Mke wangu ana tatizo kubwa msaada please

Mpende sana mke wako kwani anahitaji upendo, mfanyie vile anavyopenda na pia kuwa rafiki yake akufuate wewe tu pindi anapokuwa na shida. Kiufupi unatakiwa uwe kioo pindi akutazamapo ajione katika kioo hicho.
 
hayo ulitakiwa kuyajua kabla ya kumuoa
 

Pole sana!maadam umegundua kosa ni hili basi jitahidi kutomgombeza na kumkemea!najua itakuwa vigumu kwako lakini jitahidi for the sake of ur marriage.

Pia jitahidi kumpeleka maeneo tofauti todauti ya kuvutia kubadilisha mazingira itamsaidia pia.Anza utamaduni mpya kumsifiasifia na kumpelekea zawadi kama maua mbalimbali.maua ni dawa pia .

Ukiweza mpeleke kwa prof Japhet mbobezi wa matatizo ya akili na mshauri mzuri sana wa mahusiano wewe kamuone kwanza mweleze hali halisi halafu siku mkienda jifanye kwa mkeo wewe ndo unatatizo unamuudhiushi mkeo unahitaji ushauri sasa mkifika pale atawahoji kila mmoja wenu kirefu hadi historia ya kila mmoja wenu then tatizo na ufumbuzi.

Mtapata kwa pamoja!nina uhakika utarudi hapa kukiri mabadiliko.session zake ni three hours per couple!na sio ghali kabisa yuko BOCHI hospital Mbezi kwa Msuguri alikuwa nje kwa zaidi ya miaka ishirini ndo amerudi last year.nakushauri kutokana na kupona binamu yangumy best friend too tatizo kama la mkeo na amesota miaka kumi ndoani.
 

Huu sio ushauri bora kwanini mpige kwani hakuna njia nyingine yakueleweshana mpka umpige huyu ni mtu mzima mwenzio na sio mtoto kusema utamfundisha kwa kumchapa kuna njia bora nyingi na sio kumpiga :angry:
 
Huu sio ushauri bora kwanini mpige kwani hakuna njia nyingine yakueleweshana mpka umpige huyu ni mtu mzima mwenzio na sio mtoto kusema utamfundisha kwa kumchapa kuna njia bora nyingi na sio kumpiga :angry:

Si Wote Wanaeleweshwa Kwa Upole. Ukiwa Mpole Anakupandia, Na S Wote Wanaeleweshwa Kwa Ukari, Una Angalia Upepo Wake Ndo Mana Akikosolewa Anaongea Naneno Mia. Huyo Anahtaj Awe Mkal Kdogo
 

Kamwe katika maisha yangu sitanyanyua mkono wangu kumpiga mwanamke,na Mungu anisaidie.Pia kumpiga mtu mzima ni kukosa akili.
Anachopaswa kukifanya mleta mada ni kuwa karibu zaidi na mkewe,kumfanya amuone yeye ndiyo kimbilio lake, matatizo ya Kisaikolojia kamwe hayatatuliwi kwa ngumi!
Ni vyema kuanza kwenda naye out mara kwa mara, na outings hizo km ni mkristo zihusishe sehemu zenye concert za nyimbo za injili,lkn pia na kwenye maombi.
Anahitaji Amani ya Moyo, na ili aipate lazima Asamehe.Only good moments will make her realise that.
Yapo mengi ya kufanya,ila kubwa ni kuwa rafiki yake anayemwelewa matatizo yake na kuyatafutia suluhisho lisilo na negative impact!
Kuna siku atafunguka na Kuachia yote yaliyo moyoni!
 

Mnh huyo uliyemquote umeitoa wapi mkuu?
 
Pole sana mkuu, Sema tupo TZ kwa wenzetu mkeo ana matatizo ya kisaikolojia. Mimi nashauri muwaone wataalamu husika kwani wahenga walisema "mficha uchi maradhi humuumbua". Kila la kheri.
 
Kama ni stori ya kweli..niPM nikupe contacts za Psychologist amsaidie. She needs a professional help!
Niko pamoja na wewe katika hili chief wangu. Ni msaada wa mtaalamu wa saikolojia pekee ndo utakaomsaidia mke wa jamaa.
 
Niko pamoja na wewe katika hili chief wangu. Ni msaada wa mtaalamu wa saikolojia pekee ndo utakaomsaidia mke wa jamaa.

Mnataka kumlia tu hela huyu mkaka,tatizo la mkewe sio kubwa kihiivyo lol azidishe upendo,ampe compliments za mara kwa mara,amshirikishe kwenye mambo yake then ataona signifficant change 💃💃💃💃💃💃💃💃
 

Pole sana kwa hayo majanga. Kwakuwa umelijua tatizo la mkeo ni kuwa anajiona hathaminiki la kufanya ni kucheza na akili yake,toa time yako nyingi kuwa nae, mtoke out, muangalie movie pamoja za mapenzi za kuchekesha.

Ili kuleta bond kati yenu Pia itasaidia kuwa na story ya kupiga nae mara unapo kuwa nae. Vijizawadi ni muhimu ili kuamsha tabasamu lake na furaha yake, si lazima iwe ya gharama kubwa sometimes hata kitu cha 5000 kinatosha kumchangamsha mwanamke.

Punguza kumfokea, tafuta njia tofauti ya kumuelezea makosa yake, unaweza kuwa unafikisha ujumbe huo kwa utani.
Just mpe furaha na upendo, kwa kifupi atakuwa sawa.
 
Kijana Kwanza pole kwa changamoto inayokukabili, fanya yafuatayo kurekebisha, muache akosee mara 2,3 alafu msubiri akiwa Kwenye mood mchape bakora kali hakikisha anaifurahia akishatosheka mwisho kabisa msomee mashtaka yake kwa upole alaf mwambie alipokosea, then mnyuke tena bakora ya mwisho, atakaa tu mstarini huyo.
 
Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha japo kufuatilia na kuamua kutafuta suluhu ya hili tatizo. Kama ungeanza kuwaza kua na mwanamke mwingine ndio ingekua mwanzo wa ndoa yako kuharibika. Kama kweli nia yako ni kutafuta suluhisho la tatizo la mkeo, nna imani kwa kiasi kikubwa kwamba utafanikiwa.

Jambo la kwanza ni lazima umweleze kwa upole kwamba unampenda kwa dhati lakini haufurahishwi na hiyo tabia yake ya kutokupenda kukosolewa. Mweleze jinsi inavyokuweka katika wakati mgumu na ajue kwamba haumchukii yeye bali ni hiyo tabia.

Pili ni lazima awasamehe na aachilie hao waliomtendea ukatili, bila kufanya hivyo hilo jambo litaendelea kumsumbua sana. Atakua anaishi maisha ya kuigiza tu, anasumbuka au kuogopa kitu kisichokuwepo ki uhalisia, kipo kwa kufikirika tu. Kwa mfano hapo anaona unamnyanyasa wakati ki ukweli wewe unahangaika kutafuta suluhu.

Utakosea sana kama utaamua kumuacha anapokosea bila kumkosoa kisa unaogopa atajisikia vibaya, utatengeneza maisha ya kisanii yasiyo na uhalisia.

Mwisho wa yote UPENDO huvumilia yote na hauhesabu mabaya, mpende mkeo mkuu!
 
Nimefurahi kuwa hujamkatia tamaa mkeo ingawa ushamkon'gota vya kutosha. Kwa kuwa ushajua tatizo suluhisho kubwa hapo ni moja tu:

Mkeo kuwasamehe ndugu zake hasa yule aliyemlea toka utotoni maana ndiye aliyepanda mbegu ya kutokujiamini kwake. Akisamehe anaweza kuanza kuamini kuna kupendwa maana watu wa aina hii wakipendwa wanakasirika.

Akili zao zinataka manyanyaso. Ukimsifia anafikiri unamkejeli, ukimkosoa anaona unakuwa kama shangazi yake, ukimpa zawadi anaona humaanishi anaona unajipendekeza baada ya kumuonea.

Njia ya kuwasamehe watesi wake ni rahisi kuliko ya kwenda kwenye sessions za wanasaikolojia ambao hawana muda wa kutosha, na wengine hujifanya wanajua sana kumbe wamekariri tu, na bado utatakiwa kulipa. Akikubali ana tatizo na akaweka nia ya kupona akatangaza msamaha toka moyoni atashangaa namna atakavyobadilika.
 
Dawa !! Mkuu nitonye kwa dawa na tiba ya haraka zaidi ni bora muende Vacation, mutoke nje kwa matembezi !! mtarudi na mawazo mengine ya kimaisha!!
 
Last edited by a moderator:
Matatizo ya kiakili yana ugumu sana kutatua, ni kitu kilijengeka kwa mda mrefu, sio rahisi kukiondoa kwa siku moja au mwezi mmoja.

Kama alivyosema Riwa, tafuta wataalamu wa maswala hayo, wala usiogope, mueleweshe tu kuwa anahitaji wataalamu wa maswala ya saikolojia ili kumrudishia hali yake ya kawaida.

Lakini pia, kuwa mpenzi na rafiki yake...ongeza upendo!!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo lako dogo sana.

Haumridhishi, Haumfikishi.

Jitahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…