Mke wangu amenisaliti 'live', naombeni ushauri wenu tafadhali

Nakubaliana nawe ila inamlazimu shemeji yetu kuacha kazi huko,kwa sababu mbili kwanza kuwa karibu na mumewe ikiwezekana atafute kazi karibu ama mume amtafutie biashara yoyote afanye pili asiende kuonana na hao watu waliompelekea kusaliti ndoa yake
Kweli kabisa moja ya mambo yanayoweza kusaidia kuokoa hiyo ndoa ni pamoja na mke kuwa karibu na mumewe na ikiwezekana aache kazi kabisa.
 
Mkuu Ngoshwe, huna Mke hapo
Hata kama unasamehe, utakuwa unasamehe nini

Hivi kweli huyo mtoto ni wako?, maana ni ajabu kama mtoto bado mdogo na mama keshaanza kuigawa nje, au labda ndio alikuwa anampa baba wa mtoto

Huyo mwalimu ni msaliti na usaliti wake unatokana na wewe mwenyewe, huwezi kuwa na mtu ndani ya nyumba anafanya kazi lakini hujui anapata pesa ngapi na anaatumiaje pesa yake

Huwezi kuwa na Mke ndani anakuambia naama na kila kitu kipo tayari na hataki kupelekwa na wewe na wewe unakubali,

Kwa huyo mwanamke kama kila kitu alikuwa anapewa na alikuwa anaishi maisha ya furaha tu inakuwaje anatoka nje? hana mapenzi na wewe kabisa na hata ukimsamehe haita saidia keshaonja asali na keshachonga mzinga, hawezi kutulia kamwe

ushauri wa maana
1) Kwenda kupima Ngoma
2) Kupima DNA ya Mtoto
3) Kuachana na huyo mwanamke
 
Baba, pole na matatizo!
Nashindwa kuamini, ina maana huyo mchaga wa kimara baruti anaitumia na kuisasambua kiasi cha kuchoka ndani ya mwezi mmoja tu?! Ina maana wewe ulikuwaga unabofya tu
?
king'asti kama ulikuwa kichwani mwangu.
K bana ni kama barabara ya lami gari likipita haliachi alama, sasa huyu mtoa mada mbona anataka kutufunga kamba?
 
ptuuuu! Hapo anamtoto mchanga miezi6 hana huruma hata kwa mwanae? We kibilia angaza ukijikuta mzima mwache akae hukohuko kibaha aendelee 0kufukunyuliwa v izuri hapo
ndio vizuri kashajitenga mwenyewe.
 
Mkuu pole sana! Ingawaje haimezeki kwangu kumeza but possible haya mambo yapo! mkuu hakuna kitu kinachoudhi kama kukili kwa mwanamke kirahisi tu, bora asingekili, jitahidi umpe adhabu ya kutosha ili ajue umeumia usimsamehe kilahisi mkuu!
 
Nihitaji ufafanuzi kidogo ikulu ikitumika ndo inakuaje? Maana nadhani biolojia imekupiga chenga kidogo hapo, au umechanganya effects za uzazi ndani yake.
 
Ni rahisi kusema hivyo "MSAMEHE TU". Jamani hili donda haliponi hata ufanyeje! Afu kikubwa zaidi ni kuwa huwa sio rahisi wezi wa wake/waume za watu kuachana.
Kuna jamaa yangu aligundua kuwa mkewe anamegwa lakini hamjui! Akaanza kufanya 1+1 akajua kwa kuunganisha dots! Kumbe kila wakati walipokuwa wakikwama wife alikuwa anamshauri aende kwa mzee fulani kwenye mji waliokuwa wanaishi na mzee alikuwa anatatua shida zao fasta! Walihamia mkoa mwingine! Wife akawa ana safari za mara kwa mara kwenda mkoa ule aliokuwa anaishi mwanzo kwa kisingizio cha kufata vitu vya bishara.
Siku moja jamaa akachomeka (ingawa hakuwa anauhakika kuwa ni kweli) kuwa amekwishajua mahusiano na yule mzee!
Wacha mama aangue kilio! Ooo ni ibilisi tu! Naomba unisamehe mme wangu! Sitorudia tena! Akamsamehe maisha yakaendelea kwa masharti kuwa hakuna tena kusafiri wala nini! Kilichofuata kinauma zaidi yaani mke alimzalia jamaa mtoto anyefanana kila kitu na mwizi wake! Ngoma ilikuwa balaa! Ilibidi wife aeleze kila kitu! Eti yule mzee alikuwa anakuja huko walikohamia na mwenye nyumba akienda kazini jamaa anajibanjulia tu mpaka wakapata mtoto. Yalimsinda wakaachana. Sasa ni miaka kadhaa, yule mzee hamtaki tena yule mke wa mtu! Mke yule hana kazi tena! Jamaa keshamchukua yule mtoto wa kwanza tena baada ya kupima DNA.

Kwa suala hili n la kwako pia! na hata wengine!
Jaribuni kujua mwenzi wako anataka nini katika mapenzi! Kujificha na kudanganyana kwenye mapenzi no mojawapo ya chanzo cha cheater wengi! Utakuta aina ya mapenzi unayofanya kabla ya kuoa/kuolewa huyapati kwenye ndoa! Hisia huanza polepole kurudi kwa wapenzi wenu wa zamani na hapo ndo huanza kuwatafuta hao wa zamani! Eti ya kale hayanuki! Jiachie kwa mkeo/mmeo! Ukiogopa kuitwa malaya ama mhuni yatakupata haya haya tu!

Mwisho ndugu nyangu uamuzi unao wewe mwenye maana ndiye utakaye yaishi hayo maisha! Ila mpaka umeamua kusema K ya bi mkubwa sio tena basi ujue kuwa hata ukimsamehe naona utatafuta K ya saizi yako na huo utakuwa mpasuko mkubwa kwenye familia yako. Tafakari na uchukue hatua!
 
Na huyo mkewe kakiri baada ya mchaga kuanza kumchoka, kaona apate relief kwa mme wake.
Ndo raha ya wake za watu, mkilizana anaenda kumaliza machungu kwa mumewe.
 
Kila kitu kimtokeacho mwana wa adam hapa duniani ujue kina makusudi yake,mshukuru mola kwa kugundua hilo mapema,kwa kuwa amekiri kosa mwenyewe,msamehe,mwambie mbele yako ampigia simu huyo jamaa na aweke loud speaker na amwambie kuwa kuanzia leo hamtaki kwa kuwa amemuharibia ndoa yake na aifute namba yake mbele yako na abadilishe laini ya simu,mpime VVU,mfuatilie kwa karibu kuhusu tabia zake na akiwa habadiliki pamoja na hayo yote sasa unaweza kuchukua hatua ya kumuacha manake anaweza hata kukuua huyo,pole
 
MM pole ndugu yangu .Mimi sina cha kukushauri kwa kuwa wewe ndio unajua unavyofeel na ulivyoumia ila kaka yangu nitakuombea ili uweze kusamehe na muanze maisha upya ya ndoa na kumtunza mtoto wenu kwa mapenzi ya baba na mama
 
Pole sana ndugu,
Hizo ndizo changamoto za mahusiano. Najua hapa kila mmoja atashauri la kwake lakini wewe ndiye unayepaswa kutafakari na kufanya uamuzi unaoona ni wa faida kwako, mwanao na mkeo. Pamoja na faida uamuzi huo ukuwezeshe kupata suluhisho la kudumu. Binafsi nakushauri ufanya haya:

1. Zungumza na mkeo; kwa kuwa amekiri kosa na kuomba msamaha ahame Kibaha na arudi home (Dar). Mara nyingi kuishi mbali na mwenzi kuna vishawishi vingi sana. Hili mnalifanya kutokana na kuwa dalili zimejionesha wazi kuwa kua udhaifu. Kuishi pamoja kutakuondolea wasiwasi wa kuwa "huenda anakusailiti" pindi akiwa Kibaha.

2. Mkiwa na mkeo fanyeni ibada ya toba kwa pamoja (kama mtaona vema mnaweza kumshirikisha kiongozi wenu wa dini)
Binafsi ninaamini kuwa ni Mungu pekee aletaye msamaha wa dhati na ujasiri wa kushinda dhambi.

3. Ni vema mkashauriana na mkeo mkaenda kupata ushauri na kupima VVU ; utaniuliza why? Kupima VVU hakuna maana kuwa baada ya kukuta majibu tofauti na matakwa yenu muachane, la! Kupima kutawawezesha kufahamu hali yenu ya maambukizo na kuamua ni kwa namna gani mtaishi bila kuambukizana na kama wote mko salama kufahamu namna gani mtaishi bila kupata maambukizi.


4. Fanya utaratibu wa mkeo kupata kituo cha kazi hapo Dar; najua itachukua muda lakini ni vema kushughulikia uhamisho huo.

Hili la mwisho ni ushauri kwako; si vema sana kuanika madhaifu ya mwenzanko hadharani. ninaposema hadharani naamanisha mahali kama jukwaa hili. Ni rahisi kudhani hakuna anayekufahamu kwa kuwa wengi tunatumia majina bandia; ukweli ni kuwa yamkini wawili watatu wanakufahamu na huenda wakamfahamu hata mkeo. Unaongeza watu wa kumdharau mkeo na kutomuamini. Najua haya ni maumivu makali sana; lakini ni vema kuwashirikisha aidha wadhamini wenu wa ndoa, kiongozi wa dini au wazazi (kama unaona vema na unawaamini watakushauri vema); kinyume cha hapo mara zote jaribuni kumaliza tofauti zenu kwa kutafuta suluhisho ninyi wenyewe!

mchana mwema


EJL
 
mimi mawazo yangu ni haya;
kwanza kwakuwa umemuoa mtafutie shule karibu ya nyumbani unapoishi kwakuwa hata serikali inakubali kufanya uhamisho wa namna hiyo ili mradi tu uwe kweli kwenye ndoa na vyeti vinaonekana, pili kuwa karibu nae kujua hela zake anapeleka wapi ilo ni muhimu kwakuwa maisha ya sasa ni magumu si ya upande mmoja hata km anakazi nawe unakazi lakini kwakuwa wote mnajenga nyumba moja basi hakikisha unajua kinachoendelea, tatu na mwisho hakikisha weekend pamoja na siku za sikukuu mnakuwa pamoja katika shughuli zenu either mnaweza toka kwenda sehemu kufurahia pamoja km beach na sehemu nyingine huku mkibadilishana mawazo hapo kaka utakuwa umejaribu kuleta upendo karibu yako.
ni hayo tu kwangu.
 
Huo mtihani mkubwa ndugu
yangu. Hapo nakushauri umrudishe tu hapo Dar uishi naye akiendelea
kuishi peke yake huko Kibaha ataendelea kukusaliti.

Inasikitisha sana kwa kweli ila kama ataamua kumsamehe hatua ya kwanza iwe ni kuhakikisha anamrudisha Dar ikibidi hata kazi ahamie Dar hata private kama atakosa uhamisho.
 
Ndoa = ccm. Full longo longo. Kasema mwenyewe kwa kinywa chake kwamba kaingiliwa na kidume kingine kwa hiari yake mwenyewe = tabia yake. Hakuna sababu ya kusamehe hapo, piga chini, kama atakuachia watoto usioe tena mpaka wawe watu wazima.
 
Pole kwa yote yaliokukuta! ikiwa moyo wako URADHI kusamehe na KUSAHAU kuwa yaliopita sindwele, basi msamehe na usahau ingawa ni ngumu kwaninyi wanaume kusamehe, jenga familia yako kwa upendo ukiwa na mwenzi wako.

Dunia ya sasa imebadilika sana na haya mambo yapo sana kwenye ndoa nyingi, wapo wanaomba ushauri kwa kusema hadharani wapo wanaogumia moyoni kwa kuogopa kusemwa na mengine mengi.

Uamuzi mkubwa ni wako ila na kushauri umsamehe na wala usije fanya hasira ya kulipizia kwa wengine nje hapo utakuwa hujengi bali unabomoa, ni dhahiri mwanamke akikiri kosa na akiapa kutorudia huwa anamaanisha moyoni.

pole kwa yaliyokukuta, ila hajakusaliti LIVE umehisi
 
piga chini huyo, dharau alokuonesha ni ya hali ya juu. na wala si mwaminifu,je usingeuliza angekuambia? mwache aendelee na huyo aliyemuona wa maana zaidi yako. she should pay for her acts not just walk away with it.

kama ni mimi ningemtema jumla, kumwonesha kwamba i can do without her.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom