Mke wangu amenisaliti 'live', naombeni ushauri wenu tafadhali

Duh, pole mkuu..wanawake hao...sisemi ningefanya nini...maana uamuzi wangu labda ungekuwa sahihi kwako
 
Duh pole!! wewe mchaga nini? huko Moshi wanatabia ya kupenda kufumania wake zao kwa kupanga na kuwa du wahanga wao, lkn wanawasamehe hao wake zao nami nakushauri msamehe mkeo bila masharti au kupanga fumanizi na kujilipia kisasi kwa mtindo wa Moshi bora utumie mtindo wa Tanga kuondoa hicho kiungo anachotumia kutembelea wake za watu!!!!
 
Baba, pole na matatizo!
Nashindwa kuamini, ina maana huyo mchaga wa kimara baruti anaitumia na kuisasambua kiasi cha kuchoka ndani ya mwezi mmoja tu?! Ina maana wewe ulikuwaga unabofya tu?

Natamani ungeangalia nafasi yako kwenye kusimamia nyumba yako.
1 humuulizi mkeo hela yake anapeleka wapi. Je, ulishawahi kuwaza anatumia kiasi gani cha kipato chake kidogo cha ualimu kwa nauli na chakula mchana? Je anachoka kiasi gani kutoka umbali mnaoishi na kibaha? Ulishajaribu walau kumsaidia ahamie karibu ama kupangisha nyumba yenu na nyie kuhamia kibaha ama kibamba ili asiwe mbali sana na kazini?

2 pamoja na mkeo kuwa mnunaji, ulishawahi kuvunja ukimya hata kwa hisani yako? Unasema hujapewa unyumba muda mrefu; ulishawahi kujadili na mkeo na kumjulia khali kama yeye anapata wapi unyumba kama nyumbani haupatikani?

3 Funga kazi ni mkeo kukuambia anataka kuhamia karibu na kazini, chumba na kitanda na godoro tayari na wewe kuona ahueni! Na unaacha mkeo na mwanao kuhamia tena kwa basi mahali usipopajua! Kwa hela usizozijua?!

Pole kwa kukupa dawa chungu! Ukijitathmini ulipokosea utajua jinsi ya kushona na kuweka viraka koti lako.

Eeh bwana, wee kweli umemkomesha uyu *****,mi naweza sema yy ndio sabb ya kila kitu,hivi karne hii bado kuna wanaume wa dizaini hii kweli,et sijui ela zake anapeleka wapi,eti mi nimuache tu ubungo atapanda basi,!!!!
 
Ndugu zangu wana JF,

Mke wangu ni mwalimu wa sec, ana mtoto mdogo wa miezi 6, toka ajifungue vituko vilikuwa haviishi....kuninunia daily sometimes hadi 3 weeks or mwezi. Nilipoona mambo yanazidi nilimrudisha kwao kwa muda kama wa mwezi mmoja hivi kwa sababu alikuwa ana maternity leave. Hata hivyo nilijua huenda postnatal period ndio inamfanya awe vile hivyo kwangu nikaona ni busara kuwa mpole ili kuepusha shari.

Aliporudi kutoka kwao tuliishi kwa maelewano mazuri kwa muda wa wiki moja tu, then yakarudi yale yale...ful mnuno kwangu lakini stori nyingi tu kwa mashost zake na majirani.

Mke wangu anafundisha kibaha, na tulikuwa tunaishi sote Dar sababu ndiko nilikojenga kibanda chetu cha kuishi na pia mimi ndiko ninakofanyia kazi. Mwezi uliopita nilishangaa mke wangu kuniambia kuwa yeye anataka kuhamia kibaha ili awe karibu na kituo cha kazi, pili ili aweze kupunguza gharama za usafiri za kila siku. Ikumbukwe kuwa ameanza kazi toka February 2011 na mimi siulizii mshahara wake anafanyia nini yeye ndiye ajuaye....but baada ya hoja yake hiyo nikajiuliza apunguze gharama za nauli....? je hela anafanyia nini? sikutaka ugomvi nikamruhusu lakini nikamuuliza vipi kuhusu maandalizi akasema kila kitu kipo sawa...chumba, kitanda+godoro na mahitaji mengine yote.

Ameondoka tarehe 04 June kuhamia kibaha, nikamwambia nitampeleka na gari hadi kibaha alikataa kata kata na kusema nimuache tu ubungo atapanda bus. Pia aka-haidi weekend atarudi lakini hakurudi na bila kutoa sababu. Ijumaa ya juzi amerudi home but still hakuwa mchangamfu, pia kuonekana kama ana chuki nami.

Kwa kuwa ni muda mrefu sijapata unyumba na yeye ndio mke wangu usiku wa kuamkia leo nikaomba haki yangu,.....WANA JF HAMUWEZI KUAMINI LAKINI NAWAAMBIA UKWELI....Nimekuta ikulu ya mke wangu imetumika kiasi cha kutosha saana hadi kiasi kwamba nilipatwa na mshangao wa ajabu....hiyo ilikuwa round ya kwanza, nilipojaribu ya pili...nilishindwa kumaliza game...coz sio K bali ni hatari. NILIUMIA SANA.

Toka saa 8.30 usiku sijalala hadi saa 10.30 usiku/alfajiri, niliamua kumuuliza tena kwa upole huku nimemkumbatia....kuwa huko kibaha ana wanaume ana-do nao!Alikataa kata kata....but alipoona naongea kwa upole sana akaingia kingi na kusena ndio anakiri ...lakini ni mwanaume mmoja tu ndio anatembea nae lakini sio wengi. Nikahoji ni nani huyo? nikaambiwa ni mfanyabiashara, anakaa kimara baruti, mmeanza toka lini mahusiano yenu....akasema toka...mwezi uliopita, mlifahamiana wapi.....tulifahamiana kwenye bus wakati naenda kazini.

Baada ya hapo akaanza kuliaaa.....na kusema anaomba nimsamehe!Nikamuuliza uliomba ruhusa ya kuhamia kibaha ili uwe huru? Je umekosa nini kwangu au mimi nilikuwa sikutoshelezi? akajibu hapana!

......WANA JF am so sorry kwa maelezo marefu but nimechanganyikiwa na simuelewi mke wangu. Anataka nimsamehe, but kabla sijachukua maamuzi nimeona ni vema niwashirikishe nyie ndugu zangu ili niweze kujiridhisha kwa uamuzi nitakao uchukua baada ya kupata maoni yenu.

NARUDIA TENA.....SAMAHANI KAMA MTAKWAZIKA KWA KUSOMA MAELEZO MAREFU...!

Ni mimi NGOSWE.120




Mkapimane, Msamehe and Muonmbe Mungu akupe Nguvu ya Kusamehe Kabisa!!! All the best
 
Pole sana Mkuu!!!
Nikamuuliza uliomba ruhusa
ya kuhamia kibaha ili uwe
huru? Je umekosa nini kwangu au mimi nilikuwa
sikutoshelezi? akajibu
hapana!


Hebu Mpe SECOND CHANCE lakini hii nafasi ni kwa ajili ya kumchunguza pekee na kwenda kupima... Maana kama ni kweli anataka msamaha hata Rudia ila kama Ataendelea tafuta Usitarabu mwingine kabla hayajawa makubwa na Kukuletea UKIMWI/STD's nyumbani

Hakuna mke hapo. Binafsi sioni sababu za kujiingiza kwenye kazi ya ziada ya kuanza kumchunga mtu kama mbuzi, mwisho siku utaanza kupata maugonjwa ya kisukari kwa sababu za mjinga mmoja. Ushauri wangu.. chukua maamuzi magumu mzee. Maisha yapo tu, utapata mke mzuri ambaye atakuheshimu kwa dhati.
 
Huyo kakusudia kabisa kukusaliti tena kwa nguvu zote hakika kama ingekua kanifanyia mimi huo upuzi hata nicngetaka ushauri kwa mtu yoyote..
 
Japo 'ngumu kumesa' lakini....kwani 'sisimizi' wakiingia kwenye kopo lako la sukari unaimwaga yote kwa hasira!? Si unakung'uta tu wanatoka nduki, kisha unaendelea 'kulamba' sukari yako tar'tiiib!
 
Pole kwa yote yaliokukuta! ikiwa moyo wako URADHI kusamehe na KUSAHAU kuwa yaliopita sindwele, basi msamehe na usahau ingawa ni ngumu kwaninyi wanaume kusamehe, jenga familia yako kwa upendo ukiwa na mwenzi wako.

Dunia ya sasa imebadilika sana na haya mambo yapo sana kwenye ndoa nyingi, wapo wanaomba ushauri kwa kusema hadharani wapo wanaogumia moyoni kwa kuogopa kusemwa na mengine mengi.

Uamuzi mkubwa ni wako ila na kushauri umsamehe na wala usije fanya hasira ya kulipizia kwa wengine nje hapo utakuwa hujengi bali unabomoa, ni dhahiri mwanamke akikiri kosa na akiapa kutorudia huwa anamaanisha moyoni.
 
Baba, pole na matatizo! Nashindwa kuamini, ina maana huyo mchaga wa kimara baruti anaitumia na kuisasambua kiasi cha kuchoka ndani ya mwezi mmoja tu?! Ina maana wewe ulikuwaga unabofya tu? Natamani ungeangalia nafasi yako kwenye kusimamia nyumba yako. 1 humuulizi mkeo hela yake anapeleka wapi. Je, ulishawahi kuwaza anatumia kiasi gani cha kipato chake kidogo cha ualimu kwa nauli na chakula mchana? Je anachoka kiasi gani kutoka umbali mnaoishi na kibaha? Ulishajaribu walau kumsaidia ahamie karibu ama kupangisha nyumba yenu na nyie kuhamia kibaha ama kibamba ili asiwe mbali sana na kazini? 2 pamoja na mkeo kuwa mnunaji, ulishawahi kuvunja ukimya hata kwa hisani yako? Unasema hujapewa unyumba muda mrefu; ulishawahi kujadili na mkeo na kumjulia khali kama yeye anapata wapi unyumba kama nyumbani haupatikani? 3 Funga kazi ni mkeo kukuambia anataka kuhamia karibu na kazini, chumba na kitanda na godoro tayari na wewe kuona ahueni! Na unaacha mkeo na mwanao kuhamia tena kwa basi mahali usipopajua! Kwa hela usizozijua?! Pole kwa kukupa dawa chungu! Ukijitathmini ulipokosea utajua jinsi ya kushona na kuweka viraka koti lako.
Tatizo wanawake wa siku hizi anacho tafuta yeye yaani kipato kinakuwa chake ila anacho tafuta mwanaume kinakuwa chawote
 
Thread kama hii bila kusoma michango ya MwanajamiiOne Kongosho King'asti Mbu, TIMING na gfsonwin huwa nakosa cha kuchangia kabisa.

Inawezekana ikawa mke wangu ananicheat lakini sijui.... better that way.
Inawezekana nikahisi kuwa ananicheat tokana na mabadiliko ya tabia, siyo mbaya sana.
LAKINI: Anakiri kwa kinywa chake kuwa ANANICHEAT maana yake ni kuwa anataka nifanye maamuzi magumu ya kuachana naye. Na kwangu mie thats the best option. KWANI NINI BANA.

Kishakiri kwa KINYWA chake kuwa kuna jamaa linamvua chupi kwa hiari yake...!!! Oh God!! Afu nimsamehe turudiane?? Yaweza tokea lakini things will never be the same. So What? Oh My Lord Please Help Me.

Mwisho wa Comment.
 
Last edited by a moderator:
Usichukue uamuzi wowote sasa, probably uko na hisia sana sasa, ushauri wangu ni kumrudisha mkeo kwa muda kwao huku ukiwaza kwa kina mustakabali wa uhusiano wenu. Hapo sasa utaweza kung'amua vizuri mwenendo wako na wake nani alichangia mahusiano yenu ku deteriorate.
All things considered, huwezi kuondoa fact ya mkeo kukusaliti ni kitu kigumu ku overcome......unaweza kuishi na mtu aliyekusaliti? Hapo ni wewe mwenyewe kuamua
 
pole sana mdau. Ila kwa mtazamo wangu naona haina haja ya kumpa talaka mkeo. Cha msingi tumia upole na umrudishe nyumbani. Mpaka akakubali kuolewa nawewe nikweli amekupenda, ila tamaa yawezekana zilimzidi, naye ni binaadamu. Usibadilike kwa chochote. Endelea na huduma zako na majukumu yako kama baba na muonyeshe upendo. Hapo atakuwa kapata fundisho
 
ptuuuu! Yani mkeo ana mtoto mchanga miezi 6 tuu kashaenda kufukuliwa kiasi hicho mpaka mwenyewe umeona mashine0haifai?
Tena kakutana naligumegtume lisilo0ogopa wake za watu teeh nalimemfu
kunyua haswa lo0
kwahiyo kama ni kwenye mtandao umeshaingizwa, nakushauri ustopishe kale
kamchezo baada ya miezi mi3 kimbia angaza ukijikuta
salama mshukuru mola wako na huyo mkeo mwache akae hukohuko kibaha mojakwamoja
 
Hapa parefu
Labda tumsubiri Babu Dark City alete busara zake

Ila kwa wanamme wa kitanzania hii ilokupata ni sawa na morani kuliwa na samaki, bowa aliwe na simba Source Mr. Ebbo

Yaani ataishije maisha ya wsi wasi? Hasa akiaga anaenda Kimara?

Mlazimisha akakuonesha mgoni wako ili ujipema kama unafika bei au uachie ngapi.

Ujumbe: mahawara hawaachani.

Thread kama hii bila kusoma michango ya MwanajamiiOne Kongosho King'asti Mbu, TIMING na gfsonwin huwa nakosa cha kuchangia kabisa.

Inawezekana ikawa mke wangu ananicheat lakini sijui.... better that way.
Inawezekana nikahisi kuwa ananicheat tokana na mabadiliko ya tabia, siyo mbaya sana.
LAKINI: Anakiri kwa kinywa chake kuwa ANANICHEAT maana yake ni kuwa anataka nifanye maamuzi magumu ya kuachana naye. Na kwangu mie thats the best option. KWANI NINI BANA.

Kishakiri kwa KINYWA chake kuwa kuna jamaa linamvua chupi kwa hiari yake...!!! Oh God!! Afu nimsamehe turudiane?? Yaweza tokea lakini things will never be the same. So What? Oh My Lord Please Help Me.

Mwisho wa Comment.
 
Last edited by a moderator:
Dah Inasikitisha sana.

Kweli kama walivyosema hapo juu isingekuwa ndoa hapo ungemwambia tuu mama hebu jiondokee utafute mtu mwingine ila kwa kuwa kuna ndoa mkuu hayo ni masuala ya ndani ya ndoa.

Mkuu kuna mengi ambayo ni makosa kwako ambayo ulipaswa ujiulize kabla ya hata kukubali wazo lake la kuhamia karibu na kituo cha kazi.

Huo ulikuwa sio uamuzi wake mwenyewe ni lazima mshirikishane na mkubaliane.

Sio yeye aamue tuu kutoka huko alikotoka aje akupe uamuzi wewe na wewe ukubaliane nao bila kuhoji.

Ulipaswa umwambie wazi kuwa uamuzi kama huo ni wa familia na baada ya majadiliano na sio wa kuja kuniambia baada ya wewe mwenyewe kuamua.

na inaonekana alikuwa kashafanya kila kitu wewe ulikuja kuambiwa mwishoni maana kama ni kitanda, godoro, vyombo vya ndani vilikuwa tayari.

Mkuu naona zaidi hapo kuna lililojificha ambalo mkeo ameshindwa kukuambia kwa muda mrefu.

Hebu tafuta nafasi na muda wako uende nae mahali uanzishe mazungumzo ambayo yatafungua moyo wake kukueleza nini kinamsibu na ana nini moyoni mwake mpaka aamue kukusaliti na kuchukua maamuzi ambayo yalipaswa yacchukuliwe na nyie kwa pamoja
 
hata Jesus alikiri kwamba isipokuwa kwa uzinzi mengine yoote umsamehe mkeo.....I'm out.....fikiria then toa maamuzi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom