aje kununua gari huyo mke atakuwa salama mbele ya Amos ?
Kwa maelezo yalivyo tatizo wala sio Gari au nyumba, hata wao wana Magari na nyumba ya kiwango tu.

Tatizo ni Amos kama Amos.
 
Kwa maelezo ya Jamaa wala hadhani tatizo ni mali maana nao si kwamba wamechoka kivile.

Tatizo anadhani ni muonekano wa Jamaa, Amos ni mtanashati na mapozi yake ya kibrazameni, cheni shingoni n.k..ili hali Jamaa hizo sio pigo zake kabisa.

Mpaka Jamaa anajuta kuwa jirani na Amos.
ikiwa hivyo ndivyo basi jamaa kakwama sana kamuowa mke asie katika yeye hivyo Atapata tabu sana asubiri tu kipigo cha kupigiwa
 
Ibn, ugumu uko wapi ?, hata kama iweje jamaa akihama hapo atakuwa ametengeza distance na kuweka mkewe salama
Ugumu ulipo ni kuwa yaonyesha mwanamke ni mshamba sana hivyo kwa maisha ya mjini mipango miji wako kila mtaa atahama mala ngapi ok sawa akiona ushauri huo unamfaa na auendee hiyo ilikua ni wasiwasi wangu tu
 
Back
Top Bottom